Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Mfano upo nimeshakutolea ila wewe umeamua tu kubisha

Pale uliposema yule jamaa aliyesafiri kutoka Mbeya to Dar kwa miguu alikuwa anatafuta sifa tu niliona nikuache hivyo hivyo ila sasa naona unataka nikurudishe tena kule kule

Ni binadamu gani anayeweza kurisk maisha yake kusafiri umbali wa karibu KM 1000 kwa miguu kwa takriban wiki mbili ilihali anajua hakuna chochote anacholipwa eti ili tu kutafuta sifa
 
Inabidi akasome historia.. ndio ataelewa safari za miguu zipo nyingi, mfumo wa maisha ya sasa ndio unataka kutuaminisha kuwa bila gari au pesa huwezi safari
 
Nisaidie kumshangaa huyo ndugu yako anayetudanganya eti mtu hata ukijichanga kwa miezi kadhaa baada ya kujibanabana ukapata ka laki kako ukasema utoke Dar hadi Tanga tu hapo kuosha macho basi tayari wewe ni tajiri
 
Wewe unaona yupo timamu?
Halafu huyo jamaa alisafiri kwa ajili ya mechi,hakusafiri kwa sababu anataka ajifurahishe tu kutembea hadi Dar na kurudi.

Ongezea na wengine ambao huwa wanasafiri tu kwa miguu mikoani na wanafanya kwa hobby tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nisaidie kumshangaa huyo ndugu yako anayetudanganya eti mtu hata ukijichanga kwa miezi kadhaa baada ya kujibanabana ukapata ka laki kako ukasema utoke Dar hadi Tanga tu hapo kuosha macho basi tayari wewe ni tajiri
Tayari wewe ni tajiri,hako kalaki tano hadi umejichanga wewe siyo masikini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nisaidie kumshangaa huyo ndugu yako anayetudanganya eti mtu hata ukijichanga kwa miezi kadhaa baada ya kujibanabana ukapata ka laki kako ukasema utoke Dar hadi Tanga tu hapo kuosha macho basi tayari wewe ni tajiri
Huenda ana definition yake ya utajiri.. Kwangu mtu kuwa tajiri simpimi kwa kiwango cha pesa.. ingawa pesa ni ishara ya utajiri ila sio utajiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…