Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Yaani mwaka mzima haiwezekani[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

..............
Wateja wetu wakubwa ni hao wa elfu 5 na elfu 2 bajaji na bodaboda...wa magari nao wapo.
Tunawashukuru sana kwa mchango wao ila wachache wenye gubu wajitahidi kupunguza.
Khaa nimesema miezi siyo mwaka, mie kuna sehemu Dar hiyo hiyo nafunga zaidi ya mwaka sijaenda kabisa. Mfano maeneo ya Mbagala na majirani zake, yaani huko kumenikalia kushoto sana sijui kwanini na siwezi kuenda kabisa kama sina cha kunipeleka huko. [emoji19][emoji19]

Huko Mbezi huwa nakuja mara moja moja tena kwa kupitia njia ya Goba au Madale siyo ya Ubungo-Kimara, na huwa naishia Stendi ya Magufuli sishuki kule chini ile ya Kinyerezi. Usijali siku nikipita tena huko nitakuambia, ila tu uwepo ili nikukasirishe vizuri. [emoji1787][emoji1787]

Halafu unanisema mimi usikute hata wewe hapo utamaliza mwaka mzima utazunguruka tu huko huko kwenye wilaya ya Ilala, hutaki hata kutembelea na wilaya zingine kama Kinondoni na Kigamboni. Tembea tembea asee, au nawe utasingizia hujapapenda Dar. [emoji16][emoji16]
 
Watu wa Dar hamna upendo kabisa[emoji19]

.....
Huko kigamboni nitsenda kwa kupita darajani..
Ila kwenye maji siji kuthubutu mimi.
 
Dar ni ndogo kwenye ramani. Ila kwenye 'ground' ni kubwa kupita maelezo.

Kuna maeneo kama Buza sijawahi fika toka nizaliwe. Gongo la mboto naweza fika mara 1 kwa miaka miwili. Kigamboni naenda mara 1 kila baada ya miaka mitano.

Kama huna ishu sehemu, sio rahisi kwenda.
 
Midas hii natoka kuvuka hapa Busisi na VANGUARD hapa usiku huwa zinavuka private car nyingi sana (kulikuwa n'a foleni), sasa gari zimetoka zinafukuzana afu kwenye wheel yupo wife nilichoka hivyo nikaomba amalizie safari .

Ebwanaeeeh, hawa viumbe tuishi nao kwa akili, aiseeh gari unapigwa fimbo kwenye hizi mbio kiasi ambacho hâta mimi sijawahi kwenda, overtaking za kibabe balaa, kuna muda nilianza kupatwa na wasiwasi.

Nataka tukifika room nimuulize huu ubandidu kajifunzia wapi, atakuja kufa siku moja huyu.
 
Kwani wanaambizana kama unadaiwa?
Ni automated; taarifa zako (za gari au leseni) ndizo zinapelekea kuongezeka bila ya wao kuambizana - endapo hautolipa kwa wakati.

Ila siku hizi angalau hata usipolipa kwa muda mrefu haiwezi kuzidi mara mbili ya kile ulichoandikiwa. Kwa hiyo, ilifika 60k tu, inagota hapo hata ukae miezi 6 hujalipa.

Hapo awali ilikuwa inapanda sana. Niliwahi kupigwa faini 30k (kwa kosa ambalo baadaye nilikuja kufahamu kuwa lilihitaji onyo tu na siyo faini). Nikasahau kuilipa hadi ikiwa 120k, siku hiyo traffic kanisimamisha pale Ruvu JKT. Nikamvimbia mpaka RTO kapigiwa, nikaona hapa nitazidi kuchelewa tu. Ikabidi nilipe 120k.
 
Kumbe!
 
Kuna mwenzio anamuendeshaga mputa mputaa....joking
 
Kuna vituo hua vinauza mafuta bei cheeee sijui wanawezaje wezaje.
Faida ni kidogo lakini mauzo yanakuwa makubwa sana na stock turnover inakuwa many times maana mafuta yanaingia na kutoka haraka,,bei nzuri inavuta wateja wengi.

Ni heri kupata normal profit ila biashara inaenda kwa kukimbia kuliko kusubiri supernormal profit huku biashara mafuta yanatoka kwa spidi ya taratibu.
Kuuza chini ya bei pungufu si dhambi ,
Cha muhimu bei isije zidi au isiwe sawa na gharama mlizonunua mafuta na bei ya kuuza ikidhi gharama za uendeshaji wa kituo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…