Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Hongera sana mkuu, mimi nacheza juu kidogo ya Esther tu wiki ya pili sasa
Wakuu kati ya BMW 3 series na Audi A4, zote matoleo ya kuanzia 2010-2012, gari ipi ina handle vizuri na ina driving comfort nzuri zaidi ya mwenzie, Msaada kwenye tuta nataka nifanye maamuzi Mungu akipenda nivute moja kati ya Audi A4 na BMW 3 series.















 
Chukua A4 ila kaa mbali na gari zenye hio number plate aka Singapore product. Usithubutu.
 
Hahaaa dogo bado tu upo kwenye hayo ya ng'ombe, kama ulikuwa uko kiatu anaanguka tu mbona ukizingatia gari nayo ilikuwa kubwa. [emoji1][emoji1]
Yaani comment yako ilinichekesha tangu siku umeiandika niliona ila nikasema ngoja nikipata muda ndio nitakuja kucheka vizuri.
Hadi sasa inanichekesha,,wewe ni comedian mdogo wetu😂😂.
 
Hahahahaha gari ulikuwa unaendeshaje hadi unamgonga kiumbe wa mungu yani [emoji23][emoji23][emoji23] au uliingia highway ukiwa learner
Ndiyo nilikuwa nimetoka zangu kumaliza driving school kujifunza manual then kesho yake nikachukua automatic nikaingia barabarani. Nikaenda na akili zangu za kimanual manual kwenye automatic nikajikuta nishaiva.

Sema wakati wa kuenda nilienda vizuri tu ila wakati wa kurudi sasa ndiyo nikatoa boko. Ilikuwa ni mitaa ya home tu nikiwa narudi ndiyo nataka nitoke kwenye lami nikunje kona niingie kushoto kwenye barabara ya vumbi inayoenda home.

Tulikokuwa tunaishi baadhi ya sehemu kuna ng'ombe na punda wengi wenyeji wanawatumiaga kubeba mizigo yao. Na huwa wanawachunga na kutembea nao barabarani hovyo tu hivyo kupishana nao kila siku ni jambo la kawaida.

Sasa wakati narudi ili nikaingie kwenye ile kona nilikuwa spidi nikajisahau kupunguza hivyo badala ya kukunja kona nikaenda nikagonga kile kizingiti cha kwenye kona. Vile ambavyo vinawekwaga kwenye kona pande zote mbili.

Vile vinajengwaga kwa zege na nondo halafu kwa chini kulikuwa na kamtaro kanapita. Kwahiyo nikagonga kile kikapinda kikawa kama kinataka kuingia kwenye mtaro then tairi ya upande wangu ikaingia kidogo kwenye mtaro.

Sasa pale kwenye kona karibu kabisa na ule mtaro palikuwa na ng'ombe anakula vimajani pale na mtu anayemchunga alikuwa pembeni yake. Yule mtu alipoona nimepoteza uelekeo akaruka akamuacha ng'ombe wake pale.

Sasa alipokuwa amesimama yule ng'ombe ndipo gari ilipoenda kugota kwahiyo ikampush yule ng'ombe akaanguka then number plate ikamkata kidogo kwenye mkuu. Sikuumia na gari ilitoka nzima ila tu bumper la mbele liliachia kidogo.
 
Baada ya Wami! Wanatakiwa waje wajazie tena kifusi iwe tuta au wakwangue kusiwe na tuta ila kama kawaida yetu hamna anaejali. Hapo ili uwe salama kila tairi likanyage hayo mabaki.
Hizi imekuwa mchezo wao nchi nzima, hilo liko Mafinga. Bora uumize shockup kwa kupanda hayo mabaki maana ukiliweka kati unaacha sump
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…