Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wakuu kama mmeona njia ya Dar-Moshi mmekutana na madereva wengi wananing'iniza samaki kwenye side mirrors. Hivi ni samaki gani wale na wanatoka wapi? Na kuning'iniza vile ni kuepuka shombo kwenye gari au ?
 
Balimi hapana. Ile pombe imekaa kisukuma sana.

Safari itabaki kuwa juu.
Hahaha yeah wanasema zinanywewa sana mikoa kama Shy huko na hata hilo neno Balimi limetokana na neno Wakulima sijui ndiyo kisukuma

Hizo nikiendaga mikoani ndiyo nazifaidi sana maana bado zinauzwa shazi ila huku jijini zishaanza kupotea na kuna mahali ukiziulizia wanakushangaa

Safari oyeee

Itabaki kuwa juu mawinguni
 
Wakuu kama mmeona njia ya Dar-Moshi mmekutana na madereva wengi wananing'iniza samaki kwenye side mirrors. Hivi ni samaki gani wale na wanatoka wapi? Na kuning'iniza vile ni kuepuka shombo kwenye gari au ?
inategemea ni wapi Ila kuna Kambale wanapatikana mitaa ya Mlandizi,

wananing'iniza ili wakauke (assumed)
 
Wakuu kama mmeona njia ya Dar-Moshi mmekutana na madereva wengi wananing'iniza samaki kwenye side mirrors. Hivi ni samaki gani wale na wanatoka wapi? Na kuning'iniza vile ni kuepuka shombo kwenye gari au ?
Kuning'iniza samaki kwenye side mirrors hii inasaidia samaki asiharibike maana ndani ya gari hauna barafu za kutunzia.

Hao samaki labda ni wa Bwawa la Nyumba ya Mungu, au wa Ruvu na Malandizi ambao ni Kambale(Brigedia Ndevu).
 
Nami nashare katrip kangu ka week mbili zilizopita....
Mara nyingi napenda kusafiri usiku na hii ni imekua kama ugonjwa kwangu labda itokee dharura na natakiwa kufika mchana niendapo hapo nitasafiri kinyonge sana.

Safati inaanzia Moro kwenda Dom, nimetoka home mida ya saa tatu usiku kutafuta usafiri pale stand ya dom maana ndipo private zinapotafutia abiria wa root hiyo.. kama zali hadi saa tatu na nusu nikawa ndani ya IST iliyokua na dereva peke yake aliyekua ametoka nayo Dar na anaipeleka dom, nadhani ilitoka yard kama si bandarini moja kwa moja maana vioo vilikua bado vimeandikwa andikwa wanavyoandikaga kwa gari tuziitazo mpya.

Tukapatikana abiria wa kutosha gari hilo na tukawa tunamsubiri bwana Dere ale.. na baadae tukaingia kwenye ndinga tayari kwa kuanza safari... ila nichogundua dereva hakuwa dereva na labda aliforce kulipeleka gari dom kisa ana leseni tuu... kituko kilianzia palepale aliposhindwa kuwasha gari na kumpigia mtu simu akimueleza kuwa gari limegoma kuwaka ila mpaka analipaki ni yeye aliyelizima huku mi nikiwa nimegundua kuwa ali lock stearing na baada yakuona wanapoteza muda kujua tatizo ni nini basi nikamwambia afanye analiwasha na nikazungusha stearung ku unlock na hatimae likawaka...

Kituko cha pili jamaa alikua anatembea kawasha taa full kiasi ikawa inawapa tabu watumiaji wengine na nilipomuambia juu ya hilo akadai bora iwe full ili asijegongwa... hapo nikaanza kupata wasiwasi wa safari yetu.... lakini kituko kikubwa kilichomfanya asalimu amri na kunikabidhi gari mimi ni pale alipokua anatembea umbali flani anashusha viooo then anapandisha kwakutuambia ndani joto na awezi tembea vioo viko wazi muda wote, so nilipomuuliza juu ya uzima wa AC ndio kuniuliza kama naweza kuiwasha na hapo nikamjibu kwa vitendo. ndipo akaniuliza kama nalijua gari na baadae kupaki pembeni hatimae dereva nikawa mimi hapo bado hata Dakawa hatujafika..

TUKUMBUKE SIO KILA MWENYE LESENI NI DEREVA HIVYO TAHADHARI NI MUHIMU SANA NA KUJIFUNZA SHERIA NA MBINU ZA UENDESHAJI GARI BARABARANI HASA BARABARA KUU TUSINGOJE VYUO VYA UDEREVA.

Mpaka nakabidhiwa gari ilikua saa nne kasorobo usiku na nilifika dom saa nane kasoro ishirini napo nilislow down maeneo ya gairo kwa mvua na ukungu mkali kiasi hata taa ikiwa full ni kama unamulika kioo inakuumiza mwenyewe, ila mwendo wa wastani niliokua natembea ni speed 100 kwa 120 na sijawahi kumiliki leseni wala mafunzo ya udereva kutoka sehem rasmi zaidi ya reseni za magumashi na kupenda kujisomea mbinu za uendeshaji magari huku uzoefu nikiupata kwa trip town za hapa na pale kwa magari ya washkaji na magame ya Rally.....

Hakuna aliyekua analijua hilo na abiria wenzangu walinikubali zaidi kwakuona wako salama zaidi kwa kuweza kulimiliki gari vizuri nikuwa barabarani na kwa uzoefu wa njia hiyo maana nasafiri nayo sana.

Mpaka tunafika hakuna tatizo lolote la gari wala abiria iwe kuwarusha kwenye matuta au kutaka kusababisha ajali kwetu na kwa watumiaji wengine. Wale abiria wenzangu nahisi mpaka kesho watanikumbuka kama dereva mmoja makini sana bila kujua kwenye database ya madereva wa tanzania sipo.

Mbali nakushukuru kufika salama pia nauli yangu ilirudi maana jamaa alijishtukia japo alisingizia ile njia mgeni na alikua kachoka so nikawa nimesafiri bure na tena nilifika mpaka nyumbani bila kukodi hata boda.

But mpaka mwezi ujao nitakua namiliki leseni yangu ili niwe huru pindi nikipata zali kama hilo maana nilikuwa nawaza likitokea lakutojea na wote wangejua sina leseni imani na mimi ingewapotea na wenda ningelela lupango maana kuna gari la jeshi nililipita maeneo ya Mbande wakaja kunikuta namshusha mtu kisasa jamaa akaniambia hongereni kwakutokufa kabla mwaka haujaisha.

Muwe na Siku kuu njema na Kheri ya Mwaka mpya.
 
Wakuu kama mmeona njia ya Dar-Moshi mmekutana na madereva wengi wananing'iniza samaki kwenye side mirrors. Hivi ni samaki gani wale na wanatoka wapi? Na kuning'iniza vile ni kuepuka shombo kwenye gari au ?
Zinatoka bwawa la Mungu na maeneo mengine mkuu,wanawaweka kwny side mirrors ili wasije 'kuiva' na joto la ndani kwny gari na kuharibika.

Ila mimi siwezi kula samaki aliyeninginizwa nje ya gari akipigwa vumbi+moshi wa magari all the way,hua naona hygiene hapo inagoma/kiafya naona ni risk sana.
 
Kwahio kale kaupepo ni kama friji!
Ndio, kanasaidia samaki asiharibike.
Kuna Jamaa alizidisha idadi ya samaki katika side mirror ya kushoto alikuwa na Toyota Kluger.Kaondoka Pangani jioni katika kukimbia rough road amefika Korogwe aangalie side mirror anakuta hakuna, akapiga simu baada ya kufika kuwa amepoteza side mirror na samaki wake.
 
Ha ha ha dereva gani huyo anaendesha km zote hizo bila kuangalia nyuma kwa kutumia side mirror!
 
Hao samaki watakuwa na kitu special!
 
So far sijakutana na hiyo changamoto hapa arusha.



Sent from my SM-A720F using JamiiForums mobile app
 
Safi sana.

Sent from my SM-A720F using JamiiForums mobile app
 
Ha ha ha dereva gani huyo anaendesha km zote hizo bila kuangalia nyuma kwa kutumia side mirror!
Ukiwa Pangani Kuna shortcut ya kufika Muheza. Kwa madai yake side mirror anasema ilianguka kipande cha rough road ambacho ni Pangani-Boza-Madanga-Muheza. Na ilikuwa jioni anawahi akaungane na wadau wake High way-Korogwe kwenye Kula vyombo. Alipofika Korogwe ndio akapiga simu kulalamika samaki wameanguka na side mirror.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…