Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahaha yeah wanasema zinanywewa sana mikoa kama Shy huko na hata hilo neno Balimi limetokana na neno Wakulima sijui ndiyo kisukumaBalimi hapana. Ile pombe imekaa kisukuma sana.
Safari itabaki kuwa juu.
inategemea ni wapi Ila kuna Kambale wanapatikana mitaa ya Mlandizi,Wakuu kama mmeona njia ya Dar-Moshi mmekutana na madereva wengi wananing'iniza samaki kwenye side mirrors. Hivi ni samaki gani wale na wanatoka wapi? Na kuning'iniza vile ni kuepuka shombo kwenye gari au ?
Kuning'iniza samaki kwenye side mirrors hii inasaidia samaki asiharibike maana ndani ya gari hauna barafu za kutunzia.Wakuu kama mmeona njia ya Dar-Moshi mmekutana na madereva wengi wananing'iniza samaki kwenye side mirrors. Hivi ni samaki gani wale na wanatoka wapi? Na kuning'iniza vile ni kuepuka shombo kwenye gari au ?
Kwahio kale kaupepo ni kama friji!Kuning'iniza samaki kwenye side mirrors hii inasaidia samaki asiharibike maana ndani ya gari hauna barafu za kutunzia.
Hao samaki labda ni wa Bwawa la Nyumba ya Mungu, au wa Ruvu na Malandizi ambao ni Kambale(Brigedia Ndevu).
Interesting,jamaa anayo point aisee.Kuna jamaa yangu mmoja huwa anasema yeye anafanya service kabla ya recommended km kwasababu hata kwenye foleni engine inazunguka ila km hazihesabu.
Zinatoka bwawa la Mungu na maeneo mengine mkuu,wanawaweka kwny side mirrors ili wasije 'kuiva' na joto la ndani kwny gari na kuharibika.Wakuu kama mmeona njia ya Dar-Moshi mmekutana na madereva wengi wananing'iniza samaki kwenye side mirrors. Hivi ni samaki gani wale na wanatoka wapi? Na kuning'iniza vile ni kuepuka shombo kwenye gari au ?
Ndio, kanasaidia samaki asiharibike.Kwahio kale kaupepo ni kama friji!
Ha ha ha dereva gani huyo anaendesha km zote hizo bila kuangalia nyuma kwa kutumia side mirror!Ndio, kanasaidia samaki asiharibike.
Kuna Jamaa alizidisha idadi ya samaki katika side mirror ya kushoto alikuwa na Toyota Kluger.Kaondoka Pangani jioni katika kukimbia rough road amefika Korogwe aangalie side mirror anakuta hakuna, akapiga simu baada ya kufika kuwa amepoteza side mirror na samaki wake.
Hao samaki watakuwa na kitu special!Zinatoka bwawa la Mungu na maeneo mengine mkuu,wanawaweka kwny side mirrors ili wasije 'kuiva' na joto la ndani kwny gari na kuharibika.
Ila mimi siwezi kula samaki aliyeninginizwa nje ya gari akipigwa vumbi+moshi wa magari all the way,hua naona hygiene hapo inagoma/kiafya naona ni risk sana.
Nimemuelewa sana mshkaji,na ni eye opening kwangu na nitafanyia kazi hio kitu.Ukifikiria masaa ya kwenye foleni na km unazocover utamuelewa.
Ndio zangu hizoKama kawa yaani majuzi jamaa alinisimamisha sasa nilikuwa naongea na simu, ila kioo nikashusha, basi alichungulia tu mle ndani akarudi kuendelea na shughuli zake... Mi nikang'oa[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
Ahaa kweli siku hizi ukiwa na namba A unazidiwa na mtu mwenye pikipiki ya boxerHahahaaaaaa nimecheka sana
So far sijakutana na hiyo changamoto hapa arusha.Poliso wa Arusha wamezidi unoko.....kwa experience, kwa mfano kama unatoka Arusha kwenda Moshi....ukifika Kuanzia KIA askari wa huko mbele wapo humble kidogo.....Hawa wa Arusha unaweza ukasema wametumwa kufanya operesheni maalumu....
Sijui wanajua kila mtu anasafirisha bangi za kisimiri..?[emoji848][emoji848][emoji848]
Safi sana.Nami nashare katrip kangu ka week mbili zilizopita....
Mara nyingi napenda kusafiri usiku na hii ni imekua kama ugonjwa kwangu labda itokee dharura na natakiwa kufika mchana niendapo hapo nitasafiri kinyonge sana.
Safati inaanzia Moro kwenda Dom, nimetoka home mida ya saa tatu usiku kutafuta usafiri pale stand ya dom maana ndipo private zinapotafutia abiria wa root hiyo.. kama zali hadi saa tatu na nusu nikawa ndani ya IST iliyokua na dereva peke yake aliyekua ametoka nayo Dar na anaipeleka dom, nadhani ilitoka yard kama si bandarini moja kwa moja maana vioo vilikua bado vimeandikwa andikwa wanavyoandikaga kwa gari tuziitazo mpya.
Tukapatikana abiria wa kutosha gari hilo na tukawa tunamsubiri bwana Dere ale.. na baadae tukaingia kwenye ndinga tayari kwa kuanza safari... ila nichogundua dereva hakuwa dereva na labda aliforce kulipeleka gari dom kisa ana leseni tuu... kituko kilianzia palepale aliposhindwa kuwasha gari na kumpigia mtu simu akimueleza kuwa gari limegoma kuwaka ila mpaka analipaki ni yeye aliyelizima huku mi nikiwa nimegundua kuwa ali lock stearing na baada yakuona wanapoteza muda kujua tatizo ni nini basi nikamwambia afanye analiwasha na nikazungusha stearung ku unlock na hatimae likawaka...
Kituko cha pili jamaa alikua anatembea kawasha taa full kiasi ikawa inawapa tabu watumiaji wengine na nilipomuambia juu ya hilo akadai bora iwe full ili asijegongwa... hapo nikaanza kupata wasiwasi wa safari yetu.... lakini kituko kikubwa kilichomfanya asalimu amri na kunikabidhi gari mimi ni pale alipokua anatembea umbali flani anashusha viooo then anapandisha kwakutuambia ndani joto na awezi tembea vioo viko wazi muda wote, so nilipomuuliza juu ya uzima wa AC ndio kuniuliza kama naweza kuiwasha na hapo nikamjibu kwa vitendo. ndipo akaniuliza kama nalijua gari na baadae kupaki pembeni hatimae dereva nikawa mimi hapo bado hata Dakawa hatujafika..
TUKUMBUKE SIO KILA MWENYE LESENI NI DEREVA HIVYO TAHADHARI NI MUHIMU SANA NA KUJIFUNZA SHERIA NA MBINU ZA UENDESHAJI GARI BARABARANI HASA BARABARA KUU TUSINGOJE VYUO VYA UDEREVA.
Mpaka nakabidhiwa gari ilikua saa nne kasorobo usiku na nilifika dom saa nane kasoro ishirini napo nilislow down maeneo ya gairo kwa mvua na ukungu mkali kiasi hata taa ikiwa full ni kama unamulika kioo inakuumiza mwenyewe, ila mwendo wa wastani niliokua natembea ni speed 100 kwa 120 na sijawahi kumiliki leseni wala mafunzo ya udereva kutoka sehem rasmi zaidi ya reseni za magumashi na kupenda kujisomea mbinu za uendeshaji magari huku uzoefu nikiupata kwa trip town za hapa na pale kwa magari ya washkaji na magame ya Rally.....
Hakuna aliyekua analijua hilo na abiria wenzangu walinikubali zaidi kwakuona wako salama zaidi kwa kuweza kulimiliki gari vizuri nikuwa barabarani na kwa uzoefu wa njia hiyo maana nasafiri nayo sana.
Mpaka tunafika hakuna tatizo lolote la gari wala abiria iwe kuwarusha kwenye matuta au kutaka kusababisha ajali kwetu na kwa watumiaji wengine. Wale abiria wenzangu nahisi mpaka kesho watanikumbuka kama dereva mmoja makini sana bila kujua kwenye database ya madereva wa tanzania sipo.
Mbali nakushukuru kufika salama pia nauli yangu ilirudi maana jamaa alijishtukia japo alisingizia ile njia mgeni na alikua kachoka so nikawa nimesafiri bure na tena nilifika mpaka nyumbani bila kukodi hata boda.
But mpaka mwezi ujao nitakua namiliki leseni yangu ili niwe huru pindi nikipata zali kama hilo maana nilikuwa nawaza likitokea lakutojea na wote wangejua sina leseni imani na mimi ingewapotea na wenda ningelela lupango maana kuna gari la jeshi nililipita maeneo ya Mbande wakaja kunikuta namshusha mtu kisasa jamaa akaniambia hongereni kwakutokufa kabla mwaka haujaisha.
Muwe na Siku kuu njema na Kheri ya Mwaka mpya.
Ukiwa Pangani Kuna shortcut ya kufika Muheza. Kwa madai yake side mirror anasema ilianguka kipande cha rough road ambacho ni Pangani-Boza-Madanga-Muheza. Na ilikuwa jioni anawahi akaungane na wadau wake High way-Korogwe kwenye Kula vyombo. Alipofika Korogwe ndio akapiga simu kulalamika samaki wameanguka na side mirror.Ha ha ha dereva gani huyo anaendesha km zote hizo bila kuangalia nyuma kwa kutumia side mirror!
Hatari sana mkuuKuna gari zinatoka bandarini zimechoka kuliko namba B sijui shida nini