Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Huyo wa VX atakuwa hakuamua. Hivi majuzi hivyo vi baby walker vilinitunishia misuri Moro - Dom alafu sasa nikawa na jamaa waoga, basi roho ilikuwa inaniuma.

Kimoyo moyo nikajisema; raia wakijidai kulala tu hivyo vi IST vitasoma namba.

Ile nafika tu Kongwa raia wakawa wamelala hapo nikaanza fujo roho yangu sasa ikatulia [emoji23][emoji23][emoji23]

Ila Huwa wanakomaa na vile vigari barabarani.
 
Jitahidi ulale Singida kesho yake umalizie
 
Hakuamua sana hata hivyo baada ya wakati wa kwenda kupata vyeti…


Kuna watu mna drive mpaka abiria tunashika mioyo 😎
Juzi kati trip tu fupi LC hardtop driver anaispeedisha mpaka nikamwambia siku ukigonga ukaua. Utajifunza

Napenda speed, ila sio kivile… ukiwa mwendokasi sana mimi utanishusha kwa ambavyo uwa nalalamika 🤣🤣🤣
 
Au ndio zile Wigelekelo anaita VX bwege? Mtaani niliwasikia vijana wakiita 'kubwa jinga' nikamkumbuka ndugu yangu Wige!
 
Hawa wenye IST na wenzao nikumona anataka ligi huwa namsubiri kwenye matuta, tukishuka tuta nakamua mpaka 160kph naganda hapo kwa dakika kadhaa halafu narudi 120-130 hanioni tena maanake itabidi afikishe 150kph kunitafuta ambalo ni zoezi gumu kwake.
 
Hardtop sio gari ya kukimbia kabisa.
 
Kuna watu wakiwa wamelala huwa wanahisi gari ikiwa inakimbia sana.

Mi mmoja wapo.
 
[emoji23][emoji23] kama speed ngapi vile ndio roho inabidi inakuchonoka.

Safari ndefu inachosha asikwambie mtu. Hapa nawaza Safari ya kurudi bongo. KM 1350+ si mchezo. Hapo lazima kibati kihusike
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…