Nami nashare katrip kangu ka week mbili zilizopita....
Mara nyingi napenda kusafiri usiku na hii ni imekua kama ugonjwa kwangu labda itokee dharura na natakiwa kufika mchana niendapo hapo nitasafiri kinyonge sana.
Safati inaanzia Moro kwenda Dom, nimetoka home mida ya saa tatu usiku kutafuta usafiri pale stand ya dom maana ndipo private zinapotafutia abiria wa root hiyo.. kama zali hadi saa tatu na nusu nikawa ndani ya IST iliyokua na dereva peke yake aliyekua ametoka nayo Dar na anaipeleka dom, nadhani ilitoka yard kama si bandarini moja kwa moja maana vioo vilikua bado vimeandikwa andikwa wanavyoandikaga kwa gari tuziitazo mpya.
Tukapatikana abiria wa kutosha gari hilo na tukawa tunamsubiri bwana Dere ale.. na baadae tukaingia kwenye ndinga tayari kwa kuanza safari... ila nichogundua dereva hakuwa dereva na labda aliforce kulipeleka gari dom kisa ana leseni tuu... kituko kilianzia palepale aliposhindwa kuwasha gari na kumpigia mtu simu akimueleza kuwa gari limegoma kuwaka ila mpaka analipaki ni yeye aliyelizima huku mi nikiwa nimegundua kuwa ali lock stearing na baada yakuona wanapoteza muda kujua tatizo ni nini basi nikamwambia afanye analiwasha na nikazungusha stearung ku unlock na hatimae likawaka...
Kituko cha pili jamaa alikua anatembea kawasha taa full kiasi ikawa inawapa tabu watumiaji wengine na nilipomuambia juu ya hilo akadai bora iwe full ili asijegongwa... hapo nikaanza kupata wasiwasi wa safari yetu.... lakini kituko kikubwa kilichomfanya asalimu amri na kunikabidhi gari mimi ni pale alipokua anatembea umbali flani anashusha viooo then anapandisha kwakutuambia ndani joto na awezi tembea vioo viko wazi muda wote, so nilipomuuliza juu ya uzima wa AC ndio kuniuliza kama naweza kuiwasha na hapo nikamjibu kwa vitendo. ndipo akaniuliza kama nalijua gari na baadae kupaki pembeni hatimae dereva nikawa mimi hapo bado hata Dakawa hatujafika..
TUKUMBUKE SIO KILA MWENYE LESENI NI DEREVA HIVYO TAHADHARI NI MUHIMU SANA NA KUJIFUNZA SHERIA NA MBINU ZA UENDESHAJI GARI BARABARANI HASA BARABARA KUU TUSINGOJE VYUO VYA UDEREVA.
Mpaka nakabidhiwa gari ilikua saa nne kasorobo usiku na nilifika dom saa nane kasoro ishirini napo nilislow down maeneo ya gairo kwa mvua na ukungu mkali kiasi hata taa ikiwa full ni kama unamulika kioo inakuumiza mwenyewe, ila mwendo wa wastani niliokua natembea ni speed 100 kwa 120 na sijawahi kumiliki leseni wala mafunzo ya udereva kutoka sehem rasmi zaidi ya reseni za magumashi na kupenda kujisomea mbinu za uendeshaji magari huku uzoefu nikiupata kwa trip town za hapa na pale kwa magari ya washkaji na magame ya Rally.....
Hakuna aliyekua analijua hilo na abiria wenzangu walinikubali zaidi kwakuona wako salama zaidi kwa kuweza kulimiliki gari vizuri nikuwa barabarani na kwa uzoefu wa njia hiyo maana nasafiri nayo sana.
Mpaka tunafika hakuna tatizo lolote la gari wala abiria iwe kuwarusha kwenye matuta au kutaka kusababisha ajali kwetu na kwa watumiaji wengine. Wale abiria wenzangu nahisi mpaka kesho watanikumbuka kama dereva mmoja makini sana bila kujua kwenye database ya madereva wa tanzania sipo.
Mbali nakushukuru kufika salama pia nauli yangu ilirudi maana jamaa alijishtukia japo alisingizia ile njia mgeni na alikua kachoka so nikawa nimesafiri bure na tena nilifika mpaka nyumbani bila kukodi hata boda.
But mpaka mwezi ujao nitakua namiliki leseni yangu ili niwe huru pindi nikipata zali kama hilo maana nilikuwa nawaza likitokea lakutojea na wote wangejua sina leseni imani na mimi ingewapotea na wenda ningelela lupango maana kuna gari la jeshi nililipita maeneo ya Mbande wakaja kunikuta namshusha mtu kisasa jamaa akaniambia hongereni kwakutokufa kabla mwaka haujaisha.
Muwe na Siku kuu njema na Kheri ya Mwaka mpya.