Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Njia ya Dar mpk Arusha nimepita mara 3 tu, na kiukwel nilikuwa natembea mwendo wa kitalii maana nilikuwa na wageni nimetoka kuwapokea.

Ila njia ya kuanzia Shelui(Singida) mpaka Dodoma almost (338 KM) huwa natumia masaa 3 tu wakat wa usiku.
Ndio maana nilitaka nijue unatumia gari gani 540km Dar-Moshi utumie masaa matano. Maanake kuna Dar-Msata hapa pana usumbufu, utoke Msata hadi uimalize Wami hapajatulia. Wami hadi Segera kuna vimiji kibao. Sehemu ambayo utatembea kwa raha ni Mombo-Same na mbele kidogo. Kwa gari za kawaida hizi sijui Wish,Kluger siamini kama kuna mtu anaweza kutumia masaa 5 tu.
 
Mguu mguu chief.[emoji2]
 
Ulikuwa na gari gani Baba?maanake 243kms Kwa 1.5hr
 
Watu wanatembea na noah dume masaa 5 😂
 
Kutoka Tegeta njia panda ya wazo hadi Msata ni 1hour. Msata mpaka Segera 1hour.20minutes Segera to Tanga 1hour. Mara kwa mara natumia muda huo kutoka Hapo njia panda ya wazo kwenda Tanga. Muda wa usiku lakini
 
Masaa 4 dakika 45. Chai. Himo mpaka Korogwe ulitumia muda gani? Korogwe Hadi Msata ulitumia Muda gani? Msata-Tegets ulitumia muda gani?
Unaweza ukawa Tomasso lakini hivi vitu vipo, 500km kwa around 5hrs unakwenda vizuri kabisa. Tulikuwa tumeongozana na Hilux D4D, inatembea balaa. XT sio mashine ya kuchezea, siku nyingine tumetoka Tukuyu saa 9:30 asubuhi, saa 1.00 tulikuwa Iringa tunapata breakfast.

Kuna siku nimepanda IT, tumetoka Misugusugu saa 5.30 usiku, by 12.30 tulikuwa Nanenane Mbeya. Watu wanatembea mkuu.
 
Kama umeongozana na D4D hakuna mwendo hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…