Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

nipo Heka itigi Manyoni KM 70 KUTOKA lami na premio namba C 170K+ KMS niliyonunua kwa mtu na kesho nageuza Dar KM zaidi ya 600 nadhani gari ni Regular maintanance Mileage ni number tu kama unavyosema
Heka siyo Itigi mkuu,Heka ni Manyoni,halmashauri ya Itigi inagusa mwisho Idodyandole,ila huko Kizigo,Heka,hadi Nkonko sio Itigi tena,ni Manyoni
 
Inakubidi utoke Dar 4am ili 6am ikukute Morogoro otherwise utatumia at least 4hrs kufika Morogoro.
 
Quick and effective solution ya kuondoa kero ni kujenga hio expressway ya kulipia. Maanake useme uanze kutanua hio na magari yanaendelea kutumia Dar-Moro itakuwa 8hrs
 
Nlikuwa nimechoka leo nimetembelea 14km/l kutoka Arusha mpaka Babati. Kupanda ile milima ndio kukaongeza average.
Hicho kipaji sina. Nilijaribu from. Mombasa nikapata around 12k/l kufika border nikapotezewa karibu 2hrs bila sababu ya msingi kutoka hapo nikavuruga utaratibu wote nikaishia 9.9
 
Road Trip yangu ya tarehe 22/12/2022 from moshi to mbamba Bay Gari Tako la nyani

Safari nilianza saa kumi na mbili asubuh.. taratibu kutoka moshi pemben kukiwa na kvaaaa kubwa na energy drink.. niliamua kupita route ya arusha.. niliingia babati mapema sana nikapata supu ya nguvu ili kvaaa isinisumbue .. maana kvaaa ukinywa bila msosi lazm ikujeruh.. baada ya kupata supu nzito nikaanza safari.. kwanza nilitaka nipite njia ya kateshi then singida mpk manyoni then nidondokee dodoma... njia hii nikaona itakuwa n ndefu sana na pia nilikuwa pekee yangu itanichosha.. nikapita njia ya short kat hapo nikawa nimefika dodoma.. aisee kvaaa inateta sana njaa dodoma pale nikapiga msosi nyama nyama.. then kama kawaida energy drink n kvaaa.. ki ukwel tako la nyani n gari la safari.. ina weakness moja tu ni gari ambalo n jepesi ukiwa speed kuna wakat nilitaman kupakia hata mawe nyuma ya gar ilitu kuongeza uzito

Dodoma nikapita mtera then iringa.. nilipofika iringa ikabid nipumzike nipate kilaji.. nikaona bora nilale kesho niendelee na safar ya kwenda mbamba bay.. pale iringa nikala nyama sana pale.. ile nimeamka asubuh tumbo linauma balaaa full kuhara aiseee dahhhh ikabid nitulie.. mchana ikabid nibadili route niende tu njombe kwa wakwe zangu wa zamani.. kaa pale njombe.. stimu za kufika mbamba Bay zikaisha nikarud zangu moshi...

Next Year lazm nifike mbamba Bay nipande meli nizunguke nyasa.. .. hii Road Trip lazm itimie..then nizunguke ruvuma nitokee dar es salaam. hakika Tako la Nyani ni Gari...

Happy New Year wadau.....
 
Utamu wa mbamba bay uanzie mbinga kwenyewe sasa.

Zile kona zilivyotengenezwa mpaka raha.
 
Mkuu ulikuwa na nani? Kwahio umeendesha ulivyochoka ukaamua kukatisha safari?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…