Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Kifuatacho soon tutaingia namba E....Basi hawa wa Namba E watakuwa wanaona Dunia nzima ni yao....utakutana na Porte namba E jamaa kavaa miwani nyeusi, kakata kishoka, ndevu kaziachia kama brush....yaani atatuona tuliobaki wote ni washamba tu..[emoji848][emoji848]...akisimamishwa na askari, ataongea kwa kiburi cha namba E, basi askari hapo anachora vyeti tu.

Hawa wenye D wataanza kujiona kama sisi wenye C tunavyojiona leo hii..

Wenye C tutajiona kama wanavyojiona wenye B leo hii..

Wenye B watajiona kama wanavyojiona wenye namba A leo hii...

Wenye namba A watajiona wamerudishwa enzi za namba TZ 009844[emoji21]

Wale ambao waliwahi kuwa na namba TZ.......watajihisi wanaishi on the other side of the hell....[emoji26][emoji26]

Ndiyo Tanzania hii imetawaliwa na Plate namba na Low mileage..
Hahahaaaaaa nimecheka sana
 
[emoji23][emoji23][emoji23]

Kuna verosa nineiona jana hapo Kibo ni IT kidogo nilie. Kwani huwa magari mabovu yanauzwagwa jaman? Au lilikaa juani sana hapo bandarini? Lkn pia hapana. Ilikua zaidi ya kupauka. Hapo mbele limeishaa[emoji119][emoji119] imagine ndo namba E
Kuna gari zinatoka bandarini zimechoka kuliko namba B sijui shida nini
 
Mungu ni mwema nimevuka salama na hatimaye Kuuona mwaka 2021..

Ninaimani wazee wote wa road trip mmevuka salama..

Mungu awatangulie katika kutimiza malengo ambayo hayakutimia kwa mwaka uliopita wa 2020..

1.Wakuoa aoe.
2.wa kuolewa aolewe
3.Wakuachika asiachike tena
4.Wa kutafuta kazi/biashara/masomo afanikiwe
5.Ndoto ya Ujenzi/kiwanja/gari ikatimie.

Mapambano yanaendelea.
View attachment 1664315
Huu mwaka natazamia kuingia kwenye mabus Rasmi
 
Uncle wangu huwa ni mtu wa maspeed sana. Hiwa safari zake za dar to moshi masaa matano mpk nyumbani kbs. Lakini huwa tunashangaa sana inakuaje anatoboa bila vyeti. Akatufundishaga mbinu yake. Huwa anapanga CD pape mbele kwenye dashboard anatandaza. Anasema trafiki akipiga camera anaambulia sifuri. Kuna anayeijua hii mbinu? Kuna ambaye amewahi jaribu?

Ajitokeze mtu aijaribu basi [emoji28]

Hivi kuna matrafiki kwani huku? Tusiharibiane mbinu zingine jamani
Camera unaweza pigwa kwa nyuma.

Sent from my SM-A720F using JamiiForums mobile app
 
Nafanyia kazi zangu nyumbani. Nina kaofisi kadogo.

Natoka weekends tu au kati ya week kukiwa na ulazima sana.

Kwahiyo week nzima naweza tembea kama 50km. Na gari zipo mbili, moja ya safari nyingine town trip.

Na hiyo ya safari inaweza tembea km 1000-1500km kwa miezi minne hivi.

Sent from my SM-A720F using JamiiForums mobile app
Kwa afya ya gari ni bora gari yenye high km za kutembelewa highway kuliko gari yenye low km za kutembelewa town trip.
 
Highway hawakagui.

Labda hawa wa mjini kati.

Sent from my SM-A720F using JamiiForums mobile app
Poliso wa Arusha wamezidi unoko.....kwa experience, kwa mfano kama unatoka Arusha kwenda Moshi....ukifika Kuanzia KIA askari wa huko mbele wapo humble kidogo.....Hawa wa Arusha unaweza ukasema wametumwa kufanya operesheni maalumu....
Sijui wanajua kila mtu anasafirisha bangi za kisimiri..?[emoji848][emoji848][emoji848]
 
Hahahahah kwahiyo mkuu nimeuza raman.

Au jamaa yako alipanga vibaya? Basi nutakua sileti tena humu.

Matrafiki wa humu tunawamaindoo sana. Nyie mna roho nzurimoo[emoji28][emoji28][emoji28]
Hahaha...ndiyo hivyo mkuu jamaa wakibana mlango inabidi kutokea dirishani.
Jamaa alishauriwa aining'inize pale kwenye Kioo cha kutazamia nyuma...
Akala cheti chenye nembo ya Polisi Tanzania..
 
Kuna gari zinatoka bandarini zimechoka kuliko namba B sijui shida nini
Nahisi ni zile zinazotelekezwa baada ya waagizaji kushindwa kuzikomboa...

Mtu anaambiwa magari Japani ni bei rahisi, anaingia kichwa kichwa...

Likitua bongo anakutana na bandari wamekinga mkono, grace period ikiisha bandari wanaaza kuhesabu tu, clearing and forwarding agent amekinga mkono, TRA hawa wanakinga kikapu kabisa, Bima wanakinga mkono..

Basi muagizaji anaaza kutoa laana, lakini ndiyo hivyo tena serikali hailaaniki..[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji26][emoji26]
 
Ewaaaa mi Safari na Balimi ndiyo bia zangu pendwa yaani hapo hauniambii kitu! Japo kuna Watu huwa wananishangaa wananiambiaga natumia vitu vizito eti hizo siyo bia ni gongo!

Mi nitakunywa bia zote ila siyo hizo Lite aiseee. Yaani haujanifuma bado kwa kweli.
Balimi hapana. Ile pombe imekaa kisukuma sana.

Safari itabaki kuwa juu.
 
Back
Top Bottom