Madalali kwny kiwanja changu walitaka kunifanya kitu mbaya nikawashtukia nika ahirisha kuliuza tu.
Wale jamaa wanaoununua magari yaliyopata ajali wao nilikutana nao anga zao.
Nilipata ajali Arusha na brevis(ile ya CC 3000) No. Yake ikiwa ni CGT na kipindi hicho no. Latest ilikua ni CHA,nilikua nimetoka dar nimeenda Arusha kwa shughuli binafsi so Arusha sio home lkn nilisoma pale Chuo cha Uhasibu kwa miaka 3 kwa hio Chuga napajua jua sana.
Gari nilikua nalipia insurance ya 3rd party tu,so gari ikawa inahitaji matengenezo kama ya mil 2.5 nikaona sio inshu ngoja niwauzie hao masela wanaoyakata.
Nikaenda pale mtaa wa Disemba kuwacheki jamaa.Nikawaonyesha picha,jamaa wa kwanza tu akaniambia nitakupa Tsh. 1mil nikaona huyu ni fala nini nikaondoka bila hata kuaga,kumbe jamaa linaniona mi ndio fala tu.
Yale majamaa yana mtandao wa kiboya sana,yakabonyezana fasta tu kwamba kuna lofa mmoja wa kutoka huko Dar kapata ajali hapa arusha na huku Arusha sio kwao anaishi Lodge so hana option nyingine tukomae nae tumpige kidwanzi.
Aisee kila nilipoenda kwa wanunuzi wengine wananiambia niwauzie kwa laki 7 wengine mpk laki 4,nikaona huu ni ushenzi tu.
Nilikua nakaa lodge kwa hio nikawa nafikiria kuliuza chap chap nisepe dar niongezee pesa kidogo then nitafute usafiri wa kuzugia wkt najipanga,baada ya hizo bei za mtaa wa disemba kuzingua nikatafuta msela wangu anayeishi pale town niliyesoma nae ikabidi nimdanganye,nikamwambia anitafutie chumba cha bei rahisi chenye parking ndani nimehamia Arusha kikazi na nitaishi kwa miezi 3(nilifanya hivyo kwa kua sikutaka kuiacha gari gereji wale jamaa wangeiba kila kitu na pia nina ndg zangu pale town nao sikutaka kuwasumbua kwa kwenda kuipaki ile gari kwao, sipendi kua mzigo kwa watu wengine).
Nikalipia kile chumba(pale sakina kwa Iddi), sh.80,000 kwa miezi 3 ikawa 240,000 breakdown ikaivuta ile ile gari mpk hapo geto nikaifunika na turubai nikarudi zangu dar(mwenye nyumba ananipigia simu akiniambia sionekani,nikawa namwambia nimesafiri kikazi).
Baada ya miezi 2 nikarudi Arusha nikaivuta ile gari mpk gereji ikatumia kama siku 12 hivi ikitengenezwa,hapo nikawa nalala kwny hicho hicho chumba wkt inatengenezwa la sivyo nilitakiwa niwe lodge kipindi chote hicho).,so gari ilirudi barabarani.So kile Chumba nililipia kwa miezi 3 ili wanilindie gari yangu tu bila wao kujua.,la sivyo ningeiacha sehemu nyingine ingenigharimu zaidi.
Was it worth struggle zote hizo?Hapo sijui lkn nilimaindi tu kuona gari niwauzie wale wahuni kwa laki 7 tu,BTW hio gari mpk leo iko naitumia kama backup i.e sanasana kwny safari zangu ndefu na mara chache hapa hapa Dar, wale jamaa wa gereji waliitengeneza vzr sana imenyooka kichizi na pia siwezi kuiuza tena kwa sasa hivi maana bei za brevis mnazijua zilivyo kwa sasa,so ni kama nimefunga nalo ndoa ya kikristo and am proud of that).
Hicho ndio kilichonitokea wakuu.