Jana majira ya saa 2 usiku natoka kijichi (mgeni nani) kuelekea bagamoyo kijiji kimoja kinaitwa bom ambapo kuna mtambo wa dawasco hapo. Nilikua na mitsubish pick up ( double cabin) L200 ya mwaka 95 engine 2400, alafu left hand.
Basi bhaana kufika mtongani hapo nakutana na foleni ya kizushi tu alafu malory na daladala tupu, nikafanya vifujo fujo vya kujichomeka huku na kule hatimae nikapasua foleni maana ilitakiwa saa 7 au 8 niwe nisharudi kijichi.
Sasa nimetembea kufika maeneo ya tabata pale kwenye traffick lights, kutokana na haraka nikajikuta navuka kwenye red light, hapo kulikua na IST mbele ilivuka namm nikaunga, kumbe bhana mbele kuna yange yange. Ile kuvuka tu IST akapigwa mkono namm nikapigwa mkono.
Jamaa wa ist sijui akamalizana nae vipi, sasa akaja kwangu... Kijana naomba leseni, (hapo nikakumbuka hata leseni sikuchukua kutokana na haraka) nikaanza kumpiga sound pale jamaa haelewi kakomalia leseni namimi nina haraka zangu. Basi akatoka kidogo akaenda kupiga mkono gari zingine huko, hapo ndo alipofanya kosa [emoji23].
Pembeni kulikua na bodaboda wamepack nikamwiita mmoja nikamwambia vp huyu traffic hapa ana gari au pikipiki? Akasema huyu hana usafiri. Nikamwambia mi nataka nikimbie hapa vp njia hii haina folen mbele huko? Boda anasema ukikimbia huyu askari huwa anakodi boda anakufukuza.
Nikamwambia haina noma ni naishia hapo ubungo tu, ( sikutaka kumwambia ninapoelekea maana asije nichomesha). Basi nika cheki kwa side mirror naona jamaa yuko bize anaongea na gari ya nyuma huko.
Kimoyomoyo nikasema BINGO, manina nikaifumua chuma pale nikaingia rod yaani nilikua kama niko kwenye mashindano vile nilikua napangua gia huku nafanya overtaking za hatari. Kufika pale fly over ya ubungo nilifuta kisahani hadi 180km/hr.
Chuma inanguruma yaan sikutaka hata kujisumbua na side mirro kumcheki kama jamaa anakuja au vipi, mwishoe nikafika mwenge nikakunja bagamoyo rd nikanyoosha goti.
FUNZO : Maedereva tusikubali kuonewa ki bwegebwege, ukiona chuma iko vzuri ingia road timua. Kama anataka ligi akufate. [emoji23]