Mkorintho
JF-Expert Member
- Feb 17, 2009
- 594
- 1,141
Umenikumbusha hii ya Dodoma - Kondoa hapa nyuma kabla ya kufika Chemba kuna kituo kidogo cha polisi pia sijui ndio Itiso pale au la wao wanafunga geti kabisa hata mchana. So hakuna namna utapita juu kwa juu japo sio nyakati zote wanakagua thoroughly lakini walau mtasimamishwa pande zote za barabara muendao na mrudioOk hizo Barrier za POLISI zinawekwa kwenye maeneo ya Ujambazi wa kutumia magari.
kwa mfano Njia ya Dodoma Kondoa kuna msitu mkubwa wa Hifadhi ya Mlima Mtungutu, ndani ya Mlima huo majambazi yaliteka magari sana hiyo POLISI wakaweka mageti (Barriers) mawili, ukianza kuingia huo msitu na ukitoka, maana yake km patatokea tukio basi hatatoka huyo jambazi aliyefanya tukio, na gari za silaha zitaingia.
Mfano ukikoswakoswa kutekwa ukiikuta Barrier unawaambia
nyingine Barabara ya Dodoma Morogoro unaikuta Makalavati, Dumila Dakawa nk
Kuna kipindi Chalinze Msata Segera JWTZ waliamua waPatrol wenyewe baada ya kuona POLISI wamelemewa na inasemekana ni POLISI wenyewe walijua ni nini kinaendelea
Hivyo Barrier ni eneo lolote hatarishi lakini yanatambulika, km litatokea ghafla limetegwa na majambazi ndani ya masaa litasambaratishwa
Kwa kweli Barabara zetu kuu hapa TZ ni salama kwa usiku labda uwe na breakdown
Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app