Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

[emoji15][emoji15]
JamiiForums1472219810_720x714.jpg
 
Mkuu gari ya chini rough road/off road mbona iko wazi. Bush,ball joints,rack ends,tie rod ends etc zinakufa haraka sana
Hatari sana...

Nishawahi kata ball joint tairi ya mbele, tairi ikang'ang'ania uelekeo mmoja, disk ikadondokea juu ya rim na ikaikata, baada ya rim kutoboka upepo ukapotea wote ghafla kwenye tairi...

Haya matukio yote yalitokea sekunde 10 nyingi, bahati yangu ilikuwa ni mchana na barabara ya rough na mwendo haukuwa mkubwa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gari la kiboya ndo gari gani Mkuu?, nilikutanaga na ist road alinipita Hale tanga mi nikiwa na Subaru Forester jamaa alikaza Sana nilikuja kumpita mombo nikiwa 140 kph, Hawa jamaa wa ist , ukikutana na dereva mzuri anakuzalilisha hata Kama una gari la cc 3000 utazalilika tuu.
Tatizo barabara za TZ kuna vibao vya speed limits vingi mno kwa sababu hatuna highways...

Ukiwa Tanzania, wastani wa muda unaotumia kati ya Dar na Tanga ni masaa 5 hivi.

Kwa nchi kama US, umbali kama huo kati ya Dallas na Oklahoma City ni masaa 3 hivi...

Utofauti ni kwamba ukishaingia kwenye I-35 (interstate-35), ni wewe, mguu na steering wheel...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatari sana...

Nishawahi kata ball joint tairi ya mbele, tairi ikang'ang'ania uelekeo mmoja, disk ikadondokea juu ya rim na ikaikata, baada ya rim kutoboka upepo ukapotea wote ghafla kwenye tairi...

Haya matukio yote yalitokea sekunde 10 nyingi, bahati yangu ilikuwa ni mchana na barabara ya rough na mwendo haukuwa mkubwa...

Sent using Jamii Forums mobile app

Aiseeeh....!! Pole sana.

Umenifikirishaaa.... nimewaza hilo tukio lingenikuta mie halafu niko kwenye safari zangu..... nakuwaga pekeyangu...... aahahahahahaaaa (najikaza tuu kutokulia 🤣🤣🤣)

Namshukuru Mungu sijawahi kutana na changamoto ya namna hiyo barabarani japo bebiwoka nnayoendesha ni kuu kuu haswa.

Napenda sana magari, napenda sana safari za kwenda naendesha gari ila ......

Makorokocho ya gari siyataki, yakinikuta matukio barabarani napambana nayo mwenyewe mwanzo mwisho.

Nadeka kwenye mapenzi ila sio majukumu yangu 😜😜

K’ Matata.
 
Aiseeeh....!! Pole sana.
Umenifikirishaaa.... nimewaza hilo tukio lingenikuta mie halafu niko kwenye safari zangu..... nakuwaga pekeyangu...... aahahahahahaaaa (najikaza tuu kutokulia)

Asante Mungu ni mwema sikupata shida, nikabadilishiwa ball joint, weka spare tyre na baada ya masaa kadhaa safari ikaendelea...

Kuna wakati pia maeneo ya Iringa, nilikuwa nafanya ligi na jamaa mmoja hivi usiku yule mtu anatembea kama anawahisha gazeti...

Nipo kwenye kimteremko fulani kikali, gari imewaka na mshale wa speed hauna mahali zaidi pa kwenda...nikasikia kishindo puuuuu, tairi ya nyuma imeivaa na ishaita inarusha rusha mapande tu...

Kilichobaki hapo ni kubalance gari itulie na ikasimame yenyewe bondeni...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom