Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wakali wa hizi kazi...

Mwenye kujua vijiwe vya wazee wa favor "kunguru weupe" barabara ya Tanga <> Dar hebu aviweke bayana hapa, kuna road trip ya kutumia hiyo barabara Jumapili, nisijewaachia wakuda hao pesa ya sikukuu...

Dar - Bagamoyo - Segera - Muheza - Tanga
Mbaya zaidi sijuagi majina ya hayo maeneo.

Ila kuna spots huwa nawakuta kila nikipandisha hiyo njia.

Tochi huwa hazina sehemu maalumu.
 
Mbaya zaidi sijuagi majina ya hayo maeneo.

Ila kuna spots huwa nawakuta kila nikipandisha hiyo njia.

Tochi huwa hazina sehemu maalumu.

Nimesafiri jana badala ya j'2

Dar - Bagamoyo - Msata, ndio wapo wa kutosha, sana wanacheck speed...

Msata hadi Segera hadi Tanga, muda ulikuwa ushaenda hakukuwa na hao jamaa kabisa...

Polish_20220416_142601570.png
 
Kwema wakuu..... leo sina hamu kabisa yani, yani leo nimechezewa na Alphard kama mtoto hadi roho imeniuma sana na hadi hapa nilipo nina hasira sana na hata usingizi umegoma kabisa. Mie nilikuwa na Nissan XTRAIL old model T30.

Na ilikuwa ni msafara mmoja wa harusi na aliekuwa ananichezea ni kaka yangu na huwa hafati mziki wangu hata kidogo na hata yeye anajua hilo na kabla ya safari kuanza aliniomba nisikimbie sana. Tumetoka Singida na kwenda kuoa Mwanza, na gari zilikuwa 8 yaani Alphard 2, Nissan XTRAIL 2, IST 1, Toyota Camry 1, Kluger 1 na bus kubwa tulikodi kwa ajili ya akina mama.

Na sababu ya kuchezewa ni hii gari yani ikifika 150kph - 160kph inapandisha sana Temperature kwa hiyo inabidi upunguze hadi 100kph - 90kph ndio angalau inashusha temperature. Hii gari niliazima kwa jamaa yangu na kumuachia gari yangu Subaru Forester XT kwa kigezo cha kusave pesa kwenye masuala ya mafuta. Lakini baada ya kusave mafuta mwishowe imeniletea fedheha tu. Ila Kiukwel nimezichukia sana Nissan XTRAIL.
Kabla hamjarudi hakikisha unatembelea sehemu ya kuosha gari au gereji yenye Pressure Washer na ile ya kupulizia Upepo au kujazia Matairi kisha cheza na hiyo Radiator ipigwe Maji ya Pressure Washer sana na kisha Pressure ya Upepo sana kisha rudia Pressure Washer mpaka ujiridhishe alafu zama Mfukoni na uweke Coolant.

Huyo mwenye Alphard utampasua Kifua na utakuja kunishukuru na kuhadithia tena hapa.

In-fact & In-short: Cheza na Radiator ujuavyo utajionea muujiza njiani ukiwa unarudi.

Coolant na Maji ya kawaida ni sawa ufaninishe Energy drink na Soda... Nyingi zinafanana na wengi hawajui tofauti lakini Kazi yake ni kubwa sana.

Naomba kuwasilisha.
 
Shukraan sana kiongozi kwa trick uliyonipa, ila tulirudi siku ile ile na kiukwel nilirud kinyonge sana. Ila pia ile XTRAIL ilikuwa na coolant kwenye radiator, Ila siwezi tena kutumia XTRAIL kwenye misafara maana ni aibu mnoo, nitapambana tu na Subaru XT yangu.
 
Haya matuta mapya ya makongo lugalo ni makubwa duh. Tulip Zoea kutembea na zile humps unakutana na rasta mpya Kama za Iringa kihesa semtema alafu unalikuta li bumps kuuubwa ni yatari Sana. Usiku WA Jana nimekuta ajali mbili hapo.
Alafu walivyo ajinga hata rango hawakuyapaka. Nilijua tu lazima watu wale za uso pale
 
Kanyooka kama ndo kashuka kwenye meli vile [emoji23] na plate no mpya DZA [emoji1787][emoji1787].

Imekula shi ngapi mpaka kurudi road? Insurance ilitumika au mlimalzana na jamaa?
Imemeza milioni mbili na ushee, na bado kidogo kuna taa za nyuma zina crack itabidi nizibadilishe. Sema inatia raha.

Nlimalizana na jamaa kishkaji
 
Back
Top Bottom