Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Duh hatari sana. So far njia ya kaskazini sijasikia ajali mbaya. Ila nimeshangaa sana nimekuta watu wamegonga nyuma ya magari mengine zaidi ya matukio matatu.
Fatigue, simu, bad following distance ndio tatizo hapa mkuu hasa simu...pls guys tafuta hand free au simu weka mbali ukiwa nyuma ya usukani
 
Duh hatari sana. So far njia ya kaskazini sijasikia ajali mbaya. Ila nimeshangaa sana nimekuta watu wamegonga nyuma ya magari mengine zaidi ya matukio matatu.
Halafu hii ya kugonga nyuma sijui niaje aisee! Kuna dada mmoja alinigonga kwa nyuma, unajua kuna ile unaona kabisa ajali inakuja soon...

Ni KM chache sana kufika ilula ukitokea Iringa mjini (hilo eneo ni lile lenye upepo mwingi kwa wale wanaoijua hiyo njia) yule dada alikua na Suzuki Swifty sasa mbele yangu kulikuwa na Lorry limepata break down mie nimesimama kupisha gari za upande wa kulia zipite ili na mimi nipite.

Namuona kwenye rear view mirror anakuja tu napiga honi na hazard juu ila ndo kwanza kafunguka ghafla nikasikia kishindo!! Ikabidi nishuke namkuta anavuja damu mdomoni na puani anatetemeka hatari[emoji1787][emoji1787]. Samahani sana kaka huku anafuta damu, nikamwambia shuka nikusogezee gari pembeni kabisa ya barabara.

Aliposhuka nikamwambia kaa chini utulie nikaiweka ile gari nje kabisa ya chaki nikacheki gari yangu nyuma wala haikuumia na kubonyea zaidi ya minor scratches kwenye bampa, gari ya yule dada hood ilipinda na pia rejeta ilikuwa inavujisha. Dada alikua kafungulia mziki mkubwa nadhani ile ilimpotezea umakini.

Kaka samahani sana mi mtumishi (nurse) nimetoka manispaa nimehamishiwa ilula ndo naenda kuripoti, nikamwambia awe makini na asiendeshe gari na kobazi kama sio mzoefu ni hatari. Basi nikaondoka zangu huku nikimwambia ajaribu kwenda mdogo mdogo hadi ilula.

So mkuu hawa wanaogonga kwa nyuma ni ajali kama ila hii mara nyingi ni uzembe wa dereva.
 
Yes pale unapata nyama nzuri na ukisukumia red bull yako na maji,usingizi hamna hadi tunduma!,sunset ikikukuta pale ni safi sana kuna view nzuri ya kijani kibichi
Sure na kuna eneo mbugani lina greenish nzuri sana kwanza ukifika hilo eneo unafeel tofauti kabisa aisee wanavyosema tutunze mazingira wako sahihi miti inasaidia sana kuboresha hali ya hewa
 
Nadhani pale Ruvu Darajani ndio point ya mwisho ya kuwindana, zamani ilikua ukiimaliza Mlandizi tu tayari upo salama. Ila kwa sasa baada ya Ruvu huko mbele kiatu tuuu, ukishaivuka Chalinze ndio kabisaaa waleteee wewe unadili na taa za wanaokuja na vicheche tu. Barrier moja tu pale maeneo ya Mwidu nadhani ambao peace [emoji3577] tu wao, from there kiatu.
Umeimeza hii njia vizuri kabisa. Mule mule tu
 
IMG_20221227_112201.jpg
IMG_20221227_112158_1.jpg
IMG_20221227_112153_2.jpg


Crossing the new Wami bridge.
 
Sasa mkuu trip hii nimeona gari nyingi za kijapan zimechemka hasa harrier tako la nyani. Nilichoona wengi wamefungua bonnet wanajaza maji. Wengi wanajisahau kukagua radiator. Katika vitu muhimu usisahau kukagua radiator. Hakikisha radiator yako iko vizuri.
Hii kitu tangu mdogo nimekariri, sijawahi sahau maisha mbaka kesho. Hata mjini hii tabia ninayo na nadhani huwa inaniokoa sana mana safari za mkoa gafla huwa ni wese tu tekee
 
Back
Top Bottom