Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Wanaposema kusafiri na gari safari ndefu unapofika safari usilizime hapo hapo linabaki silence kwa mda kidogo, hii ilikuwa kwa magari ya zamani au hata ya sasa? Au dhana hiyo haipo kabisa?
Labda kwa gari ambayo ina turbo charger, Ila kwa gari za kawaida ni Bora kuizima since engine ina jipooza na kumaintain joto kupitia engine cooling system. Kama ushagundua ukipiga long trip afu ukasimama mara nyingi radiator inawasha the extra fan, ili kupoozesha engine, so hapo gari inatumia extra effort kupooza, tofauti ukiwa upo race upepo wa njiani unasaidia kupooza engine.
 
Duh hatari sana. So far njia ya kaskazini sijasikia ajali mbaya. Ila nimeshangaa sana nimekuta watu wamegonga nyuma ya magari mengine zaidi ya matukio matatu.
Watu wanaendesha kama wako dar, bumper to bumper, hakuna safe following distance. Wa mbele akifunga breki say kwenye tuta - gari zinageuka behewa za treni.
 
Halafu hii ya kugonga nyuma sijui niaje aisee! Kuna dada mmoja alinigonga kwa nyuma, unajua kuna ile unaona kabisa ajali inakuja soon...

Ni KM chache sana kufika ilula ukitokea Iringa mjini (hilo eneo ni lile lenye upepo mwingi kwa wale wanaoijua hiyo njia) yule dada alikua na Suzuki Swifty sasa mbele yangu kulikuwa na Lorry limepata break down mie nimesimama kupisha gari za upande wa kulia zipite ili na mimi nipite.

Namuona kwenye rear view mirror anakuja tu napiga honi na hazard juu ila ndo kwanza kafunguka ghafla nikasikia kishindo!! Ikabidi nishuke namkuta anavuja damu mdomoni na puani anatetemeka hatari[emoji1787][emoji1787]. Samahani sana kaka huku anafuta damu, nikamwambia shuka nikusogezee gari pembeni kabisa ya barabara.

Aliposhuka nikamwambia kaa chini utulie nikaiweka ile gari nje kabisa ya chaki nikacheki gari yangu nyuma wala haikuumia na kubonyea zaidi ya minor scratches kwenye bampa, gari ya yule dada hood ilipinda na pia rejeta ilikuwa inavujisha. Dada alikua kafungulia mziki mkubwa nadhani ile ilimpotezea umakini.

Kaka samahani sana mi mtumishi (nurse) nimetoka manispaa nimehamishiwa ilula ndo naenda kuripoti, nikamwambia awe makini na asiendeshe gari na kobazi kama sio mzoefu ni hatari. Basi nikaondoka zangu huku nikimwambia ajaribu kwenda mdogo mdogo hadi ilula.

So mkuu hawa wanaogonga kwa nyuma ni ajali kama ila hii mara nyingi ni uzembe wa dereva.
Kugonga kwa nyuma mara zote ni uzembe wa dereva except within 25 meters of an intersection (mtu kuchomekea)
 
Wanaposema kusafiri na gari safari ndefu unapofika safari usilizime hapo hapo linabaki silence kwa mda kidogo, hii ilikuwa kwa magari ya zamani au hata ya sasa? Au dhana hiyo haipo kabisa?
Ni kama kupooza pasi kwa kuiacha kwenye moto... Unachezea tu luku .

Gari inapata joto zaidi ikiwa 'silencer' kuliko ikiwa inatembea highway.

Kwa engine za turbo lakini unahitaji kuiacha kidogo joto la turbo lilingane na la engine yote

N.B fuata ushauri uliopo kwenye service manual yako ya gari
 
Watu wenye BMW au VW wanaweza kuishi na hio taa miaka. Ndio maana ni ya njano sio nyekundu. Kama issue ni serious gari yenyewe inaingia kwenye LIMP MODE.
professional Driver
I can attest to this! Ukifanya dpf na egr delete, fault ya oxygen sensor utokea mara kadhaa. Na ni kweli kabisa kama ni jambo la hatari kabisa, gari huwezi kuendesha, limp mode itakuja.
 
Back
Top Bottom