Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Kipigo cha bao 1-0 kwenye derby ya Kariakoo kimewaibua Wazee wa klabu ya Simba, ambao sasa wametoa siku saba kwa mawaziri ambao wanawashutuma kwa kile wanachodai kuwa ni hujuma dhidi ya klabu yao. Wazee hao wanadai kuwa baadhi ya viongozi wa Serikali, TFF, GSM na Yanga walihusika katika mpango wa kuihujumu Simba kwenye mchezo wa Oktoba 19 ambao umezua gumzo.
Kwa mujibu wa madai yao, kikao cha siri kilifanyika usiku wa manane, saa tisa, kikiwahusisha mawaziri sita pamoja na mwamuzi wa mchezo huo, Ramadhan Kayoko. Wazee wa Simba wanasema kuwa lengo la kikao hicho lilikuwa kuhakikisha timu ya Wananchi, Yanga, inashinda mechi hiyo kwa kuwa ni timu inayoungwa mkono na Serikali.
Soma Pia: FT: Simba 0 - 1 Yanga | NBC Premier League | Benjamin Mkapa Stadium | Oktoba 19, 2024
Katika hatua hiyo, Wazee wa Simba wamewataka mawaziri hao kutoa ufafanuzi ndani ya siku saba, wakisisitiza kuwa hujuma hizi zinaathiri ushindani wa haki katika soka la Tanzania.