Wazee wa Simba wagundua mbinu zilizo wahujumu mechi ya derby

Sababu za kijinga kabisa kutoka kwa wazee wangu wa Simba. Leo TFF kumpanga yule mwamuzi inakuwaje ni hujuma wakati sote tunajua yule mwamuzi ni pro simba siku zote na mechi nyingi tu alishawahi kutubeba?

Mechi dhidi ya Azam, simba tulishinda magoli mawili ambayo yote yalikuwa offside, vipi TFF hawakuhusika kutubeba?

Mechi dhidi ya Dodoma Jiji, Simba tulishinda goli moja la mchongo sana baada ya kupewa penati ya uongo, TFF walikuwa wapi?

Mechi dhidi ya Coastal, Simba tulitoa sare ya kubebwa wazi wazi, vipi TFF ilikuwa ni nyingine?
 
kwamba mwigulu ndio alimuagiza Camara kuutemea mpira ndani na kijili kujifunga. Kwamba Mwigulu ndio kasajili akina Nouma, Ateba, Mukwara na Okajepha.

Hawa watu wamepagawa, sasa wanatafuta sehemu ya kufia. Kwamba simba haitakiwi kufungwa? Sasa si wacheze peke yao pale Bunju ili wasifungwe au waanzishe ligi yao.

Inasikitisha kwa kweli.
 
Kama kuna nguvu kubwa kiasi hicho nyuma ya hao, basi tungetegemea wafunge magoli kama me-a see-tar hivi!

Sasa kama wanaosaidiwa hivyo ni wabovu kiasi kile, mbona hawa wengine nao wana nafasi kubwa ya kuwabamiza tu!

Au nao watakuwa ni wabovu vilevile kwa kumwogopa mpinzani mbovu?

According to Trump, ^Make it TOO BIG TO RIG!^ Just excel their cheat! A simple trick for the trade. It always works so seamlessly.
 
Mimi Abuu Kauthar wa hapa Holili, nashauri TFF fungia hao wazee wa makolo, enyi wazee wa makolo mtatafuta mchawi hadi lini. Kaeni chini muyamalize migogoro si mizuri
 
Ujinga mtupu.
 
Hawa wazee shule hamna. Wameidhalilisha sana hiyo timu yao kwa kubwabwaja bila facts na logic
2. Wanatishia kuharibu uwanja wa Taifa. Serikali iwamulike hawa na kuwachukulia hatua
3. Haileweki hoja ya msingi ni ipi. Mara kayoko, GSM, udhamini vilabu nane, Mwigulu Nchemba, Tozo, Ccm na ujinga mwingine mwingi.
JE HUU NDIO MSIMAMO WA SIMBA KAMA TAASISI??
 
Hii dunia ngumu sana, quality ya wachezaji wa Simba ni ndogo sana ukilinganisha na wa Yanga. Kwa mtu anayejua mpira game ya juzi Yanga hawakuwa katika ubora wao.oilily tashangaza hata game ya mzunguko wa pili Simba kufungwa labda waongeze wachezaji wenye quality zaidi
 
Ni ujinga uliopitiliza kulazimisha Yanga kushinda kila mara.

Ligi inaonekana ya kijinga na nchi nzima tunaonekana hatuna akili.
 
Ukiachana na ushabiki.... Endapo hizo tuhuma zipo basi zinapaswa kushughulikiwa kwa akili na hekima.


Siku sijazo tutaanza kuona mambo ya awamu ya nne yakifanyika uwanja wa taifa tena kwa ujasiri sana.


Hao mawaziri wanne na TFF kwa ujumla wajiangalie.

Nimeanza kuelewa kwanini Taifa Stars ikipoteza watu wengi wanafurahi(hapa wengi ni mashabiki wa simba).

Wanasiasa wa upinzani wanaweza tumia huu kama mwanya wa kiasa na wakafanikisha mambo yao mengi sana katika kuwa laghai mashabiki wa simba.


Lakini yanini yote hayo ya mawaziri kufanya hujuma dhidi ya Simba wakati Yanga bado inateam nzuri tena yenye mbinu kedekede za ndani ya uwanja za kushinda dhidi aya wapinzani wao.
 
Tabia zote walizonazo Mashabiki wa Simba wamerithi Kwa Hawa Wazee.,.!

Wakati Simba akiwa kwenye Ubora wake, Mashabiki wa Yanga na mimi nikiwemo tulikua tunakubari kwamba Simba Kwa Sasa Wana Kikosi Bora..!

Na sisi tulikua tunaamini utafika wakati tukipata Mdhamini tutakua na Team Bora, Mungu si Mangungu GSM kaja, kabadirisha kila kitu, Leo Simba hawataki kukubari kuwa Yanga we ana Team Bora Kwa Sasa,....!

Tutachukua Ubingwa Mfululizo miaka 10.
Tutawafunga Mfululizo mpaka Mkuubari kuwa Yanga wametuzidi.
 
hiyo namba 5 nimecheka sana...wakati yanga wanajiita wananchi wao si walijiita wenye nchi sasa walizubaa wapi wananchi kuishinda serikali amabyo ni guvu moya?nyie wazee kaeni nyumbani mlee wajukuu mpira ni burudani ya vijana
 
Mnakimbilia serikali kwanini msiseme fifa au Tff. Kumbe kiongozi wa Tff mke wakeamepewa kazi na Gsm na mwingine Bodi ya ligi kampuni yake imepewa tenda ya kufagia na Gsm.
Ngoja tule mtori nyama ipo chini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…