MR TOXIC
Senior Member
- Jun 4, 2019
- 190
- 525
Bila aibu Ummy Mwalimu amesema ajira 1360 za walimu wa physics na 599 za walimu wa hesabu kwamba zimemaliza tatizo la uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi nchini.
Kwangu kauli hiyo ya Ummy naona inalenga kutafuta umaarufu wa kisiasa kwani alichokisema ni uongo unaofaa kupuuzwa na kila mtu mwenye akili timamu.
Na , mawaziri kama hawa ni sampuli ya viongozi ambao Antony mtaka anasema hawana uchungu na elimu ya watoto wa watanzania maskini isipokuwa wapo kwaajili ya maslahi yao binafsi na familia zao.
Huku kwetu kila mwezi wazazi tunachanga elfu tatu kwaajili ya kulipa walimu wa temporary kufundisha watoto wetu kutokana na shule kutokuwa na walimu wa sayansi lakini waziri huyu bila hata hiyana anasema hakuna uhaba wa walimu wa sayansi. Hivi waziri kama huyu anafaa kuendelea kuwa msimamizi wa elimu yetu?
Au kwakuwa mtoto wake hasomi shule za kata ndio maana analeta siasa kwenye elimu kwakuwa anajua wanaoathirika sio watoto wake?
Huyu dada ni miongoni mwa mawaziri niliokuwa naona wana vision ya kiuongozi lakini kidogo kidogo ameanza kupotoka kupitia kauli na matamko yake ya kutafuta sifa za kisiasa kwenye mambo ya msingi.
Again, I stand with Antony Mtaka kwenye elimu