Waziri aagiza dereva wa gari aliyemgomea trafiki anyang'anywe leseni

Waziri aagiza dereva wa gari aliyemgomea trafiki anyang'anywe leseni

Dereva na Traffic wote wana matatizo, dereva alipaswa kutii amri ya kusimama, na traffic hakupaswa kuzuia gari kwa mikono . Wote wapimwe afya ya akili
 
Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini ameagiza kukamatwa na kuchukuliwa hatua kwa dereva ambaye ameonekana katika kipande cha video fupi akiendelea kuendesha gari aina ya Nissan huku mbele yake kukiwa na askari wa Usalama Barabarani.

Amesema “Apelekwe kwenye vyombo vya dola na leseni tuliyompa anyang’anywe kabisa, haiwezekani askari yupo kazini anakuzuia wewe unampelekea gari, nina wasiwasi na akili za madereva wetu sasa hivi, lazima atakuwa na shida mahali.”
Kwakweli amefanya makosa. Unless kama gari lilifeli breki.
 
Afisa usalama wa barabarani Hana akili hata punje.Kichwa chake ni kama Cha prawns,kimejaa mavi.Hana job description yake?Alipaswa kuzuia gari Kwa mikono? Wanataka kumnyang'anya leseni dereva,je wanauhakika ana leseni au ni mvuta bange kaingia na gari barabarani?Alitakiwa awe na namba ya gari bas ili isiingie barabarani.Usalama wake ni muhimu kuliko kitu chochote.
 
Magari kama haya yawe tu yanaingia kwenye mikono ya serikali moja kwa moja, gari la hivi litaifishwe kabisa na kuwa gari la umma likasaidia kazi nyingine za maendeleo ya kitaoifa, kama trafiki kafanyiwa hivi, vipi bodaboda, vipi mtembea kwa miguu, huu ni utovu wa nidhamu na dharau, serikali chukueni hilo gari, ashike adaby katika maisha yake yote na iwe fundisho kwa wengine, hiyo ni maana kwamba alikusudia kumuua huyo trafiki.
 
Pana watu wana Stress balaa unawaona wanaendesha huku hawapo hapo wapo Trafik wamewahi kugongwa na wengine kupoteza maisha kwa hizo mambo...sheria ya waziri kuchukua leseni ya Mwananchi kaitoa wapi...
 
Inawezekana matukio kama haya yanatokea sana ila tu hayarekodiwi na kusambazwa mitandaoni kama hili.
 
Pana watu wana Stress balaa unawaona wanaendesha huku hawapo hapo wapo Trafik wamewahi kugongwa na wengine kupoteza maisha kwa hizo mambo...sheria ya waziri kuchukua leseni ya Mwananchi kaitoa wapi...
upo sahihi mkuu, nawajua wawili waliogongwa .
 
Tungeanza na kuwa na wasiwasi na akili za askari wa barabarani kwa kutotumia akili na maarifa,
Nini maana ya gari kusajiriwa na kuwa na namba?
Mtu unarisk maisha yako kwa ujinga mtupu?
Ningekuwa waziri ningeanza na huyo polisi ndo dereva wa nissan afuatie,ila waswahili wanasema akili ni nywele kila mtu ana zake
 
Unaleta unaa unakufa,huyu traffic amenikumbusha afisa wa wanyamapori aliyejitosa mtoni kuogelea kufata jangili matokeo yake akaishia kuzikwa
Kulikuwa na haja gani kusimama mbele ya gari ikiwa gari ina plate namba?
 
Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini ameagiza kukamatwa na kuchukuliwa hatua kwa dereva ambaye ameonekana katika kipande cha video fupi akiendelea kuendesha gari aina ya Nissan huku mbele yake kukiwa na askari wa Usalama Barabarani.

Amesema “Apelekwe kwenye vyombo vya dola na leseni tuliyompa anyang’anywe kabisa, haiwezekani askari yupo kazini anakuzuia wewe unampelekea gari, nina wasiwasi na akili za madereva wetu sasa hivi, lazima atakuwa na shida mahali.”
very bad!
 
Ndiyo maana mimi huonekanaga sina dogo katika jamii, kila jambo napenda litafsiriwe kisheria zaidi!

Naanza kujihoji:

Je, video clip hiyo ni hai au mfu, ilichukuliwa lini na wapi?

Je, ninani kwa jina aliyerekodi na kurusha clip hiyo?

Je Trafiki huyo anaitwa nani na anafanyia wapi kituo chake cha kazi?

Je ni umbali gani alipokuwa amesimama Trafiki huyo huku akionesha ishara ya kuisimamisha gari, kabla ya gari hiyo haijamsogelea na kufanya kituko hicho?

Je Trafiki aliripoti tukio hilo popote?

Na kama hajaliripoti ni kwanini?

Je dereva wa gari kahojiwa na kusikilizwa dhidi ya tuhuma hiyo?

Je anaitwa nani na anaishi wapi?

Je gari lake halikuwa na matatizo ya breki?

Kama lilikuwa na tatizo, angelitumia njia gani kuokoa maisha ya askari zaidi ya kumpigia honi apishe kwa ajili ya usalama wake?

Kama gari halikuwa na matatizo, je ni sababu gani iliyosababisha kuendesha huku mbele yake kuna mtu?

Je kusimama mbele kama gogo ama kizingiti ni njia sahihi kutumiwa na askari Polisi mweledi?

Je ni hatua gani huchukuliwa kwa dereva anayekaidi kusimamishwa na Trafiki?

Je Trafiki alishindwa kuchukua hatua za kisheria za mtu anayekaidi kusimamishwa hadi kupelekea akasimame mbele ya gari kama kizingiti?

Je wawili hao (dereva na Polisi) hawajahi kuhitilafiana kwa ishu yoyote kabla ya tukio hili?

Je ukiacha video clip hii, kuna mashahidi wengine walioshuhudia tukio kuweza kuelezea mwanzo mwisho wa dhahama hii?
Je...je...je.. to infinity!
 
Back
Top Bottom