DOKEZO Waziri Angela Kairuki hili la Kilwa litakuondoa madarakani Rais Samia akijua

DOKEZO Waziri Angela Kairuki hili la Kilwa litakuondoa madarakani Rais Samia akijua

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Desprospero

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2023
Posts
1,015
Reaction score
2,493
Rais Samia Suluhu Hassan amejipambanua kuwa ni msikivu kwa watu anaowaongoza. Samia amerejesha uongozi shirikishi. Kwamba unapotaka kuwaletea maendeleo wananchi basi uwashirikishe Ili kujua nini kipaumbele chao. Usilazimishe kuwajengea daraja kumbe shida yao ni kisima cha maji nakadhalika.

Sasa turudi Wilaya ya Kilwa kwa DC. Christopher Ngubiagai ambako dhana ya ushirikishwaji wananchi ni dhambi ya mauti maana fedha zimeliwa tayari na "Mchwa".

Mvutano ni mkubwa wilayani Kilwa, wapi pajengwe Makao Makuu ya Wilaya hiyo baada ya "Wajanja" kulamba asali ya Samia zaidi ya Sh. 2.1 Bilioni na kuamua kuwapuuza wananchi wanaotaka Makao Makuu ya Wilaya yabakie Kilwa Masoko ambako tayari kuna mahitaji yote ya kiutawala na kutaka kuyapeleka Lingaula (kitongoji kati ya Nangurukuru na Mavuji) eti kujenga jengo moja tu la utawala.

Ununuzi wa eneo hilo ndipo fedha za Samia (Serikali) zilipopigwa na madiwani "Waliojiongeza" kimapato.

Serikali ya Samia ilitoa hela zaidi ya 2.1 kujenga Makao Makuu Kilwa Masoko ambako ni senta ya Wilaya ikiwa tayari ina mahitaji yote muhimu ya kijamii kama Polisi, Benki, Mahakama, Bandari, NIDA, Ofisi ya Vizazi na Vifo, Posta nakadhalika. Then "wapigaji" wakaona wapeleke makao hayo zaidi ya kilometa 40 kutoka walipo wana-Kilwa wengi. Akili za kishetani.

Wapigani wanajisahaulisha kwamba tayari Serikali ilishaingia gharama kubwa kujenga HQ Kilwa Masoko ambapo sasa wanataka Serikali iingie tena gharama za kujenga nyumba za watumishi na kulipa fedha za uhamisho. Wapigaji Kilwa shikamoo.

Kwamba hata ripoti ya wataalamu wa miamba na ardhi kwamba Lingaula kuna ardhi yenye sumu katika maji na kwamba hakuna nyumba iliyowahi kujengwa hapo ikabaki salama bila kupasuka na kuanguka ni upuuzi kwa wapigaji.

Yaani wapigaji hawaoni usumbufu watakaopata watalii watakaolazimika kusafiri kilomita 80 kusaka vibali vya kuona mji-kale kutoka Kilwa Masoko kwenda Lingaula na kurudi. Kwao hili ni giza maana "Washalamba asali ya mama" na baya zaidi ni hela za Uviko-19 ambayo Rais Samia alisema, "Ukitaka kujua rangi yangu dokoa hizi hela". Wapigaji Kilwa hawajui cha rangi ya Mama wala sura. Ni kupiga tu.

Tarehe 09/06/2022 wananchi wanaamua kufanya mkutano na kuamua kwa pamoja kwamba "Sisi ndio wenye Kilwa yetu, tunajua jiografia na mazingira yetu, tunataka Makao Makuu yetu yawe hapa Masoko tusilazimishwe tusikopenda".

Wananchi wanaamua kukuandikia barua wewe Waziri Angela Kairuki kutengua maamuzi ya wapigaji bila majibu. Wananchi wanaamua kujichangisha kiasi cha shilingi 1,050,000 ya kuwapeleka wajumbe Dodoma kukueleza kwa mdomo ana kwa ana lakini wanafungiwa milango wasisikilizwe. Wanarudi Kilwa kwa masikitiko makubwa. Hawaamini ni Serikali ya Samia au nyingine.

Yaani wananchi zaidi ya 61,000 wanasaini kwenye karatasi kwamba Makao Makuu ya Wilaya ya Kilwa yabakie Kilwa Masoko kuliko na huduma zote tayari ikiwemo hata uwanja wa ndege lakini "Wapigaji" hawataki. Na wewe Waziri Kairuki unawasikiliza wapigaji. Dah, Samia kazi anayo.

DC anaulizwa anasema, "Mimi ni mgeni, nimesikia malalamiko ya wananchi hao, ila nimekuta yalipitishwa huko nyuma wakati huo Halmashauri iliongozwa na madiwani wa CUF", anaishia hapo. Kichekesho.

"Wapigaji" tayari wameanza ujenzi wa jengo la Utawala na DC anashindwa kuusimamisha pamoja na kelele za umma kutaka kushirikishwa. Wapigaji wanaamini Kilwa ni mbali Samia hawezi kujua leo wala kesho.

Dada yangu Angela Kairuki njoo Kilwa utusikilize wananchi vinginevyo wewe ni sehemu ya wapigaji na kama wewe ni sehemu yao basi hufai, jipime achia ngazi. Ova!
 
Aondolewe? Kazi ya kumuondoa mtu unadhani kila mtu anaweza?
 
RAIS Samia Suluhu Hassan amejipambanua kuwa ni msikivu kwa watu anaowaongoza. Samia amerejesha uongozi shirikishi. Kwamba unapotaka kuwaletea maendeleo wananchi basi uwashirikishe Ili kujua nini kipaumbele Chao....
Kwa hiyo kati ya masoko na nangurukuru ni wapi center ya wilaya ?
 
Nimeishi Kilwa Kwa zaidi ya miaka 2 sasa, kitu nilichojifunza kutoka Kwa wenteji ni kwanba mnajifanya wajuaji huku hamba kitu mnajua.

Mleya maada unataka kumlaumu DC Bure; kasema ukweli kuwa yeye ni mgeni na kakuta maamuzi yalishafanyika; huu ndio ukweli. Unataka DC afanye je, au mnamtafutia sababu ya kumuondoa?

Badala ya kuelekeza lawama Kwa DC na Waziri nadhani ungeelekeza lawama Kwa Baraza la madiwani; hapo ndipo shida zinspoanzia.

Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri was haya mambo rejea ule mgogoro wa Kijiji Cha Njinjo na Nakingombe kuhusu wapi Zahanati ya kata ilipaswa kujengewa ndio utaelewa nibachokisema.

By the way mlifurahi sana yule dada kutumbuliwa, ata tuone huyu DC mpya.
 
Back
Top Bottom