Waziri Aweso ameigiza kuwasimamisha watendaji wa wizara yake walioko Morogoro

Waziri Aweso ameigiza kuwasimamisha watendaji wa wizara yake walioko Morogoro

Zygot

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2016
Posts
2,319
Reaction score
3,128
Kwa uchunguzi wangu nimestukia maamuzi haya kwa sababu kama ni ubadhirifu ulianza zamani wakati Aweso akiwa Naibu waziri, kwa nini hakuona tangu zamani?

Umbea wangu hatimaye umeangukia pazuri. Waziri Aweso anaigiza na huenda alikuwa ni sehemu ya ufisadi huu. Hii ni kutokana na urafiki wake wa karibu na mkurugenzi wa Bonde la Wami Ruvu, aliyemsimamisha. Yaaminika huyu ni rafiki yake pamoja na aliyekuwa katibu mkuu, bw. Kitila Mkumbo. Hawa watu watatu. Aweso, Mkumbo na mkurugenzi, wanafahamiana, wanajua walichokuwa wakifanya. Kinachofanyika kwa sasa ni maigizo ya kuonesha umahili wa kazi ya waziri. Badala ya kuwachunguza watendaji hawa wawili, wote wachunguzwe kwa pamoja.

Aweso.jpeg
 
Mawaziri hawa wanaojiita vijana ni tatizo kubwa la nchi. Halafu kule Bungeni nasikia spika akilaani uaminifu mdogo wa vijana. Vijana mitaani hawana mfano mzuri wa uaminifu. CAG anasema wazee maofisini ni wezi, hao wazee ndo unawaomba wafundishe maadili?

Kama Aweso alikuwa wizara hiyo na watendaji hao. Mkumbo naye akiwa wizara hiyo na watendaji hao. Angalia multiplier effect sasa; Aweso ni waziri na mkumbo ni waziri. Kama ni tabia yao sasa wameimarisha ufisadi wao na huenda hata huku kusimamishwa ni makubaliano, kwamba sasa mimi natangaza kukusimamisha maana baadaye tutajulikana.
 
Back
Top Bottom