Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amezungumza na wahitimu kwenye Mahafali ya 48 ya Chuo cha Maji, yaliyofanyika leo tarehe 13 Novemba 2024, kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, akiwa mgeni rasmi.
Akizungumza katika hafla hiyo, Aweso amesema: "Mimi familia yangu ni masikini, nimefikia uwaziri kutokana na elimu. Naamini kupitia elimu mtoto wa Mama Ntilie anaweza kuwa mhandisi tegemezi katika taifa hili. Katika nafsi yangu naamini mtoto wa maskini kabisa anaweza kuwa mkuu wa chuo cha maji kupitia elimu. Wazazi na walezi hamjakosea na hautapata hasara kuwekeza katika elimu. Leo mnaniita Waziri wa Maji, familia yangu ni masikini kabisa, mtoto wa Mama Ntilie, lakini nimesoma, nimekuwa mkemia, nimekuwa naibu Waziri, na leo nimekuwa Waziri kwa sababu ya elimu."
Soma, Pia: Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameahidi kuendelea kuzitafutia ufumbuzi changamoto katika Chuo cha Maji