Waziri Aweso: Familia yangu ni masikini, nimepata Uwaziri kutokana na elimu

Hawa mawaziri wa TZ chenga sana sana...wanaona umaskini ni sifa wakati wao ndio wanausababisha.
Masikini ni wengi, watu wengi ni mtaji wa kura, ni mara chache sana mwanasiasa atasema ametoka familia ya kitajiri isiyojua shida ni nini ili akose kura.
 
Kwahiyo chuo cha maji wanasomea nini? Mbona Tanzania maji safi bado ni changamoto? Hao wanafunzi wakigraduate huwa wanaenda wapi?
Hili nalo swali zuri sana. Maana mvja zinanyesha lakini jua kidogo utasiki mgao wa maji. Kama sie wa mororgoro tumechoshwa kabisa na hawa maengineer
 
Masikini ni wengi, watu wengi ni mtaji wa kura, ni mara chache sana mwanasiasa atasema ametoka familia ya kitajiri isiyojua shida ni nini ili akose kura.
Rizwani,Makamba,Mbowe watoto wa kishua ila huwa hawajisifu,sasa huyu mtoto wa mama nntilie kadigree kamoja kelele mlimani city yote,utafikiri umadikini ni sifa
 
  • Kicheko
Reactions: Tsh
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amezungumza na wahitimu kwenye Mahafali ya 48 ya Chuo cha Maji, yaliyofanyika leo tarehe 13 Novemba 2024, kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, akiwa mgeni rasmi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Aweso amesema: "Mimi familia yangu ni masikini, nimefikia uwaziri kutokana na elimu. Naamini kupitia elimu mtoto wa Mama Ntilie anaweza kuwa mhandisi tegemezi katika taifa hili. Katika nafsi yangu naamini mtoto wa maskini kabisa anaweza kuwa mkuu wa chuo cha maji kupitia elimu. Wazazi na walezi hamjakosea na hautapata hasara kuwekeza katika elimu. Leo mnaniita Waziri wa Maji, familia yangu ni masikini kabisa, mtoto wa Mama Ntilie, lakini nimesoma, nimekuwa mkemia, nimekuwa naibu Waziri, na leo nimekuwa Waziri kwa sababu ya elimu."
Soma, Pia: Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameahidi kuendelea kuzitafutia ufumbuzi changamoto katika Chuo cha Maji
Elimu ni nini? Ametatua tatizo gani na hiyo elimu?
 
Piga kitabu hatari ila mtaani patupu mtu km huyu akisema bora angezaliwa paka ulaya msikilize mara 2 usimpuuze
Kabisa mzeya wala huwezi mlaumu kwa hali ilivyo. Akikumbuka alivyokuwa analoweka miguu kwenye beseni asime alafu mtaa i anaambulia patupu...inauma.
Bora mie back bencha nilikuwa naenjoy life zaidi ya masomo sasa nafukuza upepo na boxer ya gu na kula wake wa watu na watoto wa fomu fooo B maisha yanaenda
 
Rizwani,Makamba,Mbowe watoto wa kishua ila huwa hawajisifu,sasa huyu mtoto wa mama nntilie kadigree kamoja kelele mlimani city yote,utafikiri umadikini ni sifa
🤣 🤣 🤣
 
Umasikini sio sifa ya kujivunia. Hakuna Nobility kwenye umasikini. Na usitumie umasikini kutafuta hururma.
 
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amezungumza na wahitimu kwenye Mahafali ya 48 ya Chuo cha Maji, yaliyofanyika leo tarehe 13 Novemba 2024, kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, akiwa mgeni rasmi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Aweso amesema: "Mimi familia yangu ni masikini, nimefikia uwaziri kutokana na elimu. Naamini kupitia elimu mtoto wa Mama Ntilie anaweza kuwa mhandisi tegemezi katika taifa hili. Katika nafsi yangu naamini mtoto wa maskini kabisa anaweza kuwa mkuu wa chuo cha maji kupitia elimu. Wazazi na walezi hamjakosea na hautapata hasara kuwekeza katika elimu. Leo mnaniita Waziri wa Maji, familia yangu ni masikini kabisa, mtoto wa Mama Ntilie, lakini nimesoma, nimekuwa mkemia, nimekuwa naibu Waziri, na leo nimekuwa Waziri kwa sababu ya elimu."
Soma, Pia: Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameahidi kuendelea kuzitafutia ufumbuzi changamoto katika Chuo cha Maji
Haka kajamaa tangu kapo udsm na kudahiliwa Makirikiri kana Nyodo sana
 
Back
Top Bottom