Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amezungumza na wahitimu kwenye Mahafali ya 48 ya Chuo cha Maji, yaliyofanyika leo tarehe 13 Novemba 2024, kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, akiwa mgeni rasmi.
Akizungumza katika hafla hiyo, Aweso amesema: "Mimi familia yangu ni masikini, nimefikia uwaziri kutokana na elimu. Naamini kupitia elimu mtoto wa Mama Ntilie anaweza kuwa mhandisi tegemezi katika taifa hili. Katika nafsi yangu naamini mtoto wa maskini kabisa anaweza kuwa mkuu wa chuo cha maji kupitia elimu. Wazazi na walezi hamjakosea na hautapata hasara kuwekeza katika elimu. Leo mnaniita Waziri wa Maji, familia yangu ni masikini kabisa, mtoto wa Mama Ntilie, lakini nimesoma, nimekuwa mkemia, nimekuwa naibu Waziri, na leo nimekuwa Waziri kwa sababu ya elimu."
Umetoka katika familia ya kimasikini lakini baada ya kujiunga na kikundi cha wachawi wamekufundisha kuwa na roho mbaya na kuwachukia masikini na kugeuka kuwa fisadi.
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amezungumza na wahitimu kwenye Mahafali ya 48 ya Chuo cha Maji, yaliyofanyika leo tarehe 13 Novemba 2024, kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, akiwa mgeni rasmi.
Akizungumza katika hafla hiyo, Aweso amesema: "Mimi familia yangu ni masikini, nimefikia uwaziri kutokana na elimu. Naamini kupitia elimu mtoto wa Mama Ntilie anaweza kuwa mhandisi tegemezi katika taifa hili. Katika nafsi yangu naamini mtoto wa maskini kabisa anaweza kuwa mkuu wa chuo cha maji kupitia elimu. Wazazi na walezi hamjakosea na hautapata hasara kuwekeza katika elimu. Leo mnaniita Waziri wa Maji, familia yangu ni masikini kabisa, mtoto wa Mama Ntilie, lakini nimesoma, nimekuwa mkemia, nimekuwa naibu Waziri, na leo nimekuwa Waziri kwa sababu ya elimu."
Kwanza miniseme tu....
Umasikini sio sifa na sio vyema kupenda kutumia historia ya umasikini ili kuonewa huruma.
Kama ni uwaziri ameupata sababu ya siasa na sio elimu.
Umaskini sio jambo la kujivunia waziri aweso. Aache kuwapiga kamba wahitimu. Wawezeshe hawa wahitimu kwa wao mawaziri kukataa kutembelea latest land cruisers.