tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,040
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Gabriel Makalla, amekutana na Waziri wa Maji, Jumaa Hamidu Aweso, leo Jumatatu Novemba 24, 2025, wakizungumza kuhusu utekelezaji wa miradi ya maji mkoani Arusha.
Katika mazungumzo hayo, Makalla ameonyesha kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi inayoendelea katika maeneo mbalimbali ya mkoa, huku akieleza mkakati wa Arusha wa kudhibiti wizi wa mita za maji unaojitokeza katika baadhi ya maeneo.
Makalla pia amempongeza Waziri Aweso kwa kuendelea kuaminiwa na Rais Samia Suluhu Hassan, na akaahidi ushirikiano wa karibu katika kusimamia sekta ya maji ndani ya mkoa.
“Uhodari, ubunifu na uchapakazi wako ndiyo umemshawishi Rais kuendelea kukuamini. Sisi tunaozunguka maeneo mbalimbali tunaona kazi kubwa inayofanywa na Wizara ya Maji, mijini na vijijini. Ninaridhishwa na namna tunavyoshirikiana,” amesema Makalla.
Kwa upande wake, Waziri Aweso amemshukuru Makalla kwa ushirikiano wake mkubwa na kumpongeza kwa namna anavyosimamia masuala ya maji, huku akiahidi kuendeleza misingi ya uwajibikaji na mapambano dhidi ya wizi na upotevu wa maji ambayo Makalla aliacha alipokuwa Naibu Waziri wa Maji.