Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kusema kuwa Wakazi wa Shamaliwa A na B wengi wao hawana huduma ya Maji kwa muda wa zaidi ya mwezi sasa kutokana na wahusika wanaotengeneza Barabara wameharibu mabomba, ufafanuzi umetolewa na Waziri wa Maji Jumaa Aweso.
Waziri Aweso amesema “Ni sahihi kuwa changamoto hiyo ipo katika eneo hilo na imesababishwa na matengenezo ya miundombinu ya Barabara yanayoendelea kutekelezwa na TARURA.
“Hata hivyo, Mawasiliano baina ya MWAUWASA na TARURA yamefanyika pamoja na taratibu za urejeshaji wa miundombinu ya maji iliyoharibiwa zimefanyika na zinaendelea.
“Tunatarajia hadi kufikia wiki ijayo miundombinu hiyo itaanza kurekebishwa na huduma ya maji katika maeneo hayo itaanza kurejea.”
Hoja ya Mdau, soma hapa ~ Wakazi wa Shamaliwa - Mwanza hatuna Huduma ya Maji zaidi ya Mwezi, Wanaoboresha Barabara wameharibu Mabomba