Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yapo mengi hata kupuyanga so kupuyanga bali ni kuchoma,lakn kw hili uprof wake waziri umeonekana.Katika vitu ambavyo naweza kusifia kwenye serikali hii ni Jambo hili. Ingawa mengine wanapuyanga sana.
Tofautisha hybridization na genetic modification, tumiaga akili wakati unaandika, sawa?Kitu kingine ni kuwa kiafya haya mazao hayana shida yoyote, labda yawe modified kutengeneza sumu. Hata kiasili genetic modification huwa zinafanyika. Mahindi tunayolima leo siyo yaliyokuwa yanalimwa miaka 1000 au 2000 iliyopita. Pole kwa pole yanabadilika.
Hata wakulima wenyewe wa kienyeji hufanya hii kitu. Unapokula mahindi madogomadogo na kuweka makubwa kuwa mbegu ujue unafanya genetic modification, baada ya miaka kadhaa utakuwa na mahindi makubwa tu. Kinachofanyika huko maabara ni kuharakisha tu.
Tofautisha hubridization na Genetic mofification, sawa? Mzungu akizaa na Mwafrika hiyo tunaita hybridization, ila ukichukua vinasaba vya mbwa ukavipandikiza kwenye yai la binadamu ili azaliwe binadamu mwenye uwezo wa kunusa kama mbwa hiyo ni generic modification, umeelewa?Mbona hizi mbegu zinazoitwa za kisasa (hybrid) vimetokana na technolojia ya kuboresha gene?kwa maana nyingine ni G.M.O
Wewe ndiyo huelewi hybridization ni nini na genetic modification ni nini? Kwanza hybridization inaingiaje hapa kama siyo kuchanganya mambo?Tofautisha hybridization na genetic modification, tumiaga akili wakati unaandika, sawa?
Mimi sio mtaalam sana wa masuala ya baiolojia, lakini sidhani kama unaweza kupata "hybrid" bila "genetic modification".Tofautisha hybridization na genetic modification, tumiaga akili wakati unaandika, sawa?
Hicho kinachofanya uharaka ndicho kibaya. Mkulima anapukuchua mbegu zake anahifafhi mahala salama kusubiri msimu ujao
Hayo mazao hayatakuwa na ladha ndio maana wazungu wanahangaika na viungo! Unakula nyanya haina ladha mdomoni.
Katika vitu ambavyo naweza kusifia kwenye serikali hii ni Jambo hili. Ingawa mengine wanapuyanga sana.
Hybridization ni kama kuchukua mbwa aina ya german shepherd ukampandisha na mbwa aina ya bulldog, hapo ni umechanganya mbegu ambazo zipo tayari kwenye nature kama zilivyo kwenye viumbe ili kupata zao bora zaidi.Wewe ndiyo huelewi hybridization ni nini na genetic modification ni nini? Kwanza hybridization inaingiaje hapa kama siyo kuchanganya mambo?
Hybridization haihusishi genetic modification at all, ila ni unachanganya vinasaba ambavyo vipo tayari in nature kwenye viumbe aina ile ile ili kupata kiumbe kipya na bora. Hybridization ni kama kuchukua mbwa aina ya german shepherd ukampandisha na mbwa aina ya bulldog, hapo ni umechanganya mbegu ambazo zipo tayari kwenye nature kama zilivyo kwenye viumbe ili kupata zao bora zaidi. Ila Genetic modification ni kung’oa vinasaba toka kwenye viumbe tofauti tofauti ambapo vingine hata sio vya species moja na kuunga unga kama tu anaetia viraka kwenye nguo, mfano kuna mchele wa GMO ambapo wamechukua vinasaba vya binadamu na kwenda kuviunganisha kwenye vinasaba vya mpunga ili kuikinga dhidi ya magonjwa flani flani, katika hali ya kawaida binadamu asingeweza kufanya mapenzi na mpunga ili kuzaa mtoto, lakini kwa GMO inafanyika, na hiyo ndio tofauti kubwa ya GMO na hybridization.Mimi sio mtaalam sana wa masuala ya baiolojia, lakini sidhani kama unaweza kupata "hybrid" bila "genetic modification".