Waziri Bashe acha kuchezea Kodi zetu kwa maono mfu! Kilimo siyo filamu

Sidhani kama Bashe ana muda wa kusikiliza loosers kama nyie..

 
Reactions: Ame
Kila kitu kinapingwa. Hii nchi ngumu sana, mnapinga kila kitu.
Waaache wajaribu serikali zilizopita zilileta mbinu nyingi, nao wajaribu.
Msisahau kilimo kwanza wakulima mlipewa na mbolea za ruzuku za mabilioni, kuna ubaya gani vijana kuwezeshwa. Mbona vijana mnapigana vita wenyewe?
Ombeni mradi huo upanuliwe nchi nzima sio kuupiga vita.
 
In short people can have buying power and still your product struggle to find market....
Kwanza wanasiasa wetu wanapoongea kuhusu kilimo huwa naona wanapenda sana kusema uongo. Badala ya kusema watu wetu zaidi ya 70% ni wakulima walitakiwa kusema watu hao wanajihusisha na Kilimo. Maana kilimo ni zaidi ya kulima.

La pili 80% ya mafukara wa Tanzania wanaishi vijijini ambako ndiko 99% ya chakula cha Watanzania kinatoka. Sasa hapo ni lazima wanasiasa wangeangalia ni kwa vipi watu wanaozalisha chakula wao ndiyo mafukara wa kutupwa? Kwa mfano kama kweli wanataka hiyo wanayoiita "Building Better tomorrow" ifanikiwe ni kwa nini kwanza wasingeanza na kiini cha matatizo kwa kilimo chetu.

Maana hiyo Programu yao waliyoizindua huko Dodoma, hadi iondoe umaskini kwa wakulima walioko kwenye vijiji vya Tanzania itachukua miaka mingapi? Wakati hiyo Programu inafanyika jee wakulima wadogo wa vijiji mbali mbali vya Tanzania watafaidikaje?

Mwaka 1969 Mwalimu alikuwa anahimiza wakulima kutumia Plau kulima, Punda kubebea mizigo, kuchagua mbegu bora, kuongeza mazao kwa heka, kuhifadhi chakula n.k. Jee miaka 54 baadae bado tunaona mambo haya bado hayajafanyika na hali ya wakulima vijijini ikiwa mbaya zaidi. Ila mtu anakuja na hoja kwamba BBT ndiyo mkombozi wa Kilimo Tanzania.
 
Kumbe unajua kwamba hizi comedy zipo kila awamu? Sasa tunapopinga tuheshimiwe.
 
Sidhani kama Bashe ana muda wa kusikiliza loosers kama nyie..

Karne ya Combined harvesters na machinery wanafundishwa kutumia rakes ?

Knowledge is Power na kama issue ni elimu tungeboresha vyuo vyetu vya kilimo ili elimu hio isiwe kwa vijana tu bali wakulima wote wanaovunjika migongo yao huko vijijini...

All in all tutajenga zaidi kwa kupunguza maigizo na ku-stick with basics
 
Wengi wao ni wataanza na kilimo Cha mazao ya mbogamboga,hapo hakuna hicho unachokisema wewe.
 
Kumbe unajua kwamba hizi comedy zipo kila awamu? Sasa tunapopinga tuheshimiwe.
Sio comedy watanzania ni wajinga,walipewa nbolea, mikopo aka n
mabilioni ya kikwete kila kijiji waliuza mbolea na kuila ile mikopo.
Viongizi wanamaono sana tu.
 
Kila kitu kinapingwa. Hii nchi ngumu sana, mnapinga kila kitu.
Acha hizi fikra kwamba mtu akiwa na mawazo tofauti basi anapinga.

Kwa mfano wote mnataka kwenda Chato kutembelea Kaburi la Magufuli, Mmoja akasema ili kumuenzi Seth Benjamin basi mtembee toka Dar Mpaka Chato kwa miguu, Mwingine aseme mpande Baiskeli kuenzi matumizi ya Baiskeli aliyokuwa anafanya Mwalimu Nyerere kutoka Pugu kuja Dar kuonana na wazee wa Dar es salaam kutayarisha mambo ya Uhuru wa Tanganyika.

Lakini Mwingine akasema badala ya kutembea kwa miguu ama kutumia Baiskeli basi Mpande Treni, mwingine Bajaji, mwingine Pikipiki na mwingine Ndege. Hayo yote ni mawazo na hakuna kupingana hapo. Ukiona mawazo ya wengine ni kupinga ujue una udhaifu wa kuvumilia mawazo ya wengine.
 
Kwa hiyo watu wasilime? Kafiche huo upuuzi wako.
 
We umeshajaribu kulima au unabwabwaja tu kwenye simu. Wako vijana wengi tu kilimo kimewatoa nyie wavivu kazi yenu kukosoa mambo msiyoyajua.
 
Eti BLOCK za kilimo jangwani Dodoma!. Wazandiki, mafisadi wa Tanzania katika anga zao. Hizi block zingefunguliwa mikoa ya nyanda za juu kusini ikiwemob Iringa,Jombe, Mbeya na mikoa mingine ya kusini na kaskazin bila kusahau Tarime kwa walima mahindi na ndizi ingeleta maana kubwa sana.


Block farming Dodoma haina tofauti na power tiller za kilimo kwanza wkt wa JKT hukohuko Dodoma kunakofidiwa fedha za umma.



"Njaa hudhalilisha heshima na Uhuru wa nchi. Njaa hutweza utu wa binadamu". Dr. Bashiru Kakuru Ally
 
Nakubaliana na wewe, tumwache waziri afanye bila pressure tuone alikuwa anamaanisha nini...Kila la heri Mh. Bashe, Mungu akutangulie mbele
 
Sasa wakilima kwa trekta hiyo cost per unit itarudishwa na soko lipi? Hawa wengine wanaolima kwa nguvu za ugali products zao in aggregate zitauzwa soko lipi? Hiyo political pressure itahimiliwa vipi?
Bado una akili za kijima? Yaani unadhani mipango ya Bashe anaongelea kulima kama alivyolima babu yako? Kaeni msubiri muone
 
We umeshajaribu kulima au unabwabwaja tu kwenye simu. Wako vijana wengi tu kilimo kimewatoa nyie wavivu kazi yenu kukosoa mambo msiyoyajua.
Una matatizo kwenye ubongo wako. Muone daktari
 
Muacheni afanyekazi. Ila sisi kitalaamu kuna kitu tumekiona kikifanyika tu hicho hakika Bashe atafanikiwa na taifa litafanikiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…