Unapozungumzia "Quality" hapo unazungumzia Soko!!
Unapozungumzia "Quantity" hapo unazungumzia Soko!!
Na unapozungumzia "Consistence" Pia unazungumzia Soko.
Hebu tulijadili kidogo.
Unapozungumzia Ubora wa mazao moja kwa moja unazungumzia kupeleka mazao hayo kwa mteja ama kuyashindanisha na ya mwengine sokoni yakiwa na ubora unaotakiwa. Sidhani unazungumzia ubora kwa ajil ya mazao ya kutumia kwenye familia.
Tukija kwenye suala la wingi nalo ni vile vile. Inawezekana kabisa kuna hisia kwamba Tanzania tunazalisha mazao yasiyo na ubora na machache yasiyotosheleza soko. Kwa ivo unaposema tatizo la Kilimo chetu ni uchache wa mazao tunayozalisha upo sahihi, lakini hapo bado unazungumzia soko.
Na pale unapozungumzia Muendelezo, ni kwamba umeunganisha mambo mawili ya mwanzo, yaani Ubora na wingi na kuyaweka yawe ni kitu cha kudumu. Unapozungumzia uendelevu bado pia unazungumzia Soko. Yaani kitu kinachouzwa leo kiuzwe kesho kikiwa na ubora na wingi ule ule.
Sasa hapo ndiyo ujue hayo matatizo ya kutokuwa na "Quality, Quantity, Consistence" ndiyo mkulima anayosumbuliwa nayo hatimaye mazao yake yanakosa soko.
Lakini kwa Tanzania hizo zinazoitwa "Program" huwa zimejaa nadharia zaidi kuliko uhalisia na wala huwa siyo suluhu kudumu kwa matatizo yetu kwenye Kilimo. Hao waliomo kwenye hiyo BBT ni wakulima maskini waliotolewa vijijini ama ni vijana wapya wa kisiasa wanaopelekwa kutumia hizo fedha kwenye jaribio la kilimo lisilo la kisayansi??
Nimechukua kipande hiki kwa muktadha wa "tujadili kidogo". Kwanza nashukuru kwamba umechanganua vizuri sana dhana ya QQC, kwamba Q+Q=C. Kwa nachojua mimi, unless otherwise, BBT inahusisha makundi yote mawili (waliokuwepo na wapya).
Hebu tujiulize, kwanini tuna tatizo la ubora na wingi, na je matatizo haya yanaweza kutibiwa vipi? Sababu ya msingi niionayo mimi ni kudhani kilimo ni kazi isiyo rasmi na hivyo ufanyikaji wake hauhitaji usimamizi, uangalizi wala utaratibu wowote unaoeleweka. Mfano mzuri wa Kilimo chetu ni kama ujenzi wa mji wa Dar es Salaam. Kwa sehemu kubwa umejengwa bila usimamizi, uangalizi wala utaratibu. Matokeo yake tija ya makazi Dar es Salaam haipo.
Tunafanyaje kutatua tatizo la Dar ( one day iwe kama New York?). Tuna option 3. Ya kwanza kurasimisha ( ila hii definitely haitatua mpangilio mbovu wa Dar). Ya pili kuvunja na kuanza upya kwa kupanga na kunyoosha mitaa na kujenga majengo tunayoyataka( utaratibu huu yumkini unaweza kuitengeneza Dar yenye mitaa kama New York au maeneo mengine duniani). Hii option huenda ni VERY EXPENSIVE maana ina maswali na interventions nyingi zinazotakiwa, kwa mfano, wakati wa utekelezaji wake hao wakazi wa Tandale, manzese, mabibo, Tabata etc etc watakaa wapi???
Option ya 3 ni kuanza na maeneo ya nje ya mji kuyapanga na kuyajenga kwa tunavyotaka kabla ya kutekeleza option ya 2 hapo juu. Kwa mtizamo wangu hiki pia ndicho kilichopo kwenye kilimo chetu. Wakulima waliopo wanaendesha kilimo chao bila uangalizi, bila usimamizi na bila utaratibu kiasi ni vigumu sana ukitaka kuwasaidia wazalishe kwa kiasi cha kufikia Q+Q=C. Wako scattered, kila mmoja ana eneo la ukubwa wake na analima anachotaka yeye. Katika eneo lenye ukubwa wa hekta 100, lina wamiliki 300, wapo wenye hekta 5, wengine 2, wengine 1 na wengine miguu 70 kwa 32, haitoshi ndani yake kuna anaelima mahindi, wengine ufuta, wengine mpunga, wengine kunde, wengine alizeti, wengine mbogamboga, wengine wanafuga mbuzi humo, wengine mabwawa ya samaki na pengine ndani ya eneo hilohilo kuna makaburi, nk nk nk.
Na zaidi, kila mmoja ana aina yake ya umiliki wa ardhi. Katika hali kama hiyo, ni interventions zipi utafanya kiwezaa kuwasaidia wakulima hawa ili waweze kuzalisha kwa msingi wa Q+Q=C? Mfano, Uukiamua uwajengee skimu ya umwagiliaji, walima mpunga watafurahi, vipi walima ufuta? Hiyo skimu utaipitishaje kwa mwenye shamba la ufuta ili imfikie mlima mpunga. Ni ngumu aana.
Kwa mifano hiyo ndipo binafsi naona namna nzuri ya kufanya interventions kwenye kilimo Tanzania ni kukifanya kiwe sekta iliyo rasmi na wanaojihusisha nacho watambulike, waaminiwe na wakopesheke. Kwa lugha nyingine, kuifanya iwe sekta yenye uangalizi, usimamizi na utaratibu kwa kuanzisha maeneo mapya na kuyapanga, kuyawekea miundombinu yote muhimu (ya uzalishaji, usindikaji, usambazaji na uuzaji). Ndiyo msingi wa BBT. Maeneo mapya hapa ima hayajawahi kulimwa kabisa au yametwaliwa kwa njia ya fidia kutoka kwenye kundi la wakulima wetu wa kikale.
Ni rahisi kwa wanunuzi kwenda kununua alizeti au kuweka kiwanda kwenye eneo moja lenye hekta 2000, kuliko kununua alizeti kwenye eneo la hekta 3000 zilizotapakaa katika mikoa 26. Hii ndiyo BBT.
Hata hivyo katika utekelezaji wa mradi huu, naamini una components za kusaidia wakulima walio nje ya mfumo huu ambao wana minimum qualifications za kuitwa wakulima wadogo na wa Kati lakini wanabanwa na changamoto kadha wa kadha zinazowafanya wasifikie (sina hakika kama component hii ipo na kama haipo natamani ijumuishwe). Kuna watu wana mashamba ya hekta 10 Hadi 100 na wanalima bila mifumo mizuri ya kilimo. Ni vema Serikali ikawatambua wakulima hawa na kubaini changamoto zao na kuzitatua kwa kadri ya kila mmoja. Kama mkulima ana shida ya trekta, apewe au akopeshwe kwa masharti nafuu. Kama ana shida na kisima achimbiwe, kama ana shida na godawn ajengewe, nk nk nk. Natamani kuona serikali inaondoa kodi kwenye mitambo ya kuchimba visima ili uchimbaji wa visima isiwe anasa. Natamani Serikali ipeleke umeme mashambani ili utumike kwenye shughuli za kilimo kwa ujumla wake. Natamani Serikali ijenge barabara za mawe kuelekea vijijini ili usafirishaji wa mazao uwe muda wote.
Kwa kufanya hivi baadhi ya hawa wanaolima kimazoea wanaweza kuondoka kwenye maeneo wanayolima kienyeji na kwenda kuingia kwenye BBT block farms (kama inavyotokea kwa baadhi ya wakazi wa Tandale, manzese nk kuuza maeneo yao na kutafuta maeneo yalipangwa Kigamboni nk). Ofkoz, tunatatamani hawa wakulima wanaolima kienyeji wawa "phased out" softly.
Hivi ndivyo tunavyoweza kuondokana na takwimu feki za kila asiye na ajira kujiandika guest MKULIMA ilhali kazi yake ya kila siku ni kubeti kwenye draft. Ni kwa kufanya hivi ndio tunaweza kupunguza umaskini na kutengeneza Taifa lenye tija ulimwenguni.