Waziri Bashe hakutakiwa kuukataa msaada wa mchele kutoka Marekani na kama alikuwa na mashaka yoyote angewatumia TBS

Mimi sijui mkuu.

Hoja yangu ni iko pale pale kwamba msaada ambao haujaombwa basi ni hiyari kuukubali ama kuukataa
Hauna uhakika kama msaada haujaombwa na hizo shule, ni uhakika Wamarekani hawajatulazimisha kuukubali huo mchele.
Hata leo hii mkisema hamuutaki hawatakosa nchi nyingine nyingine za kuupeleka.
 
Shule ambazo mchele ni anasa,
Kama ni hivyo wahisani waongeze nguvu maana shule nyingi Bongo bado hio kitu ni anasa.

Otherwise tuongeze nguvu na mikakati ya kuongeza tija shambani kwetu wenyewe.

Mh. Bashe amehisi kama amekuwa ameshambuliwa kwa mgongo (attacked indirectly) kwa hio amelinda mamlaka yake.
Yote kwa yote Bashe ana kazi ngumu mno kuliko mawaziri wengi sana.
KILIMO NI SIASA.

1. Juzi SUKARI
2. Leo MCHELE
3. Kesho mshangao !!!!!
 
Mwenye IQ kubwa anaelewa
 
Kuomba kupewa msaada au kupewa msaada bila kuomba yote hayaondoi maana halisi ya neno msaada. Ni jukumu la msaidiwa kuangalia ubora wa msaada na hapa kwenye suala la mchele, tungewatumia TBS
 
Hii nchi ina wapi uzi wengi sana.Hivi kwa akili yenu Marekani akitaka kuwawekea dawa kwenye chakula atawawekea kwenye mchele wanaokula dodoma peke yake?

Ana kwenda tangu kwenye mbolea ambayo hata hamjui wala kuiwazia Au system ya uzalishaji wa kitu chochote ambacho 80% ya wa Tz watakula.

Waziri huyu ametumia utoto sana.
 
Umeremba sana,all in all ni upumbavu kuingizwa mchele nchini wakati wetu unaozea mashambani.

Halafu America si wa kuaminiwa hata chembe, kwenye mpango depopulation ya dunia wapo,pia wanaongoza kwa maabara za kutengeneza magonjwa duniani
 
Hauna uhakika kama msaada haujaombwa na hizo shule, ni uhakika Wamarekani hawajatulazimisha kuukubali huo mchele.
Hata leo hii mkisema hamuutaki hawatakosa nchi nyingine nyingine za kuupeleka.
Hata wewe hauna uhakika kwamba msaada huo waliombwa.

Kwa mazingira yanavyoonesha ni kwamba msaada huo haukuombwa ndio maana umekataliwa.
 
TBS haina miundombinu ya kuweza ku-question (kutilia shaka) bidhaa yoyote iliyoidhinishwa Marekani.

Kuleni tu mchele, ili muwe mchele mchele.
Kwa hiyo tukatae bila sababu? Kwa hiyo tukikumbwa na baa la njaa na ukahitajika msaada wa dharula , Marekani ikawa tayari mtagoma au mtakubali? Wengi nayaona mashaka waliyonayo ni juu ya usalama na sio nia na dhamira ya msaada huo
 
Kama ulitaka kufaidika na huo misaada,pole sana
 
Umeremba sana,all in all ni upumbavu kuingizwa mchele nchini wakati wetu unaozea mashambani.

Halafu America si wa kuaminiwa hata chembe, kwenye mpango depopulation ya dunia wapo,pia wanaongoza kwa maabara za kutengeneza magonjwa duniani
Kilicholetwa ni msaada mashuleni huo wa mashambani ni msaada?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…