Waziri Bashe hakutakiwa kuukataa msaada wa mchele kutoka Marekani na kama alikuwa na mashaka yoyote angewatumia TBS

Kwa hiyo tukatae bila sababu? Kwa hiyo tukikumbwa na baa la njaa na ukahitajika msaada wa dharula , Marekani ikawa tayari mtagoma au mtakubali? Wengi nayaona mashaka waliyonayo ni juu ya usalama na sio nia na dhamira ya msaada huo
Subiri tupate njaa ndio tuombe huo misaada,sasa hivi hatuna shida na Michele,na sababu Mh. Bashe alizitoa,kaangalie alichosema maana unakurupuka
 
Hivi lini tutajitambua? kwani msaada lazima uupokee, kwanini wasituletee msaada wa technology ya kilimo cha umwagiliaji kama kweli wanatupenda?
Safi kabisa ndugu yangu,umeuliza vizuri sana
 
Waziri huyu amekosea sana kutoa kauli ya namna hii, inaharibu mahusiano mema ya kidiplomasia ya kimataifa.Alipaswa kuziagiza Mamlaka za nchi zinazohusika na masuala ya Uhakiki na Udhibiti ubora na Usalama wa Chakula ili kuchunguza ubora wa mchele huo. Je, huo mchele umeingia hapa nchini kutoka huko ulikotoka nje ya nchi kupitia njia gani? Je, ulipofika mpakani (border post) katika nchi yetu haukukaguliwa ubora wake?????
Akumbuke kwamba: Tanzania inaihitaji sana Marekani, washirika wake pamoja na Misaada yao, Tawala za Nchi zetu hizi za ki-Afrika kamwe haziwezi kutawala watu wala kuendesha Serikali katika nchi zao bila ya kupata Misaada kutoka kwa Marekani na washirika wake.
 
Nchi ombaomba tulishazoea misaada ya kila aina tangu enzi na milele yote.
 
Hakuna sehemu Bashe aligusia usalama wa huo Michele,acheni uwongo
 
Namuunga mkono Bashe. Kukubali msaada wa mchele kutoka marekani ni matusi na fedheha kwa wakulima wa Tanzania.

Wakulima wapewe hizo fedha wa_supplay mchele kwenye hizo shule
 
Kuomba kupewa msaada au kupewa msaada bila kuomba yote hayaondoi maana halisi ya neno msaada. Ni jukumu la msaidiwa kuangalia ubora wa msaada na hapa kwenye suala la mchele, tungewatumia TBS
Issue wala hata sio Ubora wala TBS.
Issue ni kuwa wameleta kitu ambacho kipo na Kubaki.
Hatuhitaji mchele kutoka nje kwa sasa.
Kama wanahisi mchele wetu hauna virutubisho waje waweke hapahapa.

Kingine ni kuwa Bashe kakataa akiwa anaelewa ni kina nani wapo nyuma ya hiyo NGO.
 
Hakuna sehemu Bashe aligusia usalama wa huo Michele,acheni uwongo
Tatizo lako umejazwa upofu wa kutokusoma katikati ya mstari. Bashe amesema kama ni virutubisho Kwa nini visingeletwa hapa vichanganywe tukiona. Hiyo kauli kwako unamaanisha nini?
 
Umatumwa!? Nchi hii haijafikia hatua hiyo ya kupokea misaada ya chakula, tuna mahitaji mengi zaidi ya mchele wa maabara so waambie mabwana zako hatuhutaji misaada hatarishi. Wapeleke Congo na Somalia kwenye janga la vita na njaa.
 
Bashe apewe hizo shule 300 ahakikishe zinapata mchele na maharage anavyosema vipo tele.
Nani kakwambia hizo shule zinahitaji huo mchele na maharage!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…