Waziri Bashe hakutakiwa kuukataa msaada wa mchele kutoka Marekani na kama alikuwa na mashaka yoyote angewatumia TBS

Akina KARLO MWILAPWA ndio wanufaika na hii misaada
 
Umatumwa!? Nchi hii haijafikia hatua hiyo ya kupokea misaada ya chakula, tuna mahitaji mengi zaidi ya mchele wa maabara so waambie mabwana zako hatuhutaji misaada hatarishi. Wapeleke Congo na Somalia kwenye janga la vita na njaa.
Ila hapohapo mkiambiwa wazazi mchangie 20000 Kila mwezi Kwa ajili ya lishe mashuleni mnalalamika ,mmepewa msaada wa kusaidia lishe mashuleni napo mnalalamika. Sijui watanzania tupoje
 
Kwa hiyo unajiona una akili kuliko Bashe? Kumiliki Tecno na kuwa na bando basi na wewe umekuwa advisor wa waziri wa kilimo
 
Hauna uhakika kama msaada haujaombwa na hizo shule, ni uhakika Wamarekani hawajatulazimisha kuukubali huo mchele.
Hata leo hii mkisema hamuutaki hawatakosa nchi nyingine nyingine za kuupeleka.
Huo mchele umeshapigwa vita nchi kibao, ni wa maabara na si rafiki kwa afya ya mtumiaji. Huko kwao wenyewe wanaupiga vita ila waswahili wenzangu wa kingugi wanautetea! Tuna chakula fresh from shamba, hebu tuache kujitia ufukara uliopitiliza kwa kupokea hata misaada tusiyohitaji. Kama kweli hao wamarekani wana huruma na sisi basi watoe hizo hela mchele ununuliwe hapa nchini na kusambazwa mashuleni. Zingatia kuwa huo mchele umeongezwa "virutubisho"
 
Tatizo lako umejazwa upofu wa kutokusoma katikati ya mstari. Bashe amesema kama ni virutubisho Kwa nini visingeletwa hapa vichanganywe tukiona. Hiyo kauli kwako unamaanisha nini?
Kwa hiyo unaogopa kwamba Marekani hapaswi kuhojiwa hata Akita kuleta sumu Kwa wa watanzania? Ukweli ni kwamba Bashe amekukatizia ulaji Mzee,pole.
 
Yeye ni waziri hivyo tunaamini hajakurupuka giving him a benefit of doubt is equally your responsibility. Inapotokea serikali ikatoa kauli kwa umma namna hio there might be a clear signal of something wrong with chabure
 
Kwa hiyo unajiona una akili kuliko Bashe? Kumiliki Tecno na kuwa na bando basi na wewe umekuwa advisor wa waziri wa kilimo
Kama Kuna sehemu mtu anateleza anaambiwa , watu tumetofautiana kuona mambo Kwa mbali. Mimi nimeona kauli za Bashe zinaweza kuharibu hali ya uhusiano kama zisipodhibitwa. Anachoona Bashe ni kwamba anaijibu NGO Kwa sababu ndio iliyoleta msaada huo lakini nyuma ya pazia iliyojibiwa ni Serikali ya Marekani
 
Huo mchele wa Tanzania ungetolewa kama msaada au ungenunuliwa ? Unajua ugumu wa wazazi kuchangia lishe mashuleni ulivyo? Tuacheni siasa, ni jambo la heri tuwapongeze wamarekani
Kwani huo mchele uliotoka Marekani haujanunuliwa kutoka kwa wakulima wa Marekani?
Walilima ili waigawie Tanzania.
 
AISEE MLETA MADA UNAKERA. NILITAMANI NIENDELEE KUKUSOMA ILA NIMESHINDWA. MTU ANAKUTIA DOLE UNASEMA LIACHE HAPOHAPO TUKAULIZE KAMA NI HALALI AU LA KUPIGWA DOLE. AISEE
 
Huwa mnaelewa mnachokisikia?

Wapi Bashe kakataa msaada? Bashe mbona kasema wazi kabisa, kuwa huo msaada wa mchele hauhusiani na serikali. Huo ni msaada unaohusu NGO na yeye kawaambia NGO waambieni waliowapa msaada, hatuna shida ya mchele wa maharage Tanzania. Kama wanawasaidia wawape pesa mnunue hapahapa. Kama ni virutunisho waje kuviwekea hapahapa wakati Watanzania tupo tunatazama kinawekwa nini.

Kamsikilize upya.
 
Pesa wanapiga hao na kununua V8.

Beggars can’t be choosers
 
Nyie ndio mnakubali ushoga wao eti kisa mahusiano ya kimataifa.

Kama kitu ni kibovu kipigwe STOP straight.
 
Hakuna sehemu serikali ya Marekani imejibiwa,hata kama ingekuwa serikali ya Marekani ingejibiwa Moja Kwa Moja Bado waziri yupo sahihi kwenye nchi iliyo huru kukubali,au kukataa misaada. Alafu mbona unalazimisha tukubali misaada wa Marekani bro,vipi????
 
AISEE MLETA MADA UNAKERA. NILITAMANI NIENDELEE KUKUSOMA ILA NIMESHINDWA. MTU ANAKUTIA DOLE UNASEMA LIACHE HAPOHAPO TUKAULIZE KAMA NI HALALI AU LA KUPIGWA DOLE. AISEE
Kupewa msaada hakukupunguzii heshima uliyonayo ila inakuongezea ushujaa. Kiongozi bora anatakiwa kuangalia mambo Kwa angle zote . Kesho ufaulu ukiongezeka mashuleni , tutafurahi na kama tutafurahi maana msaada ni mzuri umesaidia ufaulu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…