Waziri Bashe hakutakiwa kuukataa msaada wa mchele kutoka Marekani na kama alikuwa na mashaka yoyote angewatumia TBS

Huyu jamaa ameumia sana baada ya Bashe kukataa huo mchele
 
Ukipokea msaada wakati kuna wakulima wetu wanahustle kuzalisha ili wauze, unawatia umasikini zaidi.

Hebu wapeleke msosi palestina, sisi hatuna uhaba wa mchele.
Mbona bei za vyakula ziko juu kama wakulima wetu wana hustle kuuza?
Acheni kumezeshwa tu propaganda uchwara.
 
Kupewa msaada hakukupunguzii heshima uliyonayo ila inakuongezea ushujaa. Kiongozi bora anatakiwa kuangalia mambo Kwa angle zote . Kesho ufaulu ukiongezeka mashuleni , tutafurahi na kama tutafurahi maana msaada ni mzuri umesaidia ufaulu
Nan kwambia ufaulu unaongezeka Kwa kula mchele wa Marekani?
 
Waziri bashe ni mchanga sana kidiplomasia na hajui namna dunia inavyoendeshwa. Huwa anajifanya mjuaji lakini kichwani ni mweupe kama theluji.

Hivi wazungu wana shida gani ya kuwaua waafrika kupitia kwenye chakula wakati tayari tumeishajiua wenyewe? Bashe anapswa kufahamu kuwa chanjo zote zinazotumika hapa nchini zimetoka Marekani. Kama wamarekani wangekuwa na nia ya kutuua sisi waafrika (maiti) wangekwisha fanya hivyo kitambo kupitia chanjo na misaada mingine waliyowahi kutuletea.

Huyu msomali amelewa madaraka. Ni wakati muafaka sasa Rais Samia amteue mtanzania kuongoza wizara ya kilimo. Msomali kafeli big time.
 
Umesikiliza hoja ya Bashe? Kachujue wewe uwape wanao wawashwe kinyeo kwanza ndio akili itakukaa vizuri
 
Mbona bei za vyakula ziko juu kama wakulima wetu wana hustle kuuza?
Acheni kumezeshwa tu propaganda uchwara.
Kwa hiyo misaada wa mchele utashusha bei? Na sio kuwezesha wakulima Kwa dhana,na ujuzi wa kisasa Ili uzalishaji uongezeke bei ipungue,!?
 
Je, ukipewa kitu ambacho hujakiomba lakini ulikuwa unakihitaji sana utakubali au utakataa? Ile NGO ni mjumbe na muhusika mwenyewe ni Serikali ya Marekani na mashaka yoyote ya Waziri sio Kwa hiyo NGO bali ni Kwa Marekani ndio maana amewaambia wakawaambie
 
Hivi lini tutajitambua? kwani msaada lazima uupokee, kwanini wasituletee msaada wa technology ya kilimo cha umwagiliaji kama kweli wanatupenda?
Watoto shuleni wenye njaa wanaotaka chakula leo shuleni kuwanza kuwaambia story za teknolojia za umwagiliaji watakuona umechanganyikiwa tu. Waachwe waendelee kula mchele huku nyie mkiendelea kufuatilia hizo teknolojia za umwagiliaji.

Halafu mmeshaomba na kutafuta wataalamu hizo teknolojia za umwagiliaji au mmejikalisha hapo tu kama Mamwinyi mkisubiria mletewe hizo teknolojia??
 
Nan alikwambaia tuna shida na Michele?
 
Umesikiliza hoja ya Bashe? Kachujue wewe uwape wanao wawashwe kinyeo kwanza ndio akili itakukaa vizuri
Hoja zangu zipo clear, tuna TBS ambayo inachunguza ubora mashaka yoyote aliyonayo Bashe angewatumia TBS na tungekuwa na sababu madhubuti ya kukataa lakini kilichofanywa na Bashe ni kama kutoa tuhuma bila ushahidi
 
nchi yetu inaweza kukumbwa na baa la njaa na tukahitaji msaada wa Chakula kutoka nje. Je, tutapata wapi nguvu za kuomba msaada kutoka Marekani kama tumeamua kukataa msaada Sasa ?

Mnapenda kujidhalilisha sana na umasikini wenu
Kwa hiyo sisi tuwe wa kuomba tu wakati tuna Mito na Maziwa kila sehemu
Muwe na aibu basi
 
Nenda shule za umma zilizo jirani yako hapo angalia chakula chao, utakuta wanashindia suti tu. Uji mweupe wa sukari na Ugali Maharage yanayolea kwenye bakuli. Hayo mambo ya kwamba chakula kipo na kubaki ni porojo tu.
 
TBS hii hii inayoruhusu malonyalonya ya mchina kuingia Tanzania ndiyo ingepima mchele kutoka USA?.
Wewe ni mtumwa anayevaa suti.
 
Wakulima wapewe hizo fedha wa_supplay mchele kwenye hizo shule
Wakulima wa Tz wapewe fedha!??? Kamwe sikubaliani na haya maoni yako, Waafrika (watu weusi) hawaaminiki kabisa katika masuala ya kuwapa Msaada wa fedha, hawazitumia vizuri kwa namna inayotakiwa na mwishowe hakutakuwa na TIJA yoyote ile. Kwa maoni yangu, Wakulima wa Tz wanapaswa kupewa Msaada wa Elimu na Mafunzo juu ya namna ya kulima kilimo bora na kuzalisha mazao yenye virutubisho bora kama huo mchele ulioletwa kwa msaada, lakini siyo kuwapa msaada wa fedha.
 
Tatizo lako umejazwa upofu wa kutokusoma katikati ya mstari. Bashe amesema kama ni virutubisho Kwa nini visingeletwa hapa vichanganywe tukiona. Hiyo kauli kwako unamaanisha nini?
Bashe atasababisha watoto wakatae kula chakula shuleni, yale yale ya anti-vaxxers tu kupinga watoto wao wasipewe chanjo.
Kauli ya Bashe ni mbaya sana, inapaswa kulaaniwa na watu wote wenye akili.
 
Kwani huo misaada ni wa serikali ya Marekani,au NGO kutoka Marekani? Acheni kubabaisha watu bhana,na hata kama tutapata Janga,sio Marekani tu itatusaidia,nyinyi kama mlikuwa na lengo la upigaji mmeliwa mtulie tu🤣🤣🤣
 
Bwana msituchoshe, walete virutubisho wanunue mchele wa ndani ,
 
Mabadiliko yoyote sio suala la "overnight" ila ni mchakato mrefu ,kama tukikumbwa na baa la.njaa hata kama mito ipo Bado tutahitaji msaada na tutapewa bila kuomba
 
Bashe atasababisha watoto wakatae kula chakula shuleni, yale yale ya anti-vaxxers tu kupinga watoto wao wasipewe chanjo.
Kauli ya Bashe ni mbaya sana, inapaswa kulaaniwa na watu wote wenye akili.
Bashe is right!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…