Waziri Bashe hakutakiwa kuukataa msaada wa mchele kutoka Marekani na kama alikuwa na mashaka yoyote angewatumia TBS

Kuhusu Msaaada Wa USAID Wa Chakula Lishe.

📌Ni kweli kuna ukosefu mkubwa wa chakula lishe chenye virutubisho kwa wanafunzi wengi maana vyakula vingi wanavyokula ni kuzuia njaa tu na sio kuleta afya ya mwili na akili hivyo udumavu unaongezeka.

📌USAID kwa mahaba makubwa kama ambavyo wanawajengea vyoo vya kujisaidia wameamua kuwaletea msaada wa vyakula vyenye virutubisho vizuri zaidi maana wahusika si mmejisahau ngoja wao wawakumbushe vizuri

📌Sisi tuko bize sana na mambo ya umbeya na umepigwa mwingi ila kuwa makini sana kuhusu afya za watoto wetu kwa mwili na akili wengi bado wako nyuma sana ila inapotokea mambo kama haya ndo tunaanza kupaza sauti ya kushituka eti huenda wana nia mbaya .

📌Nendeni mashuleni huko muone kuanzia asubuhi mpaka saa tisa watoto wenu wanakula vyakula vya aina gani je vina ongeza tija katika afya ya mwili na akil ? kisha muanze Kulalamika.

📌Huwa nasema wazazi na walezi wengi ni wabinafsi sana kwa watoto wao licha ya kujifanya wanapenda watoto wao mfano wakisikia semina za mizagamuo hata 50k Wanaenda ila semina zinazohusu watoto wao hata bure hawaendi huo ni UNAFIKI

Kitabu changu cha MZAZI ACHA UZEMBE; MAMBO 10 YA MSINGI KUZINGATIA KUHUSU ELIMU YA MTOTO WAKO.kingekuwa kinaongelea kuifinyia kwa ndani au kusimamia muda mrefu ungeona sharing zake kuwa nyingi na maswali kibao ila kwa vile ni kuhusu elimu ya watoto wao huwaoni sababu ya UNAFIKI wa kujifanya wanawapenda watoto wao kumbe hawawapendi kiuhalisia .

NB ; Msiache Kuweka Oda Kwa Namba 0718821168.
Ndugu yenu Magoda Jr 📌
Ujamaa Ni Imani

Haya Maoni ni mazuri sana
 
Ni vizuri msaada ukatolewa kipindi cha uhitaji. Je, tuna upungufu wa chakula mpaka tuletewe msaada wa chakula? Au wamarekani wanatafuta soko la chakula chao kilazima na kuua soko la wazalishaji wa ndani?
 
Nani kakwambia hizo shule zinahitaji huo mchele na maharage!?
Sijaambiwa, nimesoma shule ambayo siku mchele au nyama vikipikwa inakuwa shangwe kama sikukuu na ukizembea unaweza kushinda njaa siku hiyo jinsi watu wanavyogombania ubwabwa au nyama.
 
Serikali ya Marekani inawasaidia wakulima wake kupata soko. Nawe unafaidika kwa kupata msaada. A win-win situation. Hawawezi kukuletea fedha.
 
Huelewei maana ya kuongezwa virutubisho, hata hapa Tanzania kuna vyakula vingi viko fortified, hata mafuta ya kula yanaoingizwa kutoka nje lazima yaongozewe virutubisho, chumvi inayochimbwa nchini lazima iongozwe virutubisho kabla ya kuuzwa.
 
Huna akili

Msaada umetolewa na wakulima wa Marekani means sehemu ya mavuno yao ndio yameletwa huku, sasa wewe unataka wauze huko halafu walete hela wanunue mchele wa huku nani atakubali upuuzi huo, yaani mfano mnataka kupewa msaada na kampuni ya magari halafu tuwaambie hatutaki magari yenu uzeni huko halafu mlete hela tukanunue magari mengine.
 
Lengo la msaada likiwa zuri hakuna sababu ya kukataa msaada, dunia nzima wanaishi hivyo
Hivi mtu mweupe ana lengo zuri na nyani kweli,hivi hujasoma history Kama vipi nenda kwao kaishi nao ndio utaona Kama wanakupenda.
Unajua wale wale black Americans wanachowafanya lakini
 
Bashe kafanya the right thing,I support him 100%.It seems sio agent wa the CIA.TBS sio trustworthy kabisa,ni already captured by the American government.Keep it up Bashe,unawafaa Watanzania.
 
Tanzania Ina shule zaidi ya 300, nani anazilisha hizo zingine nje ya hizo 300?
Kama Kuna shule 10 na kati ya hizo shule Moja ina uhitaji mkubwa sana wa walimu na vifaa vya kufundishia kuliko zingine, ukitaka kupeleka walimu utaanza na zipi?
 
Kama Kuna shule 10 na kati ya hizo shule Moja ina uhitaji mkubwa sana wa walimu na vifaa vya kufundishia kuliko zingine, ukitaka kupeleka walimu utaanza na zipi?
Hakuna popote Tanzania imewahi kutangaza crisis ya chakula kwa shule zake. Tulifikaje hapa?
 
Kwa hiyo NGO imekuwa wakulima wa Marekani? Ng'ombe ww!
 
Kwa hiyo misaada wa mchele utashusha bei? Na sio kuwezesha wakulima Kwa dhana,na ujuzi wa kisasa Ili uzalishaji uongezeke bei ipungue,!?
Hapa suala kwa sasa kwanza ni watoto mashuleni wasishinde njaa au kuona ubwabwa ni anasa, pia kutegemea na ukubwa wa msaada bei inaweza kushuka.
Pia Marekani na mataifa mengine ya Magharibi yanasaidia sana bajeti ya nchi yetu, wanatoa misaada na scholarships.
Tatizo pesa zetu za bajeti zinaenda kununulia maV8 na pia hao wataalamu wanaosomeshwa wakija hawapewi mazingira mazuri na wezeshi ya kufanya kazi husika za kilimo.
 
Tanzania Ina shule zaidi ya 300, nani anazilisha hizo zingine nje ya hizo 300?
Unataka Wamarekani wakulishie shule zako zote juu ya kukujengea matundu ya vyoo pia??
 
Kwani Dodoma ndio watoto wanashinda njaa tu?
 
Hivi mtu mweupe ana lengo zuri na nyani kweli,hivi hujasoma history Kama vipi nenda kwao kaishi nao ndio utaona Kama wanakupenda.
Unajua wale wale black Americans wanachowafanya lakini
Waziri wa Ulinzi wa Marekani ni Black
Mkuu wa majeshi wa Marekani ni Black
Balozi wa Marekani nchini ni Black.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…