Waziri Bashe punguza kelele za mitandaoni, bei ya mchele kilo moja imefika Shilingi 3,000

Waziri Bashe punguza kelele za mitandaoni, bei ya mchele kilo moja imefika Shilingi 3,000

nashicha

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2021
Posts
279
Reaction score
524
Hawa mawaziri wetu wamekuwa kama yule mpuliza filimbi wa Hamelin I kelele nyingi sana; wanashindana na MITANDAO leo nimeona kwenye tangazo moja mchele supaa kabisa kilo 1500 kutoka mikoani , akini kwa madukani na rejareja hapa Dsm Mchele unaofaa kula Sasa hivi ni 2800 na 3000.

Kwaninj tumefikia huko kama vyakula vipo. Je, nini kimesababisha bei kupanda mara mbili tatizo hapa lipo kwa wanasiasa sijui kwasababu wao wananunuliwa vyakula wanavikuta nyumbani gari wanawekewa mafuta kwa kodi zetu huku wakitulimbikizia tozo ili waweze kujigawawia?

Kwanini Mchele na unga vimepanda bei kiasi hiki SIWAONI wakijitokeza na kuwaukiza wauzaji namuomba Mh Bashe aache siasa kwenye maisha ya watu ajitokeze atoe tamko; je Kuna njaa au upungufu wa vyakula?
 
Hilo swali lako lina majibu kitambo sana,Tulitoka kwenye Covid, then ikaja vita ya Russia vs Ukraine hivi viliathiri pakubwa upatikanaji wa mbolea, then ukichukua tatizo la ukame mwaka jana, vinafanya cost za uehdeshaji mashamba kuwa kubwa, impact yake ndio bei za sasa, ila bado naona vyakula bei ipo chini iongezeke tu.
 
Huyo wa Mchele Supa kwa 1500 anataka awapige. Jamaa atawaibia. Kwa sasa hakuna Mchele wa chini ya 2000 sasa mchini kwetu. Hata Morogoro na Mbeya hakuna mchele wa bei hiyo. Vyakula vimepanda bei sana na hali ni ngumu sana.

Hakuna vyakula kwa sasa. Huyo waziri ni wa hivyo anapiga mdomo tu na hapo Wizarani wanamdharau sana. Anaongea sana ili amfurahishe na kumzubaisha Hangaya kwani ni mpigaji. Mbolea za ruzuku na mfumo wao utamuacha uchi muda si mrefu.
 
hilo swali lako lina majibu kitambo sana,Tulitoka kwenye Covid , then ikaja vita ya russia vs ukraine hivi viliathiri pakubwa upatikanaji wa mbolea, then ukichukua tatizo la ukame mwaka jana , vinafanya cost za uehdeshaji mashamba kuwa kubwa, impact yake ndio bei za sasa, ila bado naona vyakula bei ipo chini iongezeke tu
Mwanyaluke wa wapi unaongea pumba hivyo mbona Mwanyaluke wenzako kuanzia akina Jueni hadi Godfrey IQ zao ni kubwa.

Umesema bei ndogo kwa kuwa wewe una purchasing power kubwa ila huku vijijini hali ni mbaya. Kwenu tu Iringa vyakula bei juu na mleta thread anasema Waziri na serikali wafanye jitihada za kuzuia mfumuko wa bei.
 
Mwanyaluke wa wapi unaongea pumba hivyo mbona Mwanyaluke wenzako kuanzia akina Jueni hadi Godfrey IQ zao ni kubwa. Umesema bei ndogo kwa kuwa wewe una purchasing power kubwa ila huku vijijini hali ni mbaya. Kwenu tu Iringa vyakula bei juu na mleta thread anasema Waziri na serikali wafanye jitihada za kuzuia mfumuko wa bei.
Una makasiriko tu, sababu za bei kuwa juu ni hizo, na bado bei za pembejeo zipo juu, ukilipa vibarua, pembejeo, then ukifanya hesabu za muda uliotumia shambani, bado unaona faida ninayopata mkulima ni ndogo, nakupa tu hii" maharage hayapo kabisa sokoni "so tegemea bei mpya soon ya maharage.
 
una makasiriko tu , sababu za bei kuwa juu ni hizo, na bado bei za pembejeo zipo juu, ukilipa vibarua, pembejeo , then ukifanya hesabu za muda uliotumia shambani , bado unaona faida ninayopata mkulima ni ndogo, nakupa tu hii" maharage hayapo kabisa sokoni " so tegemea bei mpya soon ya maharage
Hakuna mkulima aliyeuza mchele zaidi ya tsh 1300 kwa kg waliopandisha bei hizo niwafanya biashara na serikali kuruhusu mchele na vyakula vingine kuuzwa nje ya nchi kabla hatujawa na stock ya kutosha ndani ya nchi, leo hiii huyo mkulima naye ni muathirika wa kununua mchele dukani tsh. 2800 na zaidi sababu chakula kingi alikiuza kwa bei ndogo kipindi cha msimu wa mavuno. Vita y ukrain mnaisingizia tuu bure.
 
Mtakuja kugundu kitu kimoja baada ya kufa, vita ya maendeleo ni ya mtu, serikali itaendelea kukunyonya kila siku!
 
una makasiriko tu , sababu za bei kuwa juu ni hizo, na bado bei za pembejeo zipo juu, ukilipa vibarua, pembejeo , then ukifanya hesabu za muda uliotumia shambani , bado unaona faida ninayopata mkulima ni ndogo, nakupa tu hii" maharage hayapo kabisa sokoni " so tegemea bei mpya soon ya maharage
Nyie ndo ilitakiwa panyaroad wawapunguze
 
hilo swali lako lina majibu kitambo sana,Tulitoka kwenye Covid , then ikaja vita ya russia vs ukraine hivi viliathiri pakubwa upatikanaji wa mbolea, then ukichukua tatizo la ukame mwaka jana , vinafanya cost za uehdeshaji mashamba kuwa kubwa, impact yake ndio bei za sasa, ila bado naona vyakula bei ipo chini iongezeke tu
Kama hujaelewa soma Tena mbona Kuna wafanyabiashara wanauza Mchele 1500 kwa jumla na wanaombea mpaka utufikie kwanini kwenye maduka ya rejareja unauzwa 3000?

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Hakuna mkulima aliyeuza mchele zaidi ya tsh 1300 kwa kg waliopandisha bei hizo niwafanya biashara na serikali kuruhusu mchele na vyakula vingine kuuzwa nje ya nchi kabla hatujawa na stock ya kutosha ndani ya nchi, leo hiii huyo mkulima naye ni muathirika wa kununua mchele dukani tsh. 2800 na zaidi sababu chakula kingi alikiuza kwa bei ndogo kipindi cha msimu wa mavuno. Vita y ukrain mnaisingizia tuu bure.
Acha kudanganya hivi mnafikiria wakulima wa sasa ni sawa na wale w miaka 1980s, wakulma wa sasa kwanza jua wengi wana mitaji na ndio wanafanya kilimo biashara, wanalima, wanatenga chakula chao, the rest wanapeleka kwenye magara ya kuhifazi, na ndio hao sasa wanauza mchele sasa last months nimepeleka viazi Zambia na tulikuwa na wakulima kibao wa mpunga tokea mbarali wapo kuuza, acheni kujidanganya.
 
Hiyo ni kazi ya wazri wa biashara nadhani mh. Ashantu Kiazi.

Waziri wa kilimo kazi yake ni kuongeza uzalishaji wa mazao kwa wakulima tu.

Naona Bashe anataka kuonewa tu
 
Hawa mawaziri wetu wamekuwa kama yule mpuliza filimbi wa Hamelin I kelele nyingi sana; wanashindana na MITANDAO leo nimeona kwenye tangazo moja mchele supaa kabisa kilo 1500 kutoka mikoani , akini kwa madukani na rejareja hapa Dsm Mchele unaofaa kula Sasa hivi ni 2800 na 3000.

Kwaninj tumefikia huko kama vyakula vipo. Je, nini kimesababisha bei kupanda mara mbili tatizo hapa lipo kwa wanasiasa sijui kwasababu wao wananunuliwa vyakula wanavikuta nyumbani gari wanawekewa mafuta kwa kodi zetu huku wakitulimbikizia tozo ili waweze kujigawawia?

Kwanini Mchele na unga vimepanda bei kiasi hiki SIWAONI wakijitokeza na kuwaukiza wauzaji namuomba Mh Bashe aache siasa kwenye maisha ya watu ajitokeze atoe tamko; je Kuna njaa au upungufu wa vyakula?

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Kuna shida kubwa sana katika uzalishaji na mbeleni tusipochukua hatua sasa itafika sh. 5,000, mfumo wa elimu umekimbiza ile 1st cream kwa uzalishaji vijijini wamekuja mjini huku hakuna wanachofanya zaidi ya white color job na ushubwada. Matokeo yake waliobaki huko shamba wameshindwa kupambana na mabadiliko ya tabia nchi na kukua kwa soko na wanaamini ipo serikali siku moja itawakomboa (very wrong).

Sasa wadau wote JF mtafute mashamba tukalime nyie ndio wenye nguvu na maarifa, babu zenu kule wameshachoka inatakiwa akili nyingi shambani sasa kuliko wakati wowote ule. Manake zamani wenzenu walijua nguvu ndio inatakiwa lakini ukweli ni akili nyingi na maarifa ya uzalishaji mali ndio tunatakiwa kuwa nayo. Kuanzia best practices katika kupata arable land, mbegu bora, kilimo bora na post harvest handling pamoja na masoko.

Bashe ni mwanasiasa na yeye anachosema na anachofanya priority ni kushinda uchaguzi unaokuja, sie wagonga nyundo tunaendelea kulalama wakati tuna ardhi na sehemu kubwa ya ardhi yetu haitumiki katika uzalishaji. twendeni kwetu Tabora, Nsenda, Nkorongo, Izimbili na Usinge huko tukaanzie na jembe la mkono hii shida ya mchele tunamaliza. ndio mitaji mikubwa tutapata huko, tukivuna zaidi ndio akili ya harvesting na post harvesting handling itakuwa kama mbele. Kule bush kuna shida kubwa ya storage maghala yote ni Tumbaku na vyama vya ushirika hakuna vihenge vya kuhifazia chakula cha ziada matokeo yake tumeuza gunia la mpunga 36, 000 julai mwaka jana na tumenunua gunia hilo hilo sh. 100,000 januari 2022.

Ukiangalia msafara wa malkia barabarani utagundua jamaa hawana idle land, huko vijijini kwetu wako watu wachache wenye akili nyingi na maarifa na wanasubiri dude linaloitwa serikali kuja kuwatoa lakini ngoma inazidi miaka 60 sasa na ahadi ni zile zile.
Tuliwaambia humu kipindi cha corona msinunue midege tuwekeni nguvu katika kilimo tutatusua lakini walichotujibu acheni tukaushe tu.
 
Hawa mawaziri wetu wamekuwa kama yule mpuliza filimbi wa Hamelin I kelele nyingi sana; wanashindana na MITANDAO leo nimeona kwenye tangazo moja mchele supaa kabisa kilo 1500 kutoka mikoani , akini kwa madukani na rejareja hapa Dsm Mchele unaofaa kula Sasa hivi ni 2800 na 3000.

Kwaninj tumefikia huko kama vyakula vipo. Je, nini kimesababisha bei kupanda mara mbili tatizo hapa lipo kwa wanasiasa sijui kwasababu wao wananunuliwa vyakula wanavikuta nyumbani gari wanawekewa mafuta kwa kodi zetu huku wakitulimbikizia tozo ili waweze kujigawawia?

Kwanini Mchele na unga vimepanda bei kiasi hiki SIWAONI wakijitokeza na kuwaukiza wauzaji namuomba Mh Bashe aache siasa kwenye maisha ya watu ajitokeze atoe tamko; je Kuna njaa au upungufu wa vyakula?

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Bashe yeye anajua kiingereza tu cha Nzega cha It is Very Danger, lakini matokeo hakuna Wizarani kwenyewe watumishi karibu wote hawamtaki kwa sababu amekuja kuwaharibia wizara leo nchi inakumbwa na njaa chini ya utawala wake wakati wenzake kina Hasunga na Mkenda waliiacha wizara ikiwa safi. Yeye amekuja na mambo yake ya biashara zake ya Mbolea ili ruzuku wapewe watu wake wa karibu.
 
Hawa mawaziri wetu wamekuwa kama yule mpuliza filimbi wa Hamelin I kelele nyingi sana; wanashindana na MITANDAO leo nimeona kwenye tangazo moja mchele supaa kabisa kilo 1500 kutoka mikoani , akini kwa madukani na rejareja hapa Dsm Mchele unaofaa kula Sasa hivi ni 2800 na 3000.

Kwaninj tumefikia huko kama vyakula vipo. Je, nini kimesababisha bei kupanda mara mbili tatizo hapa lipo kwa wanasiasa sijui kwasababu wao wananunuliwa vyakula wanavikuta nyumbani gari wanawekewa mafuta kwa kodi zetu huku wakitulimbikizia tozo ili waweze kujigawawia?

Kwanini Mchele na unga vimepanda bei kiasi hiki SIWAONI wakijitokeza na kuwaukiza wauzaji namuomba Mh Bashe aache siasa kwenye maisha ya watu ajitokeze atoe tamko; je Kuna njaa au upungufu wa vyakula?

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Wapumbavu wanaishi Dar es Salaam na mijini wanataka wanunue unga kilo Tsh 1,000 na Michele Tsh 2,000 milele. Hawajui mkulima anavyohangaika na kununua mbolea kwa bei juu kufyeka pori, kulima na kupalilia . Hawajui bei ya pembejeo eti leo wanalalamika mahindi na Michele vinakwenda nje ya mipaka ya Tanzania.

Huu ndiyo wakati wa mkulima wa Tanzania kupata bei nzuri, hakuna kufunga mipaka. Chakula kikiisha na sisi Tanzania tutanunua nje ya Tanzania. Vile vile kama tutauza nje basi soko litakua hivyo basi watu wengi watajishirikisha na kilimo
 
Ukosefu wa sera nzuri za kilimo ndio matokeo yake haya

Nchi hii pamoja na changamoto za ukame vita na covid 19 bado haikua sababu kubwa ya vyakula kupanda kiasi hiki

Tuna vyanzo ving vya maji serikal ingesamabaza miundo mbinu ya kilimo chaumwagiliaji kila sehemu yenye chanzo Cha maji nadhan. Tingekuewa mbali

Swala la mbolea hali ilishaonekana dalili za kuwa na vita Ukraine kwann wasingejiandaa kuagiza mzgo mkubwa ili kukabiliana na hili?

Tuna kiwanda Cha mbolea Cha minjingu kwann kisianze kuzalisha mbolea nyingne Zaid Kama CAN SA UREA DAP NPK n wakat sasa wakutafuta wabia wa maendeleo waanzishe kiwanda au viwanda

Kuna jamaa n waisrael alitaka kifungua kiwanda Cha mbolea mikoa ya kusin lakn urasimu aliokutana nao nchi hii ikabid aende rwanda na sasa ameanza ujenz wa kiwanda hicho

Wanasiasa wanatumia ujinga wetu na jeshi la polisi kutusababishia umasikin huku wao wakineemeka

Wakati n sasa tuamke

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom