Waziri Bashe punguza kelele za mitandaoni, bei ya mchele kilo moja imefika Shilingi 3,000

Angalia mpaka sasa suluhisho l a maagrovet wenye liseni za kuuza mbolea bado suluhisho wauzaji wamebaki waagizaji tu.
 
Akili za kijinga kabisa, badala ya kuipigia kelele serikali kushindwa kuzuia upandaji holela wa pembejeo au kutoa ruzuku kwenye pembejeo unashangilia upandaji wa bei... wakati mama yako mzazi anashindwa kununua unga na nafaka nyingine. Thamani ya fedha inaporomoka kila uchao...unadhani wakiuza bei kubwa ndio wanakuwa matajiri wakati nao wanakuja kuzitumia kwa kununua vitu kwa bei kubwa???!!!.... acha ushabiki maandazi.
 
Nenda na wewe kalima ,wewe unalalmika bei ya mchele,mbona hukulalamika bei ya pembejeo zilivyopanda, au unadhani kulima mpunga ni sawa na kwenda kununua mchele sokoni. Wanasiasa hawafanyi wala kuuza mchele, bei inapanda kutokana na mambo mengi pia likiwemo la usafiri, gaharamma za usafiri zipo juu kutokana na kupanda kwa bei za mafuta, tukisema rudini vijijini mkashike jembe kama maisha ya mjini yamewashinda hamtaki mumebaki kumshangilia Mayele pamoja na kushadidia malumbano ya akina Haji,Mwijaku na akina Karia
 
Na inavyosemekana, bei itaendelea kuongezeka
Safi sana.Wakulima tutafaidi jasho letu
Na iendelee kupanda tu

Jua letu ,mvua yetu walaji wako kwenye viyoyozi vya hewa baridiiiii wanakula upepo wa feni na AC halafu wanataka kutukandamiza bei Sisi washinda juanita na kwenye mvua tukilima.

Asante Mungu kwa bei kupanda wakulima tunakushukuru
 
Wewe una akili za kipumbavu. Mama yangu ni mkulima, analima, anatunza mahitaji yake na kuuza ziada.

Nyie wenye mama wapumbavu ndiyo muikemee Serikali kwa vile hamlimi, mko tu mijini mnataka mlimiwe na wenzenu.
 
We unafikiri wale waombolezaji Kwenye msiba wa bibi . Wangekula nn. Mchele mwingi umepelekwa huko[emoji58][emoji58][emoji58]
 
Shida inakuja pale mkulima wa mahindi anafurahia kuuza kwa bei ya juu. Ila, akipata pesa na kwenda kununua mchele kwa mwingine, anashangaa.
 
Kama hujaelewa soma Tena mbona Kuna wafanyabiashara wanauza Mchele 1500 kwa jumla na wanaombea mpaka utufikie kwanini kwenye maduka ya rejareja unauzwa 3000?

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Wapi huko unapatikana kwa 1500, nije kununua. Am serious plz nipe taarifa nichangamkie fursa
 
Wewe una akili za kipumbavu. Mama yangu ni mkulima, analima, anatunza mahitaji yake na kuuza ziada.

Nyie wenye mama wapumbavu ndiyo muikemee Serikali kwa vile hamlimi, mko tu mijini mnataka mlimiwe na wenzenu.
Ukiitwa mjinga usilalamike tena unishukuru, ebu jisome ulichoandika hutashangaa ukiitwa jinga namba one. Unategemea kulishwa na mama yako mkulima wa jembe la mkono? Pathetic ..... kupanda kwa chakula hakuna uhusiano wowote na kutajirika kwa mkulima aina ya mama yako.... na siongelei nafaka pekee naongelea kupanda kwa gharama zote. Ila mjinga kama wewe hutanielewa.
 
Bashe ndio anauza hayo mazao we bwege? Unamlalamikia nani. Jilimie chakula chako mwenyewe. Kuna mtu anakupangia matumizi ya mapato yako? Hizi akili za kipumbavu mziachage
 
Jibu lake ni yale ma misururu ya Malori yaliyokwama Kule #Namanga boarder yakiwa yamesheheni maelfu ya tani za Mahindi kuelekea nchi jirani ya Kenya.

Tatizo tuna serikali ambayo iko auto Pilot.
 
Jibu lake ni yale ma misururu ya Malori yaliyokwama Kule #Namanga boarder yakiwa yamesheheni maelfu ya tani za Mahindi kuelekea nchi jirani ya Kenya.

Tatizo tuna serikali ambayo iko auto Pilot.
Autopilot inatokea wapi? Toka mumeanza kulalamika mipaka ifungwe ni kama miezi 5. Je umelima matuta mangapi ya mahindi wewe binafsi?

Nyie mumekaa mijini kwenye viyoyozi mnataka muendelee kununua mahindi kilo Moja kwa Tsh 500/-. Je ni lini mkulima wa mahindi ataboresja maisha yake?

Mimi natoka Nyanda za Juu Kusini na mimeshuhudia gunia la mahindi likiuzwa mpaka Tsh 95,000.

Mwaka 2016-20 ya ukiritimba wa DIKTETA Magufuli gunia likiteremka kutoka Tsh 60,000 hadi Tsh 24,000 na wakulima wengi walifirisika.

Wanaotaka mipaka ifungwe kuzuia mahindi wanionyeshe leo ñi Mtanzania gani amekufa kwa bei ya mahindi kupanda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…