Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa amefunga mashindano ya mpira wa miguu ya KNK CUP 2024 yaliyotanguliwa na Bonanza la michezo mbalimbali ambapo amempongeza Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt.Dotto Biteko Kwa kuendelea kuunga mkono kwa kasi jitihada za Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye sekta ya michezo nchini.
Waziri Bashungwa amesema Jitihada za Dkt.Biteko ambaye ni mbunge wa Jimbo la Bukombe zitasidia kukuza vipaji vingi Nchini hasa katika Wilaya ya Bukombe kwa kuwaweka pamoja vijana, kuimarisha afya na kuibua vipaji vyao.
Akizungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye fainali hizo zilizofanyika katika uwanja wa Kilimahewa wilaya ya Ushirombo mkoani Geita tarehe 17 Septemba 2024 ameahidi kutoa kiasi Cha shilingi Milioni 15 kwa ajili ya ukarabati wa uwanja huo.
“Nikupongeze kwa hatua hii ya kuendesha ligi Bora ndani ya WILAYA ya bukombe, hongera umeleta viongozi wakubwa wa michezo ambao wao wataweza kuchagua wachezaji wenye vipaji zaidi na kuwapeleka ligi kubwa za kitaifa” Amekaririwa Waziri Bashungwa
Kuhusu suala la miundombinu ya barabara, Bashungwa amemuhakikishia Naibu Waziri Mkuu huyo kuwa Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala ya Barabara (TANROADS), tayari imeanza manunuzi ya kumpata Mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Ushirombo – Katoro (km 59) kwa kiwango cha lami na kusisitiza hadi kufika mwishoni mwa mwezi Disemba 2024 kazi za ujenzi zitakuwa zimeanza.
Soma;
==> Ligi ya Bashungwa Karagwe CUP 2024 yahitimishwa kwa kishindo, Rais Samia apewa tano