Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi za ujenzi wa vyumba vya madarasa, mabweni na mindombinu mingine ya shule ili kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa kutoa fursa ya idadi kubwa ya wanafunzi kujiunga na elimu ya sekondari na kidato cha tano na sita pamoja na Kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani.
Bashungwa ameeleza hayo Oktoba 08, 2024, mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mabweni manne, madarasa mawili na vyoo matundu sita katika Shule ya Sekondari Viziwaziwa iliyopo katika Kata ya Viziwaziwa Halmashauri ya Mji Kibaha Mkoani Pwani.
Waziri Bashungwa ameridhishwa na hatua za utekelezaji wa miundombinu hiyo ambayo inagharimu kiasi cha Shilingi Milioni 534 na kueleza kuwa kukamilika kwa Mabweni katika Shule hiyo kutapunguza changamoto za wanafunzi kusafiri mwendo mrefu kila siku kufika shuleni.
Akitoa taarifa ya mradi, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Viziwaziwa, Abasi Kiwayo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiboresha Shule hiyo kwa kuipanua zaidi na kuwa na hadhi ya Kidato cha Tano na Kidato cha Sita.
Abasi Kiwayo ameeleza kuwa hadi sasa jumla ya Shilingi Milioni 177.363 zimetumika katika utekelezaji wa mradi huo tangu ulipoanza kutekelezwa mwezi Agosti, 2024.