Waziri Bashungwa atoa siku 7 mabasi yote ya mikoani yawe yanaingia Magufuli Bus Terminal, si Shekilango

Stendi ya Magufuli ni Ndogo mbona viongoz wa kisiasa hawa wagumu kuelewa!? hivi abood, alsaedy, shabiby wakaleta gari zao kwa wakati mmoja si wanajaza stendi yote! tuwe na busara
Amesema kushusha na kupakia. Sio kupaki na kulaza.
 
Kuna Daraja la Kuvukia Juu labda kama halijaanza kutumika..
 
Waziri wa Tamisemi mh Bashungwa ametoa siku 7 mabasi yote yanayotoka mikoani yawe yanaingia Magufuli bus terminal

Lengo ni kuiongezea serikali mapato amesisitiza

Source ITV habari
 
Waziri wa Tamisemi mh Bashungwa ametoa siku 7 mabasi yote yanayotoka mikoani yawe yanaingia Magufuli bus terminal

Lengo ni kuiongezea serikali mapato amesisitiza

Source ITV habari

Hapo ambapo hakuna choo?
 
Mkuu, Kuna magari hayaingii kabisa pale. Mfano, tahmeed, Kilimanjaro, bm, etc. Kifupi gari nyingi za kwenda kaskazini zinazopaki shekilango hazipiti mbezi(asubuhi) na haziingii(kwa zinazotoka mkoani).
Stand zinakwenda kujengwa nje ya mji unategemea nini, gharama ya mtu kutoka mbagala,chanika,kigamboni or ukongaetc mpaka kufika stand ya mbezi gharama yake asubuhi inaweza shinda nauli ya mkoanii, hivyo kampuni nyingi zimeona zifuate wananchi walipo which is very fair, na mara nyingi unakuta basi likifika stand ya magufuli limeshajaa, hapo wanapandia watu wa maeneo ya huko tu.so mi naafiki hoja ya waziri ya kupita pale ila iwe kwa wanaopandia hapo sawa ila wakishashusha abiria wa hapo waendelee kuwapeleka abiria wengine mpaka mwisho wa basi kama ni chanika ama mbagala ama popote basi linapoishia.hii imerahisisha sana usafiri na kupunguza makali ya nauli kwa abiria
 
Anatafuta jinsi ya kula kwa kamba yake huyo. Siku zitaisha na shekilango kitaendelea kuwa kituo holela cha mabasi. Usicheze na kitu inaitwa fweza.
 
Daraja la kuvusha watu lipo
 
Mkuu, Kuna magari hayaingii kabisa pale. Mfano, tahmeed, Kilimanjaro, bm, etc. Kifupi gari nyingi za kwenda kaskazini zinazopaki shekilango hazipiti mbezi(asubuhi) na haziingii(kwa zinazotoka mkoani).
Kuna magari hawana abiria wa stand ya mbezi, huwa wanaenda kulipa uhuru na kuondoka. Mfano gari toka Tanga kwenda Mtwara zinapita stand mbezi wanalipa ushuru na kwenda mbagala, sasa abiria wengi wanashuka shekilango. Sasa mnataka hayo mabasi yasishushe na kupakia abiria shekilango?
 
Mamiradi yote ya Mwendazake ni useless na liability mpaka watu walazimishwe kutatumia..

Bei za pango ni kubwa Sana sasa sijui utamlazimisha mtu akulipe pesa ambayo hana au?

Hivyo hivyo kule Soko la Ndugai,Stand ya Dodoma na maeneo mengi,mamiradi ya mabilioni hayatumiki na CAG alisema hili..

Incompetence of Jiwe Administration.
 

Aisee kuna kipindi nilitoka mbagala naenda kupanda esther kwenda moshi nikakuta basi limeondoka.nilikuwa na watoto na mabegi kadhaa,ilinibidi nichukue tax hadi ubungo ambapo nilipigwa 35000 wakati huo nauli ya kwenda moshi na basi ilikuwa sh.22000/-
 
Ni kweli. Kuna siku nieshuka Mbezi saa 6 usiku kutoka Mwanza, nilipata shida sana kuvuka kuja kupata magari ya Gongolamboto. Kwanza, lile daraja la kuvukia lilikuwa limejaa wahuni. Huwezi kuvukia huko kwa usalama. Pili kuvuka barabara kuu ni risk. Wakati huo magari yanakuwa hayajali, yankimbia kasi sana. Hatari ya kugongwa ni kubwa

Cha msingi, mabasi yanayotokea nje yalipe pamoja na ushuru wa abiria waliowapakia nje ya terminal kama tunavyofanya Ngorongoro na Mayara, ili mapato ya Stendi yasiathirike

Sent from my Infinix X573 using JamiiForums mobile app
 
Pia ni muhimu kuangalia kwa awaingii, watunga sera yaani masta planners kabla wajaplan mradi ni vyema wawashirikishe watumiaji au wadau wa mradi Ili kuchukua maoni yao.
 
Biashara ni ushindani mabus yanafata walipo abiria mengine uanzia gongolamboto , mbagala , chanika, bunju. Nk lengo ni kuwapungumzia mzigo abiria. Maana kukodi tax toka mbagala hadi ufike mbezi ni lazima uwe na sh elf 40 Ili uwahi kupanda basi la alfajiri ambalo nauli yake ni elf 10 au 15.
Kuna haja ya kuliweka sawa hili.
Shekilango ni rahisi kufika Ili kuwahi usafiri kuliko mbezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…