Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 38,657
- 44,759
Ni ngumu sana ku control natureKupiga mbuzi gitaaa...hayo matamko yalishatolewa sanaaaaa hii itakuwa Kama Mara zaidi ya Tano Bado shughuli zote shekilango...sidhani na naona halitatekelezwa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni ngumu sana ku control natureKupiga mbuzi gitaaa...hayo matamko yalishatolewa sanaaaaa hii itakuwa Kama Mara zaidi ya Tano Bado shughuli zote shekilango...sidhani na naona halitatekelezwa
Tuliwashauri wajaribu kwanza kuyaacha magari ya serikali wanayotumia wafanye hizo safari kwa kutumia usafiri wa public waone uhalisia ndipo waje na hayo matamko, ila kwakuwa wanapenda kuwakandamiza tabaka la chini basi inakuwa hakuna namnaHivi
Hivi inaingia akilini mtu anayetoka Mbagala kwenda mikoa ya kusini aje kupandia na kuteremkia mbezi? Wanasiasa huwa wanatoa majibu ya kisiasa kwa tatizo la kitaalamu
Foleni itakuwa ya kufa mtu stand ile bado ndogoStendi ya Magufuli ni Ndogo mbona viongozi wa kisiasa hawa wagumu kuelewa!?
Hivi abood, Alsaedy, Shabiby wakaleta gari zao kwa wakati mmoja si wanajaza stendi yote! Tuwe na busara
Wanasiasa wana akili za hovyo sana, practically wanatengeneza shida ambayo ilishashindikana kutatuliwa huko nyumaSasa si vibaya abiria wengine hasa wenye mizigo wapandie hapo au washukie hapo ukizingatia stendi nyingi hizi mpya zimejengwa mbali na mji.
Una mabasi mangapi? Kile ki stand kidogoSafi sana Waziri simamia hapo hapo tena wafatilie kwa karibu haiwezekani kila mtu apaki anakojua yeye.
Uko sahihi viafisa Serikali vinafunga tai shingoni na visuti mitumba havijui karahaTuliwashauri wajaribu kwanza kuyaacha magari ya serikali wanayotumia wafanye hizo safari kwa kutumia usafiri wa public waone uhalisia ndipo waje na hayo matamko, ila kwakuwa wanapenda kuwakandamiza tabaka la chini basi inakuwa hakuna namna
panda DALADALA au mwendo kasi.Wanazidi kuyafanya maisha kuwa magumu sana
- Kama mtu hana shughuli ya kufanya hapo terminal kwanini ashushwe hapo wakati mabasi yanakwenda mjini?
- Je wana mabasi ya public ya kutosha kuwavusha abiria toka hapo mpaka mjini? DART wamezidiwa na hakuna jitihada zozote za kutatua kero ya usafiri ndani ya jiji, mbona wanaturudisha nyuma?
Population ya sasa haifanani na population ya wakati huo, kwani mabasi ya mikoani yakiwapa lift abiria kwenda na kutoka mjini wewe na serikali mnapungukiwa nini?Hata stendi ya zamani ya Ubungo ilikuwa mbali ma maeneo mengi ya Jiji lkn hapakuwa na tabia hii ya kijinga kila basi kupakia na kushusha abiria wake sehemu yoyote. ila sasa watu wanaanza kuijaribu mamlaka
Hizo huduma haziwatoshelezi hata wakazi wa Dar wenyewe bado unazungumzia kuwaongeza watu kutoka mikoani.panda DALADALA au mwendo kasi.
Mi nimefika hapo kituoni.Waziri wa Tamisemi Mhe. Bashungwa leo amesisitiza mabasi yote yaendayo Mikoani pamoja na nchi jirani lazima yapakie na kushushia abiria katika kituo kikuu cha Mabasi cha Magufuli ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wadau wa usafirishaji.
Ni vyema waziri kalizungumzia hilo maana hali ilipo kuwa imefikia ilikuwa ni vurugu yaani kama vile hakuna wasimamizi wa sheria au hakuna viongozi maana kila basi illikuwa inaamua ikapakie abiria wapi na ikashushie wapi!! askari wapo! wanaangalia jinsi watu wanavyo vunja sheria!!
Hapana, lazima kituo chetu cha Magufuli kitumiwe kama ilivyo kusudiwa, hivyo ni vyema wenye mamlaka wakasimamia hilo.
===
Waziri Bashungwa atoa siku saba Stendi Kuu ya Magufuli-Dar
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa ametoa siku saba kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla kukutana na LATRA, Wadau na Wamiliki wa Mabasi kuweka uratibu mzuri wa kusimamia maelekezo ya Serikali kwa mabasi yote kushusha na kupakia abiria ndani ya Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli jijini Dar es Salaam.
Bashungwa ametoa maelekezo hayo leo Mei 30, 2022 wakati akikagua mradi wa Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli (Magufuli Bus Terminal) kilichopo Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam.
Amesema, Serikali imetumia kiasi cha shilingi bilioni 50 kujenga kituo hicho, hivyo Serikali haitakubaliana na watu ambao hawazingatii utaratibu uliowekwa katika kituo hicho.
“Ninafahamu kuwa Mkuu wa Mkoa, Amos Makalla ameshapokea changamoto ya Mabasi kutoingia ndani ya kituo hiki cha Magufuli na mimi nimekuta changamoto bado iko pale pale, sasa kwa sababu ameshanza kulifanyia kazi nampa siku saba awe amekutana na LATRA pamoja na wadu wa mabasi (TABOA) kuangalia utaratibu wa mabasi yote kuingia ndani ya kituo kushusha na kupakia abiria,”amesema Bashungwa.
Pia Mheshimiwa Bashungwa amemuagiza Mkuu wa Wilaya Ubungo, Kheri James kuweka utaratibu wa kukutana mara kwa mara na Wadau wa Kituo cha Magufuli, Mawakala na Makalani ili kusikiza na kuweka utaratibu wa kutatua changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza katika kituo hicho na kuzifanyia kazi kwa ushirikiano.
Kama viongozi wetu wangekuwa na akili wangefanya utafiti kwanza kabla ya matamko, lakini kwakuwa akili zao ndiyo hizo wanadhani matamko ndiyo kufanya kazi na siyo kutafiti changamoto na kuleta ufumbuziMi nimefika hapo kituoni.
Kituo ni kidogo kwenye maegesho .stand ni kubwa kwa upande ofisi lakini kwa mabasi eneo lao ni dogo hasa upande wa chini asubuhi huwezi kwenda kupaki gari kunakuwa kumejaa sana.
Kwanza heshimu watu, usiite wamiliki wa mabus na abiria wajinga kwa kukataa kuingia magufuli terminal..kwa sabb aliyejenga hakujua hata uhitaji wa stand unataka stand ya aina gani, amepoteza pesa kujenga jengo la ukubwa usiohitajika..na inawezekana walioplan lengo Lao lilikuwa 10% ndio akili yao ilikuwa inaona kwanza, siyo kufahamu kama stand ya aina hiyo ilikuwa inahitajika..panda DALADALA au mwendo kasi.
Hata stendi ya zamani ya Ubungo ilikuwa mbali ma maeneo mengi ya Jiji lkn hapakuwa na tabia hii ya kijinga kila basi kupakia na kushusha abiria wake sehemu yoyote. ila sasa watu wanaanza kuijaribu mamlaka........naomba mamlaka zote ziongeze ukali na kusimamia maamuzi na maelekezo yanayo tolewa
Hapa ni pigo kwa wale wazee wa big brother pale urafik
Ingawa waziri amechelewa kutoa hilo tamko wasiwasi wangu watamtii? Watu wa mabasi ni wakorofi sana. Kuna makampuni kama Dar Express hata Arusha hawaingii stand kuu, Dar wanashusha na kupakia pale Shekilango walinipa shida sana siku moja wakati huo nilitakiwa niunganishe safari kwenda kusini Tunduru kumbuka una mizigo nilipata gharama ya ziada. Hata mabasi yayotoka kusini km Lindi, Mtwara, Masasi, Tnduru, Songea yanaishia Temeke mwisho. Fikiria kesho yake unatakiwa uunge kwenda kaskazini Arusha una mizigo unafikaje stand ya Magufuli. Nawashangaa LATRA ni mpaka waziri awaboost? na Jeshi la Polisi je? Taasisi nyingi za nchi hii zina shida sana.Waziri wa Tamisemi Mhe. Bashungwa leo amesisitiza mabasi yote yaendayo Mikoani pamoja na nchi jirani lazima yapakie na kushushia abiria katika kituo kikuu cha Mabasi cha Magufuli ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wadau wa usafirishaji.
Ni vyema waziri kalizungumzia hilo maana hali ilipo kuwa imefikia ilikuwa ni vurugu yaani kama vile hakuna wasimamizi wa sheria au hakuna viongozi maana kila basi illikuwa inaamua ikapakie abiria wapi na ikashushie wapi!! askari wapo! wanaangalia jinsi watu wanavyo vunja sheria!!
Hapana, lazima kituo chetu cha Magufuli kitumiwe kama ilivyo kusudiwa, hivyo ni vyema wenye mamlaka wakasimamia hilo.
===
Waziri Bashungwa atoa siku saba Stendi Kuu ya Magufuli-Dar
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa ametoa siku saba kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla kukutana na LATRA, Wadau na Wamiliki wa Mabasi kuweka uratibu mzuri wa kusimamia maelekezo ya Serikali kwa mabasi yote kushusha na kupakia abiria ndani ya Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli jijini Dar es Salaam.
Bashungwa ametoa maelekezo hayo leo Mei 30, 2022 wakati akikagua mradi wa Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli (Magufuli Bus Terminal) kilichopo Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam.
Amesema, Serikali imetumia kiasi cha shilingi bilioni 50 kujenga kituo hicho, hivyo Serikali haitakubaliana na watu ambao hawazingatii utaratibu uliowekwa katika kituo hicho.
“Ninafahamu kuwa Mkuu wa Mkoa, Amos Makalla ameshapokea changamoto ya Mabasi kutoingia ndani ya kituo hiki cha Magufuli na mimi nimekuta changamoto bado iko pale pale, sasa kwa sababu ameshanza kulifanyia kazi nampa siku saba awe amekutana na LATRA pamoja na wadu wa mabasi (TABOA) kuangalia utaratibu wa mabasi yote kuingia ndani ya kituo kushusha na kupakia abiria,”amesema Bashungwa.
Pia Mheshimiwa Bashungwa amemuagiza Mkuu wa Wilaya Ubungo, Kheri James kuweka utaratibu wa kukutana mara kwa mara na Wadau wa Kituo cha Magufuli, Mawakala na Makalani ili kusikiza na kuweka utaratibu wa kutatua changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza katika kituo hicho na kuzifanyia kazi kwa ushirikiano.
Nilitaka kuuliza hiki kitu. Mfano abiria tayari ana ticket. Anapandia Shekilango bus likitoka pale linapita Mbezi stendi ya Magufuli linakia abiria wengine na kuendelea na safari. Wakati wa kurudi ni hivyo hivyo. What is wrong with that? Au abiria wakipandia na kushuka stendi ya Magufuli kuna tozo au ada yoyote wanalipa apart from the ticket? Naomba kueleweshwa.Mtoa mada unafurahia ujinga tu bila kutumia Busara, Basi likianzia Mbagala halafu likaingia hapo Magufuli likalipa ushuru kama kawaida nini kitapungua? Kuna abiria wanatoka mbali sana kumbuka.