Waziri Bashungwa atoa siku 7 mabasi yote ya mikoani yawe yanaingia Magufuli Bus Terminal, si Shekilango

Waziri Bashungwa atoa siku 7 mabasi yote ya mikoani yawe yanaingia Magufuli Bus Terminal, si Shekilango

Stendi ya Magufuli ni Ndogo mbona viongozi wa kisiasa hawa wagumu kuelewa!?

Hivi abood, Alsaedy, Shabiby wakaleta gari zao kwa wakati mmoja si wanajaza stendi yote! Tuwe na busara
Labda ungeanza kutafuta maana ya kituo cha mabasi (bus station) na uendeshaji wake ndio uandike
 
ALIYESHIBA HAMJUI MWENYE NJAA !! WAO WANAJUA KILA MTU HAWEZI KUKOSA PESA YA KUKODISHA TAXI YA KUMFIKISHA STENDI YA MAGUFULI !! KUMBE WAPO WANAOSAFIRI HATA PESA YA CHAKULA NJIANI HAWANA !!
We

Wenye kupambana na Hali Yao wanatamani Mabasi yawachukue karibia na wanakoishi, ila wanasiasa wasiojua ukubwa WA dar, na ambao wanawachanganya wenye mabasi waliotoa huruma kuwasaidia wananchi wao wapo dodoma wanasababishia Dar matatizo, huyu Waziri sijui anatafakari vipi!?
 
Hapo ambapo hakuna choo?
Tunawasaidia nyie Walala hoi msianze kuleta vipingamizi...Sisi hatutumii hizo stendi zenu tunapanda Ndege au ma V8.

Kama ni suala la kwenda choo Dreva atasimama huko njiani mtaingia vichakani mchimbe dawa.
 
Stendi kujengwa kwa billion 50 sio hoja yenye nguvu kusababisha mabasi yote yaingie hapo.
 
Inasikitisha sana
Tatizo moja la stendi ya Magufuli ni kwamba haliko accesible kwa mabasi madogo yanayoleta na kupokea wasafiri.

Magufuli alisema anatambua ile ni stendi ya wanyonge na akataka iwahudumie accordingy.

Sasa watu wanaosafiri na mabasi ya mikoani hawaletwi pale au kupokelewa pale na ma landcruisers binafsi.

Lakini stendi kuu ya daladala, Mbezi Louis, iko opposite side of the highway. Wengi watapondwa na magari.

Tatizo la nchi yetu, watu wanao design miundombinu na mifumo mbali mbali ya umma, wao hawaitumii, kwa hiyo hawajui inavyofanya na isivyofanya kazi.

Disastrously poor designing.
 
Hiyo stendi ilipaswa kujengwa na kusimamiwa na Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam, haya ni matokeo ya kukosekana ugatuzi wa madaraka. Kituo hicho kujengwa na kusimamiwa na wabunge kutoka Kisarawe na Karagwe ni tatizo kubwa.
 
Sijui huyu Waziri anamfurahisha nani watu wanaamka saa Tisa hawajui watafikaje huko Magufuli!? Yeye ana vx anajifanyisha kuwatetea!?
Anadhani kila MTU anamiliki Mavieite !!
 
Tunawasaidia nyie Walala hoi msianze kuleta vipingamizi...Sisi hatutumii hizo stendi zenu tunapanda Ndege au ma V8.

Kama ni suala la kwenda choo Dreva atasimama huko njiani mtaingia vichakani mchimbe dawa.
Exactly, ndivyo wanavyotuchukulia !!
 
Mtoa mada unafurahia ujinga tu bila kutumia Busara, Basi likianzia Mbagala halafu likaingia hapo Magufuli likalipa ushuru kama kawaida nini kitapungua? Kuna abiria wanatoka mbali sana kumbuka.
Yaani kuna watu wa ajabu mtu anafurahia bila kuangalia kuna watu wanatoka Kigamboni na basi kama kilimanjaro linatoa huduma huko kuwapunguzia garama na usumbufu fikiria mtu anayetoka saa basi saa 12 anaishi kigamboni. Kama issue ni kuingia Stendi Mbezi wafanye kama stendi ya Pwani Gari inaingia kuchukua abiria na kutoka. Au mnataka watu walipe nali ya taxi kubwa kuliko nauli ya basi?
Mtu anayesafiri Morogoro Aboud 8000 akitokea Kinondoni hadi Mbezi taxi 30,000 yaani apewe mzigo msafiri kweli?
 
Back
Top Bottom