Waziri Bashungwa atoa siku 7 mabasi yote ya mikoani yawe yanaingia Magufuli Bus Terminal, si Shekilango

Mtoa mada unafurahia ujinga tu bila kutumia Busara, Basi likianzia Mbagala halafu likaingia hapo Magufuli likalipa ushuru kama kawaida nini kitapungua? Kuna abiria wanatoka mbali sana kumbuka.
Shida yao si ushuru vipi wakilipa bila kuingia je.
Kuna vistand vingine njiani unakuta basi linaingia halisimami kisha linaondoka hii inapunguza mda wa safarii,kwann wasichukue tu pesa bila kulazimisha mabus kuingia wakati hakuna abiria wa kupanda au kushuka,mfano stand ya kibaha,basi linazunguka weee,pili stand zote zijengwe jirani na barabara kuu na sio uchochoroni.
 
Kama Yule aliyeugua tezi dume na kwenda mutinies marekani,hatakufariki ,Tanzania haitapata amani na utulivu especially kupitia CCM.
Huyo mbona siku zake zinahesabika ni swala la muda tu , huyo ni adui no 1 wa tz ameiweka nchi chini ya mikono ya mafisadi wachache wa kiarabu na kiindi na mabeberu ,sasa hivi CCM NI SAKOZI YA KINA ROSTAM ,ABUDI,MANJI, ZUNGU NA GSM , na pesa za serikali ni mali yao wanachota watakavyo.
 
Mimi nilishauri kuanzia kimara hadi kiluvya yote wangeibulldozer iwe flat waondoe vilima vyote kisha wajenge mji wa kibiashara. Darcity one stop center yaani KILA kitu sehemu moja Ili kupunguza ulazima wa watu kuja mjini.

Kimara yote ile hadi jirani na stand ya Magufuli, vilima na vibonde visambaratishwe vyote pawe flat Ili zipatikane heka 300 pajengwe business center, pajengwe soko kubwa Sana la bidhaa toka mikoani, zijengwe supermarket kubwa sana, macomplex makubwa Sana , mahotel,magest house,vilabu vya pombe za kienyeji,magodown makubwa Sana, viwanja vya michezo, bustani kubwa Sana, stand nzuri za daladala iwe jirani na stand ya mabus, parking kubwa Sana za mabus na malori,mabenk, makumbi makubwa ya sinema, music, nk, sehemu za machinga, magarage, viwanda vidogo vidogo, vituo vya bodaboda na bajaj, nk yaani pawe ni one stop border. Lengo ni nini Ili wafanyabiashara wote watokao ndani na nje ya nchi wapate pa kuchukuliwa bidhaa zao na kupata huduma zote sehemu moja,nchi kama zimbabwe, zambia, Congo, Malawi, Comoro kwa wingi Sana watu wao huja KILA siku nchini yaani wao TANZANIA ndio Dubai yao, wapanga sera watengeneze mazingira mazuri ya kuchukua pesa zao.
Faida ya mradi hii. Itazaliza ajira milioni 2,jiji na serikali watapata mapato mengi zaidi. Mradi utapendezesha mji. Mradi kama huu pia ujengwe Tunduma mkoa wa Songwe, Isaka Shinyanga.Na sehemu zingine nchini zenye muingiliano Mkubwa wa watu na nchi za jirani.
 
Mtoa mada unafurahia ujinga tu bila kutumia Busara, Basi likianzia Mbagala halafu likaingia hapo Magufuli likalipa ushuru kama kawaida nini kitapungua? Kuna abiria wanatoka mbali sana kumbuka.
Kuweni na utaratibu wa kusomba abiria wenu na coaster hadi stand kuu kwenye bus kuu,pia mnatupunguzia msongamano na hayo ma bus yenu, maana yana occupy more space kwa roads za Mijini!!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Hapa ni pigo kwa wale wazee wa big brother pale urafik
Pigo kivipi?
Sijaona sehemu iliyoandikwa "waziri kazuia mabasi yasishushe au kupakia big brother au kwingineko"

Swala hapa Ni wewe mwenye Basi nenda popote upendako ila sharti lazima upite magufuli stand ,uingie ili ulipe ushuru serikali ipate mapato..

Wito wangu:Tuwe tunasoma vizuri taarifa tukiwa na Afya ya akili
 
Upuuzi kama ule ukitoka Moshi kwenda Arusha unalazimishwa uingie stand ya Hai bila sababu
Sasa sisi wa Manzese, Sinza, Kino, Mabibo na maeneo jirani tuanze safari saa ngapi na tulipie bajaj kiasi gani twende tukapande basi Mbezi ilhali tungepandia Shekilango
Nani yule alisema nchi inatawaliwa na washamba tena?
 
Huu ni upuuzi mkubwa sana. jiji la Dar es salaam ni kubwa sana kijiografia. Watu wanatoka maeneo zaidi ya km 50 ili kuifikia stand ya Magufuli. Mtu anatoka chanika apande dalala hadi mbezi itamchukua muda mrefu na gharama kubwa. Kuna mabasi yamesogeza huduma hadi wananchi walipo. Zipo gari zinaanzia Chanika kwenda Arusha na Kilimanjaro na wakazi wa huko wanapanda hizo gari kwasababu zinawarahisishia maisha. Stand ya mabasi siyo kitega uchumi ni huduma kwa wananchi. Sasa huduma ikiwa kero hiyo huduma siyo huduma tena. Mtu akishushwa pale stand ya Magufuli anamizigo na watoto asafiri hadi kigamboni atafika lini? Position ya stand ya Magufuli ndilo tataizo wala siyo mabasi yanayojitahidi kufikisha huduma karibu na mwananchi. Ukifika kwenye ile stand kukata tiketi unaweza kuchoka kabla ya kukata tiketi kwasababu ya kero ya wapiga debe. ukienda shekilango unachangua mwenyewe unataka basi lipi na hakuna kero ndogo ndogo. Narudia tena stand ya mabasi siyo kitegauchumi ni huduma kama yalivyo maji na umeme na barabara.
 
Stendi ya Magufuli ni lango kuu la Uchumi wa Jiji la DSM ni Nchi kwa Ujumla Endapo tu viongozi wenye dhamana watasimamia kikamilifu stendi hiyo vinginevyo mapato yote yataingia kwenye mifuko ya watu binafsi.

Viongozi Someni Mapendekezo ya CAG ktk Ripoti yake ya 2022/2023 kuhusu Stendi ya mabasi ya Magufuli.
 
Haya yote ni matokeo ya kukurupuka katika kufanya maamuzi. Ubungo lilikuwa ni eneo mwafaka kwa stendi kuendelea kuwepo pale. Unaweka stendi Mbezi mbali na sehemu nyingi za Dar na usafiri wa kwenda huko ni mgumu. Fikiria mtu anatoka Chanika, Mbagala, Chamazi, Kigamboni, Gongolamboto na maeneo mengine ya mbali hadi Mbezi ni changamoto kubwa.
 
Hiyo aya ya mwisho nimekuelewa sana
 
Huyu ndo mfano wa mawaziri mizigo..

Kwamba msafiri anayekwenda Mbagala, au Kigamboni, au Gogo la Mboto kutokea Mwanza au Kigoma au Bukoba alazimike tu kuingia Magufuli Terminal kisa tu ya hizo bil.50 au hilo jina la hiyo Stand?
 
Hivi
Hivi inaingia akilini mtu anayetoka Mbagala kwenda mikoa ya kusini aje kupandia na kuteremkia mbezi? Wanasiasa huwa wanatoa majibu ya kisiasa kwa tatizo la kitaalamu
 
Kupiga mbuzi gitaaa...hayo matamko yalishatolewa sanaaaaa hii itakuwa Kama Mara zaidi ya Tano Bado shughuli zote shekilango...sidhani na naona halitatekelezwa
 
Wanazidi kuyafanya maisha kuwa magumu sana
  1. Kama mtu hana shughuli ya kufanya hapo terminal kwanini ashushwe hapo wakati mabasi yanakwenda mjini?
  2. Je wana mabasi ya public ya kutosha kuwavusha abiria toka hapo mpaka mjini? DART wamezidiwa na hakuna jitihada zozote za kutatua kero ya usafiri ndani ya jiji, mbona wanaturudisha nyuma?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…