Waziri Bashungwa atoa siku 7 mabasi yote ya mikoani yawe yanaingia Magufuli Bus Terminal, si Shekilango

Kupiga mbuzi gitaaa...hayo matamko yalishatolewa sanaaaaa hii itakuwa Kama Mara zaidi ya Tano Bado shughuli zote shekilango...sidhani na naona halitatekelezwa
Ni ngumu sana ku control nature
 
Stendi ya Magufuli ndio stendi pekee nchini inayo ingiza mabasi kutoka mikoa yote pamoja na nchi za Kenya, Uganda, Zambia, Malawi, DRC, Rwanda n.k.
Hivyo stendi hii ni uchumi kwa nchi yetu.
 
Nashauri kila bus linaloanza/maliza safari DSM lilipie ushuru hata kama haliingii stendi ya JPM.Endapo bus litakamatwa barabarani halina risiti ya stendi ya JPM lipigwe faini ya kuanzia 1M ili heshima irudi.
Hii nchi hivi sasa kila mtu ni kambale ana ndevu na manyoya ya chini.
 
Hivi

Hivi inaingia akilini mtu anayetoka Mbagala kwenda mikoa ya kusini aje kupandia na kuteremkia mbezi? Wanasiasa huwa wanatoa majibu ya kisiasa kwa tatizo la kitaalamu
Tuliwashauri wajaribu kwanza kuyaacha magari ya serikali wanayotumia wafanye hizo safari kwa kutumia usafiri wa public waone uhalisia ndipo waje na hayo matamko, ila kwakuwa wanapenda kuwakandamiza tabaka la chini basi inakuwa hakuna namna
 
Stendi ya Magufuli ni Ndogo mbona viongozi wa kisiasa hawa wagumu kuelewa!?

Hivi abood, Alsaedy, Shabiby wakaleta gari zao kwa wakati mmoja si wanajaza stendi yote! Tuwe na busara
Foleni itakuwa ya kufa mtu stand ile bado ndogo
 
Sasa si vibaya abiria wengine hasa wenye mizigo wapandie hapo au washukie hapo ukizingatia stendi nyingi hizi mpya zimejengwa mbali na mji.
Wanasiasa wana akili za hovyo sana, practically wanatengeneza shida ambayo ilishashindikana kutatuliwa huko nyuma
 
Lazima viongozi awetu wawe IMARA kusimamia maamuzi, tuache ulegevu, wala tusikubali kuyumbishwa na maneno maneno yasiyo ya msingi
 
Tuliwashauri wajaribu kwanza kuyaacha magari ya serikali wanayotumia wafanye hizo safari kwa kutumia usafiri wa public waone uhalisia ndipo waje na hayo matamko, ila kwakuwa wanapenda kuwakandamiza tabaka la chini basi inakuwa hakuna namna
Uko sahihi viafisa Serikali vinafunga tai shingoni na visuti mitumba havijui karaha

Vipande usafiri wa mabasi mikoani vipate uhalisia wa karaha ya abiria kuhusiana na hiyo stendi
 
panda DALADALA au mwendo kasi.

Hata stendi ya zamani ya Ubungo ilikuwa mbali ma maeneo mengi ya Jiji lkn hapakuwa na tabia hii ya kijinga kila basi kupakia na kushusha abiria wake sehemu yoyote. ila sasa watu wanaanza kuijaribu mamlaka........naomba mamlaka zote ziongeze ukali na kusimamia maamuzi na maelekezo yanayo tolewa
 
Hata stendi ya zamani ya Ubungo ilikuwa mbali ma maeneo mengi ya Jiji lkn hapakuwa na tabia hii ya kijinga kila basi kupakia na kushusha abiria wake sehemu yoyote. ila sasa watu wanaanza kuijaribu mamlaka
Population ya sasa haifanani na population ya wakati huo, kwani mabasi ya mikoani yakiwapa lift abiria kwenda na kutoka mjini wewe na serikali mnapungukiwa nini?
 
ABIRIA WA NJIA YA BAGAMOYO TUNAOELEKEA KASKAZINI PIA SISI NI WATU TUNASTAHILI STAND NZURI SAWASAWA NA WATU WA NJIA YA KATI.
°position matters alkadhalka magari ya kusini nayo yapate stand labda mbagala au mbele zaidi
 
Mi nimefika hapo kituoni.
Kituo ni kidogo kwenye maegesho .stand ni kubwa kwa upande ofisi lakini kwa mabasi eneo lao ni dogo hasa upande wa chini asubuhi huwezi kwenda kupaki gari kunakuwa kumejaa sana.
 
Mi nimefika hapo kituoni.
Kituo ni kidogo kwenye maegesho .stand ni kubwa kwa upande ofisi lakini kwa mabasi eneo lao ni dogo hasa upande wa chini asubuhi huwezi kwenda kupaki gari kunakuwa kumejaa sana.
Kama viongozi wetu wangekuwa na akili wangefanya utafiti kwanza kabla ya matamko, lakini kwakuwa akili zao ndiyo hizo wanadhani matamko ndiyo kufanya kazi na siyo kutafiti changamoto na kuleta ufumbuzi
 
Kwanza heshimu watu, usiite wamiliki wa mabus na abiria wajinga kwa kukataa kuingia magufuli terminal..kwa sabb aliyejenga hakujua hata uhitaji wa stand unataka stand ya aina gani, amepoteza pesa kujenga jengo la ukubwa usiohitajika..na inawezekana walioplan lengo Lao lilikuwa 10% ndio akili yao ilikuwa inaona kwanza, siyo kufahamu kama stand ya aina hiyo ilikuwa inahitajika..
Hivi niwaulize waliojenga, priority ni mapato au huduma nzuri na rahisi kwa wananchi? Mbona wanahimiza ujenzi wa vituo vya afya na hospitali kila eneo, kwa nini hawasemi watu wote wa Dsm waende kutibiwa Temeke, au Mwananyamala au Muhimbili? au usafirishaji siyo huduma? Wenye mabus kuweka vituo vyao karibu na wanaowahudumia kosa liko wapi? Unalazimisha watu wapitishwe mbezi hata km bus halina abiria anayepandia terminal unatumia akili kweli? Km ni kodi, kodi ngapi wenye mabus wanalipa..
Mjifunze kuheshimu watu/walipa kodi wao ndio wanafanya wamiliki wa mabus waweke vituo shekilango au waanzie safari kigamboni..tafuteni vyanzo vingine vya mapato mlipe hayo madeni ya kujenga hiyo stand, sabb ham kufikiri sawa sawa kabla ya kujenga hiyo terminal..
 
Ingawa waziri amechelewa kutoa hilo tamko wasiwasi wangu watamtii? Watu wa mabasi ni wakorofi sana. Kuna makampuni kama Dar Express hata Arusha hawaingii stand kuu, Dar wanashusha na kupakia pale Shekilango walinipa shida sana siku moja wakati huo nilitakiwa niunganishe safari kwenda kusini Tunduru kumbuka una mizigo nilipata gharama ya ziada. Hata mabasi yayotoka kusini km Lindi, Mtwara, Masasi, Tnduru, Songea yanaishia Temeke mwisho. Fikiria kesho yake unatakiwa uunge kwenda kaskazini Arusha una mizigo unafikaje stand ya Magufuli. Nawashangaa LATRA ni mpaka waziri awaboost? na Jeshi la Polisi je? Taasisi nyingi za nchi hii zina shida sana.
 
Mtoa mada unafurahia ujinga tu bila kutumia Busara, Basi likianzia Mbagala halafu likaingia hapo Magufuli likalipa ushuru kama kawaida nini kitapungua? Kuna abiria wanatoka mbali sana kumbuka.
Nilitaka kuuliza hiki kitu. Mfano abiria tayari ana ticket. Anapandia Shekilango bus likitoka pale linapita Mbezi stendi ya Magufuli linakia abiria wengine na kuendelea na safari. Wakati wa kurudi ni hivyo hivyo. What is wrong with that? Au abiria wakipandia na kushuka stendi ya Magufuli kuna tozo au ada yoyote wanalipa apart from the ticket? Naomba kueleweshwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…