Waziri Bashungwa atoa siku 7 mabasi yote ya mikoani yawe yanaingia Magufuli Bus Terminal, si Shekilango

Stendi ya Magufuli ni Ndogo mbona viongozi wa kisiasa hawa wagumu kuelewa!?

Hivi abood, Alsaedy, Shabiby wakaleta gari zao kwa wakati mmoja si wanajaza stendi yote! Tuwe na busara
Wanasiasa hawana kauli za ukweli hata kama ukweli wanujua
Basi za kusini nyongibzinaondokea temeke na mbagala , kama hili nalo linawahusu hapo magufuli stand itakuwa ni kero
 
Stendi ya Magufuli ni Ndogo mbona viongozi wa kisiasa hawa wagumu kuelewa!?

Hivi abood, Alsaedy, Shabiby wakaleta gari zao kwa wakati mmoja si wanajaza stendi yote! Tuwe na busara
Kwa hiyo wanataka watu wote kupandia na kushuka stendi ya Magufuli wakati bus linaelekea mjini mpaka Shekilango au Mbagala likiwa tupu. Halafu wale abiria walioshuka stendi ya Magufuli waanze kuhangaika tena na usafiri wa kwenda Mbagala kwa pesa nyingine tena!!!!

Aliyewaloga viongozi wa CCM alishakufa!!! Hata mtoto wa darasa la 4 atashangaa!!!
 
Maamuzi mengine kama haya waziri anatakiwa akutane na wadau wa usafirishaji kwanza si kukurupuka tu. Mabasi yote yaingie magufuli, patatosha? Yaani gari la kwenda mtwara, kwa mfano liko temeke na abiria wote wanajua hilo kisha liende mbezi kwanza?

Hiyo magufuli bus terminal in ukubwa gani kuweza kubeba mabasi 200-300 kwa wakati mmoja? au ndiyo bado waziri anaishi zama za kumwabudu mtu na hivyo anadhani jina limeanza kufifia>
 
Hiyo stend haiwezi kuhimili mabasi yote Kwa Muda wa Asubhi aache utani
 
Hawakufikiri kabla ya kujenga
 
Mkuu, Kuna magari hayaingii kabisa pale. Mfano, tahmeed, Kilimanjaro, bm, etc.

Kifupi gari nyingi za kwenda kaskazini zinazopaki Shekilango hazipiti Mbezi(asubuhi) na haziingii(kwa zinazotoka mkoani).
Sasa kama hakuna ulazima, kwanini mlazimishe zipite?
 
Mtoa mada unafurahia ujinga tu bila kutumia Busara, Basi likianzia Mbagala halafu likaingia hapo Magufuli likalipa ushuru kama kawaida nini kitapungua? Kuna abiria wanatoka mbali sana kumbuka.
Well said. Hii serikali inalazimisha kufanya maisha ya wana Dar es Salaam kuwa magumu sana bila sababu ya msingi. Ili mtu atoke Chanika/ Vikindu, Kisarawe II, au Mgeni Nani awahi basi saa 12:00 asubuhi kituo cha Magufuli inabidi alale stendi. Kama atalala nyumbani kwake atalazimika kukodi usafiri ambao utamgharimu fedha nyingi sana. Baadhi ya makampuni ya mabasi yameweka utaratibu wa kuanzia maeneo mbalimbali na abiria, na baadaye ayanapita Stendi ya Magufuli yanachukua abiria wanapandia hapo, hayapitizi kabisa. Vile vile mabasi yanayoanzia Urafiki yanachukua abiria wa maeneo ya karibu na hapo yanaondoka nao hadi stendi ya Magufuli yanalipa ushuru, shida iko wapi?
 
Mtoa mada unafurahia ujinga tu bila kutumia Busara, Basi likianzia Mbagala halafu likaingia hapo Magufuli likalipa ushuru kama kawaida nini kitapungua? Kuna abiria wanatoka mbali sana kumbuka.
Hii ni kutaka kuwatesa abiria tu, Abiria anayetokea mbagala akodishe taxi kutoka mbagala mpaka stendi ya Magufuli atatozwa bei gani ??!! Au waziri amesahau kuwa watu wengi nchi hii hawana magari ya kutembelea !! Na Madaladala asubuhi huwa ni vurugu tu na kuibiana !! Kuna tatizo gani abiria wakipandia sehemu nyingine baadhi yao na kisha Bus lipitie hapo Stendi ya Magufuli ??
 
Kweli kabisa !! Huwa wanasahau kuwa watu wengi nchi hii wana hali ngumu za maisha !! Waswahili husema " ALIYESHIBA HAMJUI MWENYE NJAA "
 
Wamiliki wa mabasi pamoja na wananchi hawapendi jina la kituo hicho, hawakutaka kiitwe magufuli, wanamchukia sana
 
CAG akikagua hiyo bilioni 50, tutarudi hapa tumeshikana masharti, bilioni 50 na bado stendi haijaisha
 
Nchi ya matamko

Mama anaridhika na matamko na usingizi mzuri anaupata[emoji1787]
 
Huyu Waziri hajui kwamba anazipunguza kwa wingi kura za CCM mwaka 2025 kwa amri anazotoa.
 
We
Stendi ya Magufuli ni Ndogo mbona viongozi wa kisiasa hawa wagumu kuelewa!?

Hivi abood, Alsaedy, Shabiby wakaleta gari zao kwa wakati mmoja si wanajaza stendi yote! Tuwe na busara
Wenye kupambana na Hali Yao wanatamani Mabasi yawachukue karibia na wanakoishi, ila wanasiasa wasiojua ukubwa WA dar, na ambao wanawachanganya wenye mabasi waliotoa huruma kuwasaidia wananchi wao wapo dodoma wanasababishia Dar matatizo, huyu Waziri sijui anatafakari vipi!?
 
Stendi ile haina miundombinu accessible. Ingetakiwa eneo liwe na accessible train au dalalala za kuelekea mjini.
Sijui huyu Waziri anamfurahisha nani watu wanaamka saa Tisa hawajui watafikaje huko Magufuli!? Yeye ana vx anajifanyisha kuwatetea!?
 
Huyu Waziri hajui kwamba anazipunguza kwa wingi kura za CCM mwaka 2025 kwa amri anazotoa.
Hajui analolifanya Kwa kweli sijui kinamuwasha nini huyu Mtu, alizuia boda boda kuwekewa utaratibu na kuvuruga Jiji lote na Bado anazidi kufanya mambo yake ya kuchefua watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…