GE2025 Waziri Bashungwa: Polisi boresheni doria mtandaoni kama mnavyofanya mitaani ili kudhibiti wanaotaka kuvuruga amani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Naunga mkono hojaaaa...watu wamezid yaan i habari za uongo na matusi ya ovyooo ,tena waanze kupiga doria Facebook,insta ,afu ndio jf 😃

Akiwa anazungumza leo, Waziri Bashungwa amemtaka IGP na Jeshi La Polisi kwa ujumla waboreshe "doria za mtandaoni" kama ambavyo wanafanya doria mtaani.

Amesema Doria za mtandaoni zitasaidia kuondoa utapeli pamoja na kukamata wahalifu ambao wanania ya kuvunja amani

=========
​
BASHUNGWA AMUAGIZA IGP KUDHIBITI WAHALIFU WANAOTUMIA MITANDAO KUVURUGA AMANI.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura, kuhakikisha Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama linaimarisha doria mtandaoni (online patrol) kwa lengo la kudhibiti baadhi ya wahalifu wanaotumia mitandao kuvuruga amani na utulivu wa nchi, pamoja na kukabiliana na uhalifu unaofanyika kwa njia ya mtandao.

Bashungwa ametoa agizo hilo leo, tarehe 6 Agosti 2025, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo kipya cha Polisi cha "Daraja B" kilichopo Sanya Juu, Wilaya ya Siha, mkoani Kilimanjaro, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kuboresha miundombinu ya majengo na vitendea kazi ndani ya Jeshi la Polisi.
ā€œIGP, kwa sasa baadhi ya wahalifu wamehamia kwenye mitandao. Kama mnavyofanya doria za kawaida, vivyo hivyo tuimarishe doria mtandaoni ili kudhibiti wizi wa kifedha na wahalifu wanaolenga kuvuruga amani na utulivu wa nchi yetu kupitia mitandao,ā€ amesisitiza Bashungwa.

Aidha, Waziri Bashungwa amelielekeza Jeshi la Polisi kuendelea kutekeleza maagizo mbalimbali ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, yanayohusu kupambana na uhalifu, udhibiti wa madereva wazembe, pamoja na kuondoa vyombo vya moto visivyokidhi viwango vinavyosababisha ajali barabarani.

Bashungwa amelitaka Jeshi la Polisi kushirikiana na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kubaini maeneo hatarishi katika barabara kuu ambazo zimekuwa zikiripotiwa kusababisha ajali mara kwa mara, ili yafanyiwe upembuzi yakinifu na kutengewa bajeti kwa ajili ya kutafutiwa suluhisho la kudumu.
Katika hatua nyingine, Bashungwa amelitaka Jeshi la Polisi kuendelea kushirikiana na madereva wa pikipiki (boda boda) kwa kukutana na viongozi wao katika ngazi ya wilaya na mikoa ili kuwapa elimu ya usalama barabarani na kuweka mikakati ya pamoja ya kupunguza ajali nchini.

Kadhalika, Bashungwa ameviagiza vyombo vyote vya usalama vilivyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuendelea kushirikiana katika kuimarisha amani, usalama na utulivu, hasa katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 na baada ya uchaguzi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura, ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kudumisha amani na utulivu, huku akiwatoa hofu Watanzania kwa kuwahakikishia kuwa nchi ipo salama na itaendelea kuwa salama.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, amesema kuwa kituo cha Polisi cha Wilaya ya Siha kimejengwa kwa fedha za Serikali kupitia Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na michango ya wananchi wa wilaya hiyo.
 
Endelea kusoma zaidi, pia imeandikwa kuhusu kukoma wadhifa wa uwaziri.
Pia tafuta kujua wakati Kikwete anamalizia awamu yake ya mwisho Baraza la Mawaziri lilivunjwa lini.
Vifungu unavyovitaja ni uhuni uliowekwa na Kikwete mwenyewe.

Sharti kuu la kuwa Waziri ni uwe mbunge.
 
Polisi nao sio WAJINGA wakusikiliza kila tamko hii dunia ya Leo huwezi kuzuia mitandao isiongee.
Acha ujinga na wew Kwan kazuia mitandao isiongee ?
Matusi na habari za uongo hazitakiw kwenye mitandaoni mbona Hilo liko wazi ?
Apo kakosea nn Sasa au. Na ww ni mmoja wa waleta habar za uongo kwenye mitandao
 
Hizi Banana Republics zinashida kama nini.

Yani nyie mnaoshindwa hata kuwa na umeme ambao haukatwi katwi hovyo hamna kazi za kutosha.

Focus on the real issues.

Kwa watu wengi ambao hawana makando kando hii nchi haikaliki.

Uonevu kila mahali.

Na mnauongeza kila siku.

Utaongezaje uchumi hamna umeme unaoeleweka.

Hata mtu akisema aanze kuuza ice cream fridge itawaka mfululizo kweli ? Biashara kubwa zaidi ndio usiseme.

Halafu mnakataga umeme kama TANESCO inakisirini, kama inajaribu kuua vitu vya watu makusudi.

Hamwezagi kukata moja kwa moja mpaka ukate urudishwe ukate urudishwe. Na tuliosomaga na mishuma kwa sababu ya mascandal ya serikali tunakumbuka.

Home affairs -- baki na kulinda wananchi -- wananchi wananyanyaswa sana -- watu serekelani wanaabuse raia -- what do you do about it ?

Mnafanya nini kukomoa ufisadi serekalini ambao mpaka mtaani sasa imetegeneza culture ya watu kutokuwa waaminifu -- watu wakiona watu walioko na madaraka wanafanya vitu ambavyo hawapaswi kufanya -- nawao wanapata signal kuwa utapeli unakubalika kote.
Huyo sio wazir wa nishati ebu tuliza wenge
 
TANESCO inavyooperate vibaya miaka nenda rudi na uharibifu wao inahusu mambo ya ndani kwa hiyo usianzishe mabishano ambayo hauwezi kumaliza.

Kuzima umeme hovyo hovyo kwa wananchi maskini bila mipango na taarifa ni uhalifu tayari.

The way TANESCO is run in itself inatuweka kwenye league ya failed states kabla hata hatujaongelea mengine.
 
Acha ujinga na wew Kwan kazuia mitandao isiongee ?
Matusi na habari za uongo hazitakiw kwenye mitandaoni mbona Hilo liko wazi ?
Apo kakosea nn Sasa au. Na ww ni mmoja wa waleta habar za uongo kwenye mitandao
Nchi nyingi za Africa ushindwa kutofautisha kati ya tusi na kukosoa.
 
Uraibu wa madaraka unawasumbua wabantu level of immaturity.
 
Akiwa anazungumza leo, Waziri Bashungwa amemtaka IGP na Jeshi La Polisi kwa ujumla waboreshe "doria za mtandaoni" kama ambavyo wanafanya doria mtaani.

Amesema Doria za mtandaoni zitasaidia kuondoa utapeli pamoja na kukamata wahalifu ambao wanania ya kuvunja amani

=========
​
BASHUNGWA AMUAGIZA IGP KUDHIBITI WAHALIFU WANAOTUMIA MITANDAO KUVURUGA AMANI.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura, kuhakikisha Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama linaimarisha doria mtandaoni (online patrol) kwa lengo la kudhibiti baadhi ya wahalifu wanaotumia mitandao kuvuruga amani na utulivu wa nchi, pamoja na kukabiliana na uhalifu unaofanyika kwa njia ya mtandao.

Bashungwa ametoa agizo hilo leo, tarehe 6 Agosti 2025, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo kipya cha Polisi cha "Daraja B" kilichopo Sanya Juu, Wilaya ya Siha, mkoani Kilimanjaro, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kuboresha miundombinu ya majengo na vitendea kazi ndani ya Jeshi la Polisi.
ā€œIGP, kwa sasa baadhi ya wahalifu wamehamia kwenye mitandao. Kama mnavyofanya doria za kawaida, vivyo hivyo tuimarishe doria mtandaoni ili kudhibiti wizi wa kifedha na wahalifu wanaolenga kuvuruga amani na utulivu wa nchi yetu kupitia mitandao,ā€ amesisitiza Bashungwa.

Aidha, Waziri Bashungwa amelielekeza Jeshi la Polisi kuendelea kutekeleza maagizo mbalimbali ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, yanayohusu kupambana na uhalifu, udhibiti wa madereva wazembe, pamoja na kuondoa vyombo vya moto visivyokidhi viwango vinavyosababisha ajali barabarani.

Bashungwa amelitaka Jeshi la Polisi kushirikiana na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kubaini maeneo hatarishi katika barabara kuu ambazo zimekuwa zikiripotiwa kusababisha ajali mara kwa mara, ili yafanyiwe upembuzi yakinifu na kutengewa bajeti kwa ajili ya kutafutiwa suluhisho la kudumu.
Katika hatua nyingine, Bashungwa amelitaka Jeshi la Polisi kuendelea kushirikiana na madereva wa pikipiki (boda boda) kwa kukutana na viongozi wao katika ngazi ya wilaya na mikoa ili kuwapa elimu ya usalama barabarani na kuweka mikakati ya pamoja ya kupunguza ajali nchini.

Kadhalika, Bashungwa ameviagiza vyombo vyote vya usalama vilivyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuendelea kushirikiana katika kuimarisha amani, usalama na utulivu, hasa katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 na baada ya uchaguzi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura, ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kudumisha amani na utulivu, huku akiwatoa hofu Watanzania kwa kuwahakikishia kuwa nchi ipo salama na itaendelea kuwa salama.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, amesema kuwa kituo cha Polisi cha Wilaya ya Siha kimejengwa kwa fedha za Serikali kupitia Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na michango ya wananchi wa wilaya hiyo.
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI WA TANZANIA. HAJUI MAANA YA AMANI YA NCHI
INASHANGAZA SANA
 
Wameacha kujiandaa kuwasaidia CCM kuiba kura katika uchaguzi ambao hautokuwepo bali igizo liitwalo uchaguzi?

Wameacha kufuatilia majizi yaliyotajwa kwenye ripoti ya CAG.?
 
Huyo jamaa alikuwa mtu smart, nini kimempata?
IMG_1918.jpeg
 
Back
Top Bottom