Waziri Bashungwa: Tunafanya uchambuzi wa taasisi za Dini zinazofanya kazi kinyume na utaratibu

Waziri Bashungwa: Tunafanya uchambuzi wa taasisi za Dini zinazofanya kazi kinyume na utaratibu

Mungu nipe uvumilivu mengine niyapite tu kama sijayasikia vile. Sikatai juu ya uwepo wa utitiri wa Mkanisa na mambo ya ajabu tokea humo, ila tunayasajili wenyewe na kwenye malengo ya kibajeti tunajiwekea makadirio ya kupata pesa toka huko kwenye usajiri wake. Cheki and balance. Muda wa Bashungwa kama waziri sio mwingi sana, lakini kwa kipindi kifupi kilichobaki nakuona ukiiumiza wakiristo wenzako wengi tu, na hata raia wa kawaida kutia vyombo vilivyo chini yako.

Waharifu ni wengi sana, lakini wako salama zaidi kuliko raia wema wa nchi hii katika uongozi wako. Nimejikuta namkumbuka Lyatonga Mrema (R.I.P) akiwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi.
Bashungwa ni mtu katili kama alivyo maza
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amesema Serikali inaenda kufanya uchambuzi vizuri kuhusu taasisi na Watu wanaofanya huduma za kidini bila kujisajili.

Amesema hayo wakati akizungumza baada ya wasilisho la Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26 Bungeni Jijini Dodoma, Mei 26, 2025.
Hapo kikubwa zile taasisi zinazoenda kinyume na msimamo wa serikali...
 
Hii ni sahihi hawa wanaojiita manabii wamekua wengi sana,kila mtu akiamka anasema kaoteshwa 😀😀😀
Yaani ni vurumai,badala Waombee Nchi wao ni kuoteshwa tu


Hapa serikali wapo sahihi,wadhibitiwe
 
Walianza kumuiga Mu7, sasa wamehamia kwa Kagame... Mdogo mdogo nchi ya Syria ile pale.
 
Ila kusifia serikali sio kwenda kinyume na utaratibu 😂
 
Unafanya na nani? Mnajitengezea anguko.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amesema Serikali inaenda kufanya uchambuzi vizuri kuhusu taasisi na Watu wanaofanya huduma za kidini bila kujisajili.

Amesema hayo wakati akizungumza baada ya wasilisho la Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26 Bungeni Jijini Dodoma, Mei 26, 2025.
IMG-20250603-WA0009.jpg
 
Back
Top Bottom