Waziri Bashungwa: Tunafanya uchambuzi wa taasisi za Dini zinazofanya kazi kinyume na utaratibu

Waziri Bashungwa: Tunafanya uchambuzi wa taasisi za Dini zinazofanya kazi kinyume na utaratibu

Tengeneza tatizo, tatua tatizo...

Yanapoanzishwa huwa wanayaona, yanakua makubwa wanayaona...
 
Huyu Bashungwa tayari, anazidi kujiharibia tu, na alivyo mpole akija kushtuka watu wameishachukua nafasi
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amesema Serikali inaenda kufanya uchambuzi vizuri kuhusu taasisi na Watu wanaofanya huduma za kidini bila kujisajili.

Amesema hayo wakati akizungumza baada ya wasilisho la Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26 Bungeni Jijini Dodoma, Mei 26, 2025.
Kumwombea Tundu Lissu ni kosa?
 
Huyu jamaa ni one of the biggest BOGUS, ila kuna watu wanamtabiria Urais. Kama TAIFA , lipo kwenye hali mbaya sana. Ila it is good thing , mambo lazima yaharibike ili yakae sawa
 
Huyu jamaa kajiharibia sana heshima na sifa aliyokuwa nayo miongoni mwa watanzania wenye akili timamu.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amesema Serikali inaenda kufanya uchambuzi vizuri kuhusu taasisi na Watu wanaofanya huduma za kidini bila kujisajili.

Amesema hayo wakati akizungumza baada ya wasilisho la Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26 Bungeni Jijini Dodoma, Mei 26, 2025.
Ni vizuri ingawa wanachelewa kufanya hivyo. Kanisa sijui ya yule mwanamke anajiita mfalme Zumaridi ile unaweza kuiita kanisa? Mashetani yamejificha kwenye makanisa
 
Ni muda wa dini zote kuungana against huu upuuzi.
 
Kwa hiyo wanataka kuwalazimisha watu wa Mungu waombe mabalaa yasiendelee kutokea au ni mimi sijaelewa? Kwa nini hawa viongozi wa kiserikali wasiache kuyafanya hayo mambo dhulumati ambayo husababisha watu wa Mungu kuoteshwa? Hilo ndilo suluhisho, ndoto zitaendelea maana ndivyo Mungu anavyoongea na watu wake... kama hawataki, Mungu atawapiga nyundo kama la Farao wa Misri....
Kanisa siyo jukwaa la kumtukana mkuu wa nchi, si mahala pa kupandikiza na kueneza chuki acheni serikali ifanye kazi yake.
 
Gwaji boy kawapiga spana za kutosha mnatafuta pa kutokea, mnajitia aibu tuu, solution acheni utekaji na mauaji ya msiokubaliana nao
 
Mungu nipe uvumilivu mengine niyapite tu kama sijayasikia vile. Sikatai juu ya uwepo wa utitiri wa Mkanisa na mambo ya ajabu tokea humo, ila tunayasajili wenyewe na kwenye malengo ya kibajeti tunajiwekea makadirio ya kupata pesa toka huko kwenye usajiri wake. Cheki and balance. Muda wa Bashungwa kama waziri sio mwingi sana, lakini kwa kipindi kifupi kilichobaki nakuona ukiiumiza wakiristo wenzako wengi tu, na hata raia wa kawaida kutia vyombo vilivyo chini yako.

Waharifu ni wengi sana, lakini wako salama zaidi kuliko raia wema wa nchi hii katika uongozi wako. Nimejikuta namkumbuka Lyatonga Mrema (R.I.P) akiwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi.
Hili nalo lina udini?..weeh unakumbuka lyatonga alimfanya nini Mchungaji Mtikila alivyosema kuhusu magobachori?
 
Back
Top Bottom