Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
VIJANA ACHENI MAISHA YA GHARAMA KUBWA MKIPATA FURSA ZA AJIRA: BASHUNGWA
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amewasihi vijana wenye taaluma za Kihandisi kujipanga, kuwa na subira pamoja na utayari wa kujitoa, sambamba na kuacha kuishi maisha ya gharama kubwa na yenye tamaa mara tu wapatapo fursa kwani kufanya hivyo kutadumaza taaluma yao na kushindwa kuendelea kiuchumi.
Bashungwa ameeleza hayo jijini Dodoma wakati akizungumza kwenye mkutano wa mwaka wa Mafundi sanifu ambapo amesema kuwa Serikali itahakikisha miradi yote yenye kilomita chache inatengwa na kutekelezwa na Makandarasi wa ndani hasa vijana ili kuwakuza kiuchumi na kitaaluma.
“Sifurahishwi kuona barabara ina kilometa 10 au 20 inasimamiwa na msimamizi kutoka nje ya nchi, nataka kuona Kesho iliyo Bora ‘Build Better Tomorrow’ kwa vijana yenye mfanano kwa Sekta ya Ujenzi ambapo tutatenga baadhi ya miradi na itakuwa chini ya uangalizi maalum”, amesema Bashungwa.
Aidha, Bashungwa ametoa rai kwa vijana hao kutumia fursa ya kujiajiri na kuanzisha kampuni zao pamoja na kuzisajili katika Bodi za Usajili wa Wahandisi na Wakandarasi (ERB na CRB) ili iwe rahisi kutambuliwa na kupewa kipaumbele.